Afya ya Lwakatare YAZOROTA

Afya ya Lwakatare YAZOROTA

Mchemba ni DOA kwenye SIASA za NCHI HII..

unakosea- Nchemba ni fuata upepo ili ajaze tumbo lake, tatizo la nchi hii ni bosi mkuu watu walikuwa hawajua rangiyake halisi lakini kwa sasa hata mtoto wa nasery anajua anateswa na nani
 
Ugaidi unauona kwenye film iliyowekwa kwenye YOU TUBE? Kwa nini munapenda kuongelea kesi ya Ponda hapa? Sioni kufanana kwa haina yoyoye kati ya makosa yanayomkabili Ponda na huyu Lwakatare. Acheni chuki za mambo yenu, kaziongelee huko huko kwenye vikundi vyenu.

gaidi si lazima akamate usukani wa ndege na kwenda kugongesha ndege WTC..Hata ukiwa masterminder tena ndo unapata adhabu kubwa kuliko waliofanya huo ugaidi.
 
ama kweli!kwani wao wajinga hawajuhi Rwaka hana hatia ya kumpeleka kisutu ..wanajua sema ni kuwapotezea focus CDM
 
Wana chademaaaaaa, naona ngumu kumeza safari hii.

Mtuhumiwa kwenye huu mkakati wa umafia angekuwa kiongozi wa CCM najua mngeandamana mwaka mzima!
 
unakosea- Nchemba ni fuata upepo ili ajaze tumbo lake, tatizo la nchi hii ni bosi mkuu watu walikuwa hawajua rangiyake halisi lakini kwa sasa hata mtoto wa nasery anajua anateswa na nani

siamin kama jeshi la polisi hawana vifaa vya kisasa vya kuweza kutambua jins technolojia inavyoweza kuhatalisha amani ya nchi, kama ni hvyo basi IGP Mwema bado anaendesha jeshi kwa ku2mia technologia ya karne ya 18
 
Mkuu Nderi, nakubali yote kwa moyo mweupe tena bila kinyongo chochote, mimi Pasco wa jf si lawyer, ni kanjanja tuu mganga njaa tz!. Tuwasubiri watu wa forensic ndio wathibitishe!, kumbe hata video na sauti inathibitishwa kwa vinasaba!, na tusubiri!.

Kama una uhakika wa karatasi ni jeupe na unalishuhudia kwa macho kuwa ni jeupe, mtu akilazimisha kuwa ni jeusi kwa matumaini ya kusubiri uthibitisho kuwa ni jeusi, then utasubiri kwa hamu, ila uthibitisho ukishapatikana na kuthibitisha ni jeupe, utamkumbuka yule mliobisha naye!.

Pasco.
Njaa itakuua Pasco.
 
Wana chademaaaaaa, naona ngumu kumeza safari hii.

Mtuhumiwa kwenye huu mkakati wa umafia angekuwa kiongozi wa CCM najua mngeandamana mwaka mzima!
Kwa mtu yeyote mwenye akili anajua kinachoendelea, hii movie ya Lwakatare ilishaongelewa na Nchemba, na Nchmba hayo maelezo alipewa na Ikulu kuyasema na huo ni katika mkakati wa TISS ambao unaratibiwa na Ikulu kuhakikisha kuwa CDM inasambaratika!

Hivi kama ni kweli jeshi la Polisi lingekuwa linafanya shughuli zake kitaaluma na siyo kwa maagizo toka Ikulu lingeweza kweli hadi leo kushindwa kuwatia mbaroni watu waliomteka Dr Ulimboka?!

Hata ukiangalia issue nzima ya Lwakatare lengo kuu ni kutaka kuwatwist wananchi ili wasiwajue wahusika wakuu wa skandali ya Kibanda ambao ni vyombo vyetu vya ulinzi na usalama!!
 
kuwepo
Njaa itakuua Pasco.
Mkuu Mrejesho, kama issue ni njaa, then I would have done what pays off most!. Kitendo cha mimi kuendelea kuwepo kwenye fani hii ambayo doesn't pay at all, ni uthibitisho tosha kuwa I'm doing this job for the love of it and not to make money. Sasa hii njaa ya kuniua ni njaa gani hii?!, unless na wewe unaamini kuna watu are paid ku post humu jf, then I must be filthy rich!.
Pasco
 
Huyo anatakiwa afie huko huko asitoke watu walikuwa wanashabikia hapa Masuala ya akina shekhe Ponda leo yamewafika wanaanza kulia lia, Ugaidi na dhamana wapi na wapi?

Sheikh Faridi naye alikuwa na sukari kama Lwakatare lakini wadau wakawa wanasema asipewe dhamana.

Ila hii ya sukari ya Lwakatare kwa vile ni mkuu wa CHADEMA, serikali haitendi haki?

Kweli nimeamini sio kwamba CHADEMA inatetea wanyonge na haki ila inatetea inaowajua tu.
 
Naamini Lwakatare anashikiliwa kwa amri ya ikulu vinginevyo pilisi wa nchi hii kwa rushwa wangekwishamuachia kwa kutoa kitu kidogo, vituo vyote vya polisi hapa nchini kama una hela hukai selo.

Kwa upande wa ubabe wa usalama wa taifa kama mnalinda maslahi yenu kwa njia hii, jiulize libya, misri na kwingineko kulikokuwa na tawala za udikteita kulikalika baada ya wenye nchi kuchoka?
 
Tumuombe uzima na salama, maana mahabusu za polisi wetu na baadhi ya mbinu chafu za mahojiano, Mungu bariki Rwakatare sio tuu ni public fugure, bali pia anazijua hakizake mikononi mwa polisi!, angekuwa ni mwenzangu za mimi, saa hizi angekuwa umekwisha sema kila kitu!.

Pamoja na yote, mimi nimeiangalia clip ile na kujiridhisha ni "bonafide genuine!".

Pasco.

kuangalia huwa hakuhusishi ubongo rudi ukaitazame.
 
Wana chademaaaaaa, naona ngumu kumeza safari hii.

Mtuhumiwa kwenye huu mkakati wa umafia angekuwa kiongozi wa CCM najua mngeandamana mwaka mzima!
Na hata wengi mnaopost humu kushangilia kukamatwa kwa Lwakatare kwa issue ya Kibanda nyinyi mtakuwa watu wa TISS mnaopokea maelekezo toka Ikulu, jambo la hatari zaidi mmejigeuza toka usalama wa Taifa ulivyokuwa enzi za Nyerere na hivi sasa mmegeuka kuwa ni wana usalama wa CCM ambapo mmejiapiza kuwa kwa vyovyote vile mtahakikisha CCM hawapndoki madarakani hata kama wananchi wa nchi hii asilimia 90 watawakataa kwenye sanduku la kura!!

Kwa mazingira tunayoyaona sasa, nchi hii inakabiliwa na hatari kubwa sana ya kuingia kwenye machafuko kutokana na TISS na Jeshi lake la Polisi kujitokeza waziwazi na kufanya kila wanaloweza kutaka kuiokoa CCM ambapo sasa ni dhahiri kabisa chama hicho kinaelekea kuzimu!!

Kwa hali tuliyofikia nchi hii kwa sasa wananchi wote tunapaswa kufanya maombi kwa Mungu ili aweze kulinusuru Taifa hili na hatari ya dhahiri ya kuangamia kwa raia wake wasio na hatia.
 
Tupa ndani nyang'au huyo! Kama kosa la Kuvamia kiwanja mtu yupo ndani zaid ya miezi 5 seuze la umafia? Awe na kisukari au kichumvi haituhusu, Tanzania bila ya Ulwakatare inawezekana, iyo safari imeanza wasakwe mpaka wanaojianya wako bize shinyanga mpaka watambue kuwa ncha ya Mkuki haipigwi kichwa!

Mkuki kwa NGURUWE kwa BINADAMU ni MCHUNGU!... Agosti mwaka jana Shehe ILUNGA katoa maagizo wakristo wauawe!... Leo anapeta!... kwa SABABU tu anatoka dini ya wakubwa wa nchi!.. Lwakatare (mkristo) kakamatwa waislamu mnashangilia!.
 
Sheikh Faridi naye alikuwa na sukari kama Lwakatare lakini wadau wakawa wanasema asipewe dhamana.

Ila hii ya sukari ya Lwakatare kwa vile ni mkuu wa CHADEMA, serikali haitendi haki?

Kweli nimeamini sio kwamba CHADEMA inatetea wanyonge na haki ila inatetea inaowajua tu.

Agosti mwaka jana Shehe ILUNGA katoa maagizo wakristo wauawe!... Leo anapeta!... kwa SABABU tu anatoka dini ya wakubwa wa nchi!.. Lwakatare (mkristo) kakamatwa waislamu mnashangilia!.
 
Tumuombe uzima na salama, maana mahabusu za polisi wetu na baadhi ya mbinu chafu za mahojiano, Mungu bariki Rwakatare sio tuu ni public fugure, bali pia anazijua hakizake mikononi mwa polisi!, angekuwa ni mwenzangu za mimi, saa hizi angekuwa umekwisha sema kila kitu!.

Pamoja na yote, mimi nimeiangalia clip ile na kujiridhisha ni "bonafide genuine!".

Pasco.

Pasco, itakapogundulika tofauti au Polisi watakapoamua kucheza picha la kihindi kwenye 'mashitaka' ya Lwakatale uje tena hapa kutupa your 'bonafide genuine opinion'.
 
Last edited by a moderator:
Na hata wengi mnaopost humu kushangilia kukamatwa kwa Lwakatare kwa issue ya Kibanda nyinyi mtakuwa watu wa TISS mnaopokea maelekezo toka Ikulu, jambo la hatari zaidi mmejigeuza toka usalama wa Taifa ulivyokuwa enzi za Nyerere na hivi sasa mmegeuka kuwa ni wana usalama wa CCM ambapo mmejiapiza kuwa kwa vyovyote vile mtahakikisha CCM hawapndoki madarakani hata kama wananchi wa nchi hii asilimia 90 watawakataa kwenye sanduku la kura!!
Kwa mazingira tunayoyaona sasa, nchi hii inakabiliwa na hatari kubwa sana ya kuingia kwenye machafuko kutokana na TISS na Jeshi lake la Polisi kujitokeza waziwazi na kufanya kila wanaloweza kutaka kuiokoa CCM ambapo sasa ni dhahiri kabisa chama hicho kinaelekea kuzimu!!

Kwa hali tuliyofikia nchi hii kwa sasa wananchi wote tunapaswa kufanya maombi kwa Mungu ili aweze kulinusuru Taifa hili na hatari ya dhahiri ya kuangamia kwa raia wake wasio na hatia.

Wewe lazima utakuwa na PhD. Kama huna basi walimu wako wa chuo watakuwa walikubania tu. Hapo kwenye red 100% ndilo jibu la kweli.
 
Back
Top Bottom