Afya ya Lwakatare YAZOROTA

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
lwakatare.jpg


Mkuu wa Usalama na Ulinzi wa Chadema, Wilfred Lwakatare

Na Beatrice Moses, Mwananchi

Hali ya afya ya Mkuu wa Usalama na Ulinzi wa Chadema, Wilfred Lwakatare anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwahamasisha watu kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kupitia mitandao ya jamii, imezorota.

Gazeti hili imemshududia jana akizungumza na wakili wake Nyaronyo Kicheere, huku akilalamikia hali yake kuwa si njema kutokana na ugonjwa wa kisukari alionao.

Alikuwa akitembea kwa kujivuta, na alidai kuwa ameshindwa kula chakula inavyotakiwa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, wakili Kicheere alisema amehangaika sana katika kuhakikisha kuwa mteja wake anapata dhamana lakini imeshindikana, hali ambayo inamtia hofu kutokana na hali aliyomwona nayo.

"Mteja wangu ni mgonjwa wa kisukari, kwa kawaida hutakiwa kula chakula na kunywa maji mengi, lakini nimehangaika sana, leo (jana) nilikuwa na matumaini kwamba atapelekwa mahakamani ambapo nilijipanga kwa kuandaa watu makini wenye hati za nyumba nikiwa na imani kwamba angepata dhamana, lakini wamemrudisha mahabusu," alisema Kicheere.

Kicheere muda mwingi alionekana kuhaha kuwasiliana na viongozi wa Chadema kwa simu yake ya mkononi, pamoja na kuwasiliana na baadhi ya wanasheria akiwamo Tundu Lissu na Peter Kibatala ambao walijipanga katika kuhakikisha kuwa wanapata wadhamini watakaoweza kumdhamini Lwakatare.

Wakili huyo alisema kuwa kinachotendeka kwa mteja wake ni kinyume cha sheria kwa kuwa ni tuhuma ndizo zimemfanya akamatwe.

Alisema mteja wake ana haki ya kupewa dhamana hasa kwa kuzingatia kuwa saa zaidi ya 24 zimepita na hali yake si njema, na kwamba kuendelea kuwa mahabusu ni kuhatarisha usalama wa afya yake.

Maofisa wa juu kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelelezi wa Makosa ya Jinai, waliwasili Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam ambapo walikutana na wakili Kicheere na mtuhumiwa huyo na kufanya mazungumzo.

Taarifa za kuaminika zilizopatikana awali zilieleza kuwa juzi saa 11 jioni maofisa kadhaa wa polisi, walimchukua mtuhumiwa huyo na kwenda naye nyumbani kwake wakiwa na lengo la kufanya upekuzi kwa mara ya pili lakini juhudi zao ziligonga mwamba baada ya kutokuwa na kibali cha upekuzi.

"Wakili wake anawabana maofisa wa polisi akitaka wafanye kazi zao kwa mujibu wa sheria hivyo juzi hawakuweza kuingia ndani, pia walizuiwa na wakili huyo huyo kumhoji kwa kumrekodi kwa video, ambapo kulitokea hali ya majibishano ya kisheria, lakini hatimaye akahojiwa bila kurekodiwa," kilieleza chanzo cha habari.

Lwakatare alikamatwa Jumatano ya wiki hii katika makao makuu ya chama hicho na tangu siku hiyo anaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano.
 
Zile chafya, mafua na kuvuja kwa makamasi kwenye ile video, ni ishara tosha kwamba yule mjomba afya yake ni mgogoro mtupu. Ni vyema serikali ikawa makini na watu wenye afya mbovu kama yule na ikibidi awekwe katika cell ambayo hatachanganyika na wengine. Au ni vizuri zaidi kama aliruhusiwa kuishi nyumbani kwake huku akiwa chini ya ulinzi na polisi wamuone tuu pale wanapotaka kumsaili.
 
Polisi yaibua utata sakata la Lwakatare

• Video yake yaacha maswali mengi mtandaoni

na Mwandishi wetu|Tanzania Daima

WAKATI Jeshi la Polisi likiendelea kumshikilia na kumhoji Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, baadhi ya wananchi wameonyesha wasiwasi na jeshi hilo katika kushughulikia matukio ya kihalifu nchini.

Lwakatare alikamatwa juzi makao makuu ya chama hicho, kisha kuhojiwa na kupekuliwa nyumbani kwake kwa tuhuma za uchochezi na uvunjifu wa amani nchini.
Kada huyo ambaye anahusishwa na picha ya video iliyosambazwa kwenye mtandao ikimwonyesha akipanga mikakati na kuwaelekeza watu ambao sura zao hazionekani kufanya matukio ya kumteka mtu ambaye hatajwi kwa jina, kwa siku ya pili jana aliendelea kuhojiwa na kupekuliwa.

Hata hivyo, hatua hiyo ya Jeshi la Polisi kumkamata haraka Lwakatare na kumhoji kwa kutumia mkanda huo wa video kwenye mtandao imeleta mashaka ambapo baadhi ya watu wanatafsiri kitendo hicho kama mkakati maalumu wa kuichafua na kuidhoofisha CHADEMA.

Wachambuzi hao wa masuala ya kisiasa na watalaamu wa mitambo licha ya kutotaka kulizungumzia suala hilo kwa undani ili wasiingilie kazi ya polisi, walisema inashangaza kuona wepesi wa jeshi hilo katika tukio la Lwakatare wakati wako watuhumiwa wametajwa kuhusika na uhalifu mkubwa hawakamatwi wala kuhojiwa.

Katika orodha hiyo, wanamtaja mtumishi wa Ikulu, Ramadhan Ighondo, ambaye alitajwa na gazeti la MwanaHalisi pamoja na Dk. Stephen Ulimboka mwenyewe kuwa alihusika kumteka na kumtesa kiongozi huyo wa madaktari Juni 26, mwaka huu, lakini hadi leo hakuwahi kuhojiwa na polisi.

"Naibu Katibu Mkuu wa CCM (bara), Mwigulu Nchemba, akihojiwa na kituo cha televisheni cha Star Januari, mwaka huu, alitamka kuwa anayo video inayowaonyesha viongozi wa CHADEMA wakipanga mauaji. Huyu polisi hawakumhoji ili awapatie video hiyo, kwa nini iwe haraka kwa Lwakatare?" alihoji mtoa taarifa.

Wachambuzi hao walitaja mlolongo wa matukio ya kinyama waliyotendewa baadhi ya watu akiwemao Saeed Kubenea, Dk. Ulimboka, marehemu Daudi Mwangosi na sasa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absolam Kibanda, wakisema kuwa jeshi la polisi limeshindwa kuwakamata wahusika wa vitendo hivyo licha ya kujitutumua kuunda kamati za uchunguzi kila yanapotokea.

Waligusia pia mauaji ya raia wasio na hatia waliouawa kwa risasi na polisi kwenye mikutano na maandamano ya CHADEMA halafu uchunguzi wake ukaishia kwenye majibu yasiyowataja wazi wahusika na kuwachukulia hatua.

Kutokana na mtiririko wa matukio hayo pamoja na kejeli za hivi karibuni za mtoto wa Rais Ridhiwan Kikwete na Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye, kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kuhusu sakata la kuteswa kwa Kibanda, wachambuzi hao wanadai huo ni mkakati wa kuidhoofisha CHADEMA.

"Haya hayakuanza leo, huu ni mkakati wa wahuni wachache wanaotumia mwamvuli wa Idara ya Usalama wa Taifa kufanya matendo haya halafu wanahamisha watu kwenye ajenda kwa kutunga mambo tofauti ya kuwabambika watu," kilisema chanzo chetu na kuongeza: "Katika hili vyombo vya habari vinapaswa kushikamana kuhoji uchunguzi wa matukio makubwa umeishia wapi.

Waliomdhuru Kubenea si walijulikana? Wako wapi? La Ulimboka na Mwangosi polisi wameshindwa na sasa hili la Kibanda wanataka kuwahamisha kwenye hoja kwa kukimbilia kuhangaika na Lwakatare."


Video yakosolewa
Katika hatua nyingine, wataalamu wa mitambo ya video wamekuwa wakitoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii kukosoa ukanda wa video unaomuonyesha Lwakatare akidaiwa kupanga mikakati ya kudhuru watu.
Wataalamu hao walitoa sababu kadhaa wakidai kuwa video imechukuliwa Desemba 28, mwaka jana, baada ya sikukuu ya Krismasi bila kama inavyosikika lakini wakahoji kwa nini video ije kutolewa sasa hivi baada ya tukio la kuteswa kwa Kibanda.

Katika sababu ya pili wanasema video imechukuliwa na kamera yenye Mega Pixel zaidi ya 5, na kwamba kamera za siri huwa hazina pixel kubwa kiasi hicho. Ni wazi wahusika walikuwa wanajua kabisa kuwa wanajirekodi.

Wanaongeza kuwa kauli ya Nchemba kuhusu kuwa anayo video ikiwaonyesha viongozi wa CHADEMA wakipanga mauaji ya watu, tangu CHADEMA imtake apeleke video kwenye vyombo vya dola ili wahusika wachukuliwe hatua ni kwa nini hakufanya hivyo.

"Mhusika kuweka hiyo video ‘Bukoba Boy' amejiunga na Youtube Machi 11, mwaka huu, na tarehe hiyo akaweka hiyo video ambayo aliichukua Desemba 28 mwaka jana.
"Je, kama analipenda taifa hili kwa nini asingeweka tangu kabla ya tukio pengine Kibanda angeepukana na hatari hii? Walihoji wachambuzi hao."

Waliongeza kuwa kama kweli polisi ina nguvu kwa nini haijamkamata huyu mtu mpaka sasa hivi kwa kuwa ni hatari kwa taifa.
"Katika dakika ya 16 na sekunde ya 55 ya video hii, Lwakatare anasema ‘ama nilivyopewa na kuichunguza hii changamoto ina maana kuna mtu kamtuma kusema haya maneno, swali je ni nani?" Wanahoji.

Katika dakika ya 17 sekunde ya 32, Lwakatare anasema, "Kama huyu mtu anakuwa na sehemu nyingi sasa tutafuatilia ngapi? Lazima awe na sehemu moja maalumu kuwa hakosi."

Wanaongeza kuwa hivi mtu anayepanga mauaji anachagua sehemu, kwamba mbona Mwangosi aliuliwa kwenye mikono ya polisi; ina maana ndiyo ilikuwa sehemu yake.

Wanahoji kuwa mbona kijana kwenye maandamano ya CHADEMA alikufa ina maana Morogoro kila siku palikuwa na mikutano na hapo palikuwa sehemu yake ya kuuawa?
"Mwisho kwa nini video imekatishwa katikati? Je, kuna matukio mengine yatafanyika halafu ndiyo waje na video ya sita maana hiyo ni video ya tano? Mwanzo kabisa ya video wanarekebisha maiki, na mchukua video anasema, "tuta-‘note' upya hapo.

"Hii ina maana kuna marekebisho ya kubadili kamera yalifanyika hata video inavyoanza tunaona kabisa walikuwa kimya," alisema mtaalamu huyo wa video.

Dk. Slaa afichua mipango
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa amefichua mipango ya Jeshi la Polisi kutumika kisiasa kufanya michezo michafu dhidi ya chama hicho.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Dar es Salaam, alisema kwa mara kadhaa wameripoti polisi matukio mbalimbali kuhusu mbinu chafu walizokuwa wakifanyiwa lakini hakuna hatua iliyochukuliwa.

Alisema hata katika sakata la Lwakatare hashangazwi kwani kiongozi huyo amekuwa akiwindwa kwa muda mrefu kwa kuzushiwa tuhuma mbalimbali.
Dk. Slaa alisema ameisikiliza vizuri video inayomhusisha Lwakatare na tuhuma za uchochezi ambapo kuna mtu anamuuliza maswali elekezi lakini mtu huyo haonekani.

Alisema jeshi la polisi halijawahi kuchukua hatua stahiki kwa suala la mauaji ya Mwangosi kwa kumwajibisha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa aliyesimamia na kufanikisha mauaji hayo.

Hata sakata la Dk. Ulimboka baada ya kuteswa, polisi wameshindwa kumhoji mtuhumiwa anayedaiwa kuwa ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wa Ikulu, ambaye alidaiwa kuhusika.

Dk. Slaa alifafanua kuwa hawezi kushangaa ikiwa jeshi la polisi halitamhoji Kibanda.
Aliongeza kuwa Lwakatare kuhusishwa kwa sakata la sasa la mkanda wa video uliopo katika mtandao ni mwendelezo wa kukihujumu chama, unaoratibiwa na Usalama wa Taifa, huku ukitekelezwa na jeshi la polisi.

"CHADEMA inafahamu kwa undani kwamba uzushi huu wa tepu ya ‘Bukoba Boy' umeanzishwa na kuhusisha Usalama wa Taifa, akiwemo Ighondo na wenziwe pale Ada Estate," alisema.

Hata hivyo alishangazwa na jeshi la polisi kufanya haraka kumshikilia Lwakatare, kwani vyombo vya habari hivi majuzi vimemtaja kwa jina, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuwa alihusishwa na utekwaji na uteswaji wa Kibanda, lakini jeshi halikusema lolote hadi sasa.

"Ridhiwan Kikwete na Nape Nnauye waliingia kwa ID zao kwenye mitandao kukejeli suala la kuteswa Kibanda lakini jeshi halikuchukua hatua, lakini hili la Lwakatare wanafanya haraka kumkamata, hizi ni mbinu tu za kuichafua CHADEMA.

Alisema kuwa mara nyingi wametoa madai kwa Rais aunde Judicial Commission of Inquiry (Tume Huru ya Kimahakama kuchunguza vifo vyote vyenye utata na sura ya kisiasa) lakini hakuna hatua iliyochukuliwa.


 
Tumuombe uzima na salama, maana mahabusu za polisi wetu na baadhi ya mbinu chafu za mahojiano, Mungu bariki Rwakatare sio tuu ni public fugure, bali pia anazijua hakizake mikononi mwa polisi!, angekuwa ni mwenzangu za mimi, saa hizi angekuwa umekwisha sema kila kitu!.

Pamoja na yote, mimi nimeiangalia clip ile na kujiridhisha ni "bonafide genuine!".

Pasco.
 
Inasikitisha kuona wenye hatia na walio ratibu mpango mzima wa utekaji na utesaji wapo huru, na asie na hatia wala makosa anateseka huko mahabusu ni jambo linauma.
 
Pole sana kamanda Mungu akutie nguvu huko uliko ipo siku Neema itaonekana na wananchi wataishi maisha ya amani
 
Tupa ndani nyang'au huyo! Kama kosa la Kuvamia kiwanja mtu yupo ndani zaid ya miezi 5 seuze la umafia? Awe na kisukari au kichumvi haituhusu, Tanzania bila ya Ulwakatare inawezekana, iyo safari imeanza wasakwe mpaka wanaojianya wako bize shinyanga mpaka watambue kuwa ncha ya Mkuki haipigwi kichwa!
 
Yaani huu wa Jeshi letu la Police sijui utaisha lini,kuna watu wametajwa kabisa kua ndio vinara wa mauaji kutoka Ikulu ambapo Rama yupo lakn hahojiwi,Mungu ni Mwema sana CDM tutapita salama kwenye haya mapito
 
Pole sana kamanda Lwakatare hawa wafilisti mwisho wao upo ni siku ambayo tutaingia wenyewe mzigoni na kuwaondoa kwa mawe kama Daudi alivyomdondosha jitu kubwa Goliat nasi ndivyo tutakavyowaondosha wafilisti wa ccm.....Mungu akutie nguvu kamanda....
 
Tumuombe uzima na salama, maana mahabusu za polisi wetu na baadhi ya mbinu chafu za mahojiano, Mungu bariki Rwakatare sio tuu ni public fugure, bali pia anazijua hakizake mikononi mwa polisi!, angekuwa ni mwenzangu za mimi, saa hizi angekuwa umekwisha sema kila kitu!.

Pamoja na yote, mimi nimeiangalia clip ile na kujiridhisha ni "bonafide genuine!".

Pasco.
Sema umeitazama umeipenda,huo u genuine unaouweka unakudhalilisha kabisa,ndiyo maana kwenye ile post ulibanwa na ukatubishwa dhambi yako ya ukurupukaji,Sasa ni zamu yangu kukutubisha»Sema mimi pasco,nakiri kuwa sina uhakika na ninachoropoka hapa kwa mara nyingine,ni ushabiki wa chama na uchumia tumbo ndiyo unaoniburura.
 
Sema umeitazama umeipenda,huo u genuine unaouweka unakudhalilisha kabisa,ndiyo maana kwenye ile post ulibanwa na ukatubishwa dhambi yako ya ukurupukaji,Sasa ni zamu yangu kukutubisha»Sema mimi pasco,nakiri kuwa sina uhakika na ninachoropoka hapa kwa mara nyingine,ni ushabiki wa chama na uchumia tumbo ndiyo unaoniburura.
Mkuu Capiteni Tamari, kuhusu "bonafide genuine" only time will tell!. Hili la "ukurupukaji", naomba nilihifadhi, maana baadhi ya "wakurupukaji" wa ukweli, ni watu tunaowaheshimu, na wana daraja za juu sana katika jamii!.
hayo mengine, "wewe wasema!".
Pasco.
 
Yaani huu wa Jeshi letu la Police sijui utaisha lini,kuna watu wametajwa kabisa kua ndio vinara wa mauaji kutoka Ikulu ambapo Rama yupo lakn hahojiwi,Mungu ni Mwema sana CDM tutapita salama kwenye haya mapito

Panya wa Pemba wanakutendea haki kwa kukupuliza kisogoni kwani inaoonyesha wazi kabisa wewe ni MSENGEnyaji na ndo maana unaongea upumbavu wako. Unapata faida gani kusikia wanyonyaji na mafisadi wa nchi hii wanafanya vitendo vya kinyama dhidi ya raia na wewe unakaa kushabikia.
 
Tumuombe uzima na salama, maana mahabusu za polisi wetu na baadhi ya mbinu chafu za mahojiano, Mungu bariki Rwakatare sio tuu ni public fugure, bali pia anazijua hakizake mikononi mwa polisi!, angekuwa ni mwenzangu za mimi, saa hizi angekuwa umekwisha sema kila kitu!.

Pamoja na yote, mimi nimeiangalia clip ile na kujiridhisha ni "bonafide genuine!".

Pasco.
Pasco,nimekufatilia sana post zako nyingi naona umesisitiza kuwa clip ni bonafide genuine. Sijui,ila ninadhani kuna ujumbe unataka kuutoa ila hutaki kuwa wa kwanza kuutamka. Jee ni kuwa Lwakatare wataka kusema alinunuliwa kuandaa kitu hicho kwa ahadi ya kinga ya dola na mambo yamegeuka? Kuwa wazi mkuu,hili ni jukwaa huru.
 
Pasco,nimekufatilia sana post zako nyingi naona umesisitiza kuwa clip ni bonafide genuine. Sijui,ila ninadhani kuna ujumbe unataka kuutoa ila hutaki kuwa wa kwanza kuutamka. Jee ni kuwa Lwakatare wataka kusema alinunuliwa kuandaa kitu hicho kwa ahadi ya kinga ya dola na mambo yamegeuka? Kuwa wazi mkuu,hili ni jukwaa huru.
Mkuu Chakaza, sina ujumbe wowote zaidi ya kuuliza "the motive behind!". Tangu clip imetoka, concentration ya wengi ni on genuinity ya clip, mimi huko nilishatoka concern yangu sasa ni "if he was acting alone au ndio mpango wa chama?!.
Pasco.
 
Dhamana ya nn? Huyu hatari kuliko kina ponda na uamsho tusifanye mchezo na usalama wa nchi
Kama kina ponda wamenyimwa dhamana tena mahakamani huyu anaweza kuzuiwa kutumia sheria ya ugaidi hapa inafaa
Tusiwe double standard tuhuma ni nzito na zinahusu uhai wa watu


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hili sakata la Rwakatare limenisikitisha sana maana naona kabisa haki haitendeki kwa makusudi.

Mwisho, naomba Lwakatare akitoka nje kwa dhamana aweke wazi mbivu na mbichi.
 
Huyo anatakiwa afie huko huko asitoke watu walikuwa wanashabikia hapa Masuala ya akina shekhe Ponda leo yamewafika wanaanza kulia lia, Ugaidi na dhamana wapi na wapi?
 
Back
Top Bottom