Mkuranga, Pwani: Mwalimu afungwa kifungo cha maisha kwa kulawiti mwanafunzi

Bull Bucka

Member
Oct 5, 2023
34
46
Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga, imemhukumu kifungo cha maisha jela, aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Msingi St Mathew iliyopo Kongowe, Livingston Kyarwenda (40), baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka tisa.

Kyarwenda, mkazi wa Mbagala Chamanzi anadaiwa kumlawiti mwanafunzi huyo wa kiume aliyekuwa anasoma darasa la nne katika vyoo vilivyopo shuleni hapo.

Uamuzi huo umetolewa leo, Novemba 29, 2023 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Herieth Mwailolo, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

“Kwa kuzingatia uzito wa ushahidi uliotolewa mahakamani hapa wa mashahidi watano ukiwemo ushahidi wa mtoto mwenyewe, mahakama hii imeridhika pasina kuacha shaka yoyote kuwa mshtakiwa ulitenda kosa hilo kinyume cha sheria,” amesema Hakimu na kuongeza;

"Baada ya kukutia hatiani, mahakama hii inakuhukumu kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hii na haki ya kukata rufaa iko wazi iwapo hujaridhika na hukumu hii."
Awali, wakili wa Serikali, Leon Kaikuye alidai kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu na upande wa mashtaka upo tayari kwa ajili ya uamuzi.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 308 ya mwaka 2023, Mwalimu huyo anadaiwa kumwingilia kinyume cha maumbile mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka tisa kinyume cha kifungu cha 154 (1) (a) na (2) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu (Penal Code).

Mwananchi
 
Ulimwengu wa giza umetawala miili na roho za baadhi ya watu kwa kiasi kikubwa mno matokeo yake huchochea na kusababisha uharibifu, hasara na feddheha kubwa kwa mtenda na mtendewa maisha yake yote.

Mungu wa Mbinguni atusaidie NEEMA ya utakaso nafsini mwetu na atuwezeshe kuishi vyema katika ulimwengu wa Nuru.
 
Adhabu kama hizi zisiishie kwa hao wendawazimu pekee, bali ziende hata kwa wanasiasa na watumishi wa umma wanaohujumu mali za umma waziwazi.
Hawawezi kuweka kwa sababu zitawahusu walioweka hizo sheria.
90% ya hao watunga sheria ni wezi wa mali za umma.
Umewahi kujiuliza kwann jela za Africa ni mateso?
Mbona wenzetu ulaya jela zao nzr?
 
Back
Top Bottom