Afya ya Lwakatare YAZOROTA

Afya ya Lwakatare YAZOROTA

Acheni double Standard...
Sheikh Ponda ana Tuhuma za Kuiba Mbao na Kuvamia Kiwanja yupo ndani karibia mwezi wa Tano sasa..na mnashibikia aendelee kukaa ndani
Lwakatare ana tuhuma za Ugaidi ..yupo ndani siku mbili tu ..mnaanza kupiga kelele anaonewa
 
Pole sana Kamanada,

Poleni sana viongozi wa CDM,

Poleni sana Familiya na ndugu wa Kamanda.

Serikali wajue kuwa kamwe haitasaidia kudhoofisha upinzani kwa stahili hii.

Njia ya kudhoofisha upinzani ni kuleta maendeleo na kutatua kero mbalimbali za wananchi ndipo wataikubali serikali.

Lakini kwa mpango huu, ndio kwanza wanamwagia petrol katika moto.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Tumuombe uzima na salama, maana mahabusu za polisi wetu na baadhi ya mbinu chafu za mahojiano, Mungu bariki Rwakatare sio tuu ni public fugure, bali pia anazijua hakizake mikononi mwa polisi!, angekuwa ni mwenzangu za mimi, saa hizi angekuwa umekwisha sema kila kitu!.

Pamoja na yote, mimi nimeiangalia clip ile na kujiridhisha ni "bonafide genuine!".

Pasco.

Wewe mwanajeshi mstaafu una lako jambo. Clip kuwa geniune HAIMAANISHI kuwa Lwakatare ndio mhusika. Narudia tena HAIMAANISHI kuwa yeye ni mhusika. Ni lazima tujue kwanza mazingira ya kurekodiwa kwake na ni nina ameiweka you tube. Inawezekana kabisa alirekodiwa ki-ukweli halafu watu wengine wenye nia zao chafu wakaamua kuitumia kutekeleza malengo yao. Bado nina wasiwasi na:
1. Ile story ya chuo cha kiislam iliyotolewa na Mtanzania.
2. Kebehi ya mtu anayejiita Ridhiwani aliyoitoa mara baada ya Kibanda kushanbuliwa
3. Ridhiwani wa ukweli kusema eti account yake ilikuwa hacked.
Je hivi vitu vinaweza kuwa na uhusiano?
 
SIRI ya Kibanda, Lwakatare zafichuliwa rasmi
 
...we Pascal Mayalla...sipendi sana ku comment issue za siasa majitaka za kibongo..lakini napoona mtu anapotosha waziwazi nashindwa kuvumilia...achana na haya mambo.....wewe si forensic expert..na wala si lawyer...wewe ni kanjanja tu mganga njaa tz.......
Mkuu Nderi, nakubali yote kwa moyo mweupe tena bila kinyongo chochote, mimi Pasco wa jf si lawyer, ni kanjanja tuu mganga njaa tz!. Tuwasubiri watu wa forensic ndio wathibitishe!, kumbe hata video na sauti inathibitishwa kwa vinasaba!, na tusubiri!.

Kama una uhakika wa karatasi ni jeupe na unalishuhudia kwa macho kuwa ni jeupe, mtu akilazimisha kuwa ni jeusi kwa matumaini ya kusubiri uthibitisho kuwa ni jeusi, then utasubiri kwa hamu, ila uthibitisho ukishapatikana na kuthibitisha ni jeupe, utamkumbuka yule mliobisha naye!.

..waachie watu wenye jukumu la kuifanya hiyo kazi wafanye....vinginevyo ukiendelea kudai video ni ya kweli tutasema imetengenezewa kwenye studio yako ya PPR...goddam!
 
Tumuombe uzima na salama, maana mahabusu za polisi wetu na baadhi ya mbinu chafu za mahojiano, Mungu bariki Rwakatare sio tuu ni public fugure, bali pia anazijua hakizake mikononi mwa polisi!, angekuwa ni mwenzangu za mimi, saa hizi angekuwa umekwisha sema kila kitu!.

Pamoja na yote, mimi nimeiangalia clip ile na kujiridhisha ni "bonafide genuine!".

Pasco.

Adui..............!
 
Kweli wewe ni Songoro na akili yako ni kisongorosongoro unafananisha vitu viwili tofauti, kwa nini polisi itegemee video zilizowekwe kwenye blog za kijamii? Kama utaalamu wao ndo huo basi hatuna jeshi la polisi bali wote ni raia na hakuna mwenye mafunzo ya upelelezi hapo. Wewe kinachokufurahisha na kushabikia huyo bwana ashikiliwe na polisi kwa ushahidi dhaifu kama huo wa film. Inaelekea wewe ni sehemu ya wauaji ndiyo maana unafurahia mateso kwa wenziyo. Namalizia kwa kukwambia kwamba Tanzania bila sisiemu inawezekana tena sana, kwa vile wewe au wazazi wako wanajinufaisha kwa jasho na maisha magumu kwa watanzania basi unaona hayo ndiyo maisha ujue ipo siku na wewe utateseka tu. machozi ya walalahoi yatawageuka tu
 
JUMAMOSI, MACHI 16, 2013 05:46 NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

*Washindwa kumfikisha mahakamani

JESHI la Polisi nchini, jana limeshindwa kumfikisha mahakamani Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.

Hatua hiyo, ilionekana kuwachefua mawakili wa Lwakatare, ambao walifika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam, kwa ajili ya kumwekea dhamana.

Mawakili hao, walidai Jeshi la Polisi linaongoza kwa kuvunja sheria za nchi kwa kumshikilia mteja wao kwa siku tatu, bila kumfikisha mahakamani.

Mawakili hao, Tundu Lissu, Profesa Abdalaah Safari na Peter Kibatala, walitoa malalamiko hayo baada ya kusota siku nzima wakimsubiri mteja wao afikishwe mahakamani.

Akizungumza kwa niaba ya mawakili wenzake, Lissu alisema sheria inasema mtu akishikiliwa na polisi, anatakiwa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24, kinyume cha hapo ni uvunjifu wa sheria.

"Tangu asubuhi tuko hapa mahakamani, tulidhani wamemaliza uchunguzi wao watamfikisha mahakamani, hii ni makusudi kabisa ili wamweke rumande hadi Jumatatu…kisheria hawaruhusiwi kukaa na mtuhumiwa kwa siku tatu, wanatakiwa kumfikisha mahakamani ndani ya saa 24.

"Jeshi la Polisi Tanzania, wanafikiria sheria za nchi hii haziwahusu, wanaona wanaweza kumshikilia mtu wanavyotaka wao, hawa ndio chanzo cha ukiukwaji wa sheria za nchi.

"Nilimuuliza afande Kigondo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kujua wanafuata sheria zipi kukaa na mtuhumiwa siku zote hizo, alinijibu kwamba yeye ni mpelelezi tu, nimuulize afande Isaya Mangulu.

"Nimemuuliza Mangulu, ananijibu kwamba anayehusika ni Kigondo, lakini baadaye akanipigia simu na kuniambia hataletwa mahakamani, upelelezi bado unaendelea," alisema Lissu.

Lissu, alisema inaonekana wazi polisi hawajui kwa nini wanaendelea kumshikilia Lwakatare.

Alisema tuhuma zinazomkabili, zinaonekana wazi kuwa za mambo ya kisiasa zaidi.

Aliongeza kuwa, kama itafika Jumatatu bila kumpeleka mahakamani, watafanya utaratibu wa kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, ili kujua jeshi hilo, linatumia sheria gani kushikilia mtuhumiwa.

"Nawaambia Lwakatare hajafanya kosa lolote na hao wanaosema na kufikiria hivyo, walete ushahidi mahakamani tupambane.

"Haya ni maneno ya kina Mwigulu Nchemba (Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara), anayetangaza katika vyombo vya habari kwamba viongozi wa CHADEMA, wanapanga mauaji kama hayo, ndiyo yamefanya Lwakatare ashikiliwe na Polisi, nawaambia wajiandae sawa sawa," alisema Lissu.

Wakili Profesa Safari, akichangia hilo alisema, polisi wako kinyume na kifungu cha sheria namba 32 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, hivyo wanatakiwa kumpa dhamana mtuhumiwa ili kuepuka kujiaibisha.

"Tunamwambia IGP Said Mwema, wasijiaibishe, wampe dhamana Lwakatare, kwanza ni mgonjwa wa sukari wanataka kuhatarisha maisha yake," alisema Profesa Safari.

Lwakatare alikamatwa Jumatano asubuhi, kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya mashambulizi dhidi ya watu hapa nchini.

Taarifa kutoka ofisi za makao makuu ya CHADEMA Kinondoni jijini Dar es Salaam, zinasema Lwakatare alikamatwa saa 7 mchana na watu wanne waliojitambulisha kama maofisa wa Jeshi la Polisi, ambao walifika na gari aina ya Toyota Land Cruiser jeupe lenye namba za usajili T 140 BLA, likiwa na chata ya kitalii.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senso alisema Lwakatare amekamatwa kwa sababu ya kupanga mikakati mbalimbali ya kushambulia na kudhuru watu mbalimbali wakiwamo waandishi wa habari.

Huyo anatakiwa afie huko huko asitoke watu walikuwa wanashabikia hapa Masuala ya akina shekhe Ponda leo yamewafika wanaanza kulia lia, Ugaidi na dhamana wapi na wapi?

Ugaidi unauona kwenye film iliyowekwa kwenye YOU TUBE? Kwa nini munapenda kuongelea kesi ya Ponda hapa? Sioni kufanana kwa haina yoyoye kati ya makosa yanayomkabili Ponda na huyu Lwakatare. Acheni chuki za mambo yenu, kaziongelee huko huko kwenye vikundi vyenu.
 
Pasco, unadhani unajua kweli kumbe kisheta na poyoyo! Au ndo part of the scheme in order to derange our retrieving mind. If its bonafide genuine, why dont they take him to court?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nderi, nakubali yote kwa moyo mweupe tena bila kinyongo chochote, mimi Pasco wa jf si lawyer, ni kanjanja tuu mganga njaa tz!. Tuwasubiri watu wa forensic ndio wathibitishe!, kumbe hata video na sauti inathibitishwa kwa vinasaba!, na tusubiri!.

Kama una uhakika wa karatasi ni jeupe na unalishuhudia kwa macho kuwa ni jeupe, mtu akilazimisha kuwa ni jeusi kwa matumaini ya kusubiri uthibitisho kuwa ni jeusi, then utasubiri kwa hamu, ila uthibitisho ukishapatikana na kuthibitisha ni jeupe, utamkumbuka yule mliobisha naye!.

Pasco.

Pasco,

kunasiku nitakukumbusha,Ehe Mungu Wa Israel,Simama mwenyewe.
 
Pasco, unadhani unajua ukweli kumbe kisheta na poyoyo! Au ndo part of the scheme in order to derange our retrieving mind. If its bonafide genuine, why dont they take him to court?
 
Last edited by a moderator:
Tulitegemea Jeshi liwe dogo, na la kisayansi, kama tulivyoahidiwa na mkuu wa kaya, na siyo jeshi lisiloweza kupambanua propaganda za kisiasa na mchezo wa kiteknolojia. Hapa kazi ni kwako!!!!!
 
ovyo.... huyu senzo ni ndugu yangu ila simuhitaji kuanzia leo......nakutangazia leo.
 
Back
Top Bottom