Trapped in Oman - BBC Africa Eye documentary
View: https://m.youtube.com/watch?v=fJTh4Gdn_B8
Wakipewa ahadi kemkem kuwa ajira za ndani nchini Oman zitabadilisha maisha yao, lakini mara wakifika huko hupokonywa hati zao za kusafiria na mikataba.BBC Africa Eye investigates the plight of Malawian women lured to Oman with offers of domestic work, only to be trapped in a cycle of exploitation, with little hope of escape.
Baada ya hapo hufanyishwa kazi masaa mengi, kufanyiwa ukatili wa kijinsia na hushindwa kuondoka maana passport zao hushikiliwa na waajiri katili na pia huwekewa kigezo na masharti kuwa kuuvunja mkataba wa kazi lazima wawalipe waajiri wao kitita cha fefha kabla ya kuruhusiwa kuondoka ...
Kufuatia vitendo hivyo vinavyofananishwa na kuwageuza wafanyakazi kuwa 'watumwa', BBC News Africa imefanya uchunguzi na kuongea na wahanga pia watetezi wa haki za binadamu waliooingilia kati na kuripotiwa kulipa maelfu ya pesa sarafu ya Rial ya Oman kuwakomboa wafanyakazi wa ndani wanaotesa na baadhi ya waajiri makatili ili waachikliwe huru kurudi nyumbani.
Hii ni sawa na biashara haramu ya kusafirisha binadamu kwa mawakala kuwahadaa wafanyakazi za ndani mishahara minono Oman lakini wengine wanaishia kudhalilishwa, kubaka, kupigwa na waajiri wao bila kupata msaada wowote toka kwa mawakala waliowashawishi kusafiri kwenda Oman kufanya kazi za ndani ....
Asasi maalum (charity) imejitokeza kuokoa wafanyakazi waliojikuta katika hali ngumu nchini Oman, na tayari kazi zake zimetambuliwa na watetezi wa haki za binadamu. Serikali ya Malawi nayo imejitosa kuwaokoa baadhi ya raia wake na kuiomba asasi hiyo kusaidia raia wake waweze kuachiwa na waajiri makatili, ili warudi nyumbani ...
Oman kuna wimbi kubwa la wafanyakazi wa kutoka nchi za Afrika kama Malawi, Kenya, Uganda, Tanzania n.k waliopelekwa huko na mawakala huku kukipatikana habari baadhi ya wafanyakazi hao wanapitia magumu na serikali za baadhi ya nchi za kiAfrika kujaribu kuweka mifumo ya ufuatiliaji wa hali za raia wao zipo vipi ......
Source: BBC News Afrika