Tunduru: Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kumlawiti Mtoto wake wa miaka minne

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mkazi wa Kijiji cha Namiungo, Wilaya ya Tunduru, Mohamed Saudi Ngwelekwe mwenye umri wa miaka 25 amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia kumlawiti mwanaye wa kumzaa mvulana wa miaka minne.

A72A8C79-873B-4D1D-B8BA-EAA683726534.jpeg

Mtuhumiwa Mohamed Saudi Ngwelekwe ambaye kwa sasa ameanza kifungo chake

Hukumu hiyo imetolewa tarehe 03.03.2023 mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tunduru, Honorius Kando. Mtoto huyo ameeleza kuwa kila alipokuwa anakataa kufanyiwa kitendo hicho, baba yake mzazi alikuwa anamng'ata na kumpiga na kumtishia.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amelipongeza Jeshi la Polisi wilayani humo kupitia Kitengo cha Dawati la Jinsia kwa jitihada walizozifanya tangu Serikali ilipopata taarifa hizo.

DC Mtatiro amesema mtoto huyo (hamtaji jina) amefanyiwa kitendo hicho kwa muda mrefu na inasikitisha.

Mtatiro amewaasa wananchi wa Tunduru popote pale walipo kutoa taarifa Serikalini kila wanapobaini vitendo vya kikatili dhidi ya Watoto kwani vitendo hivyo vinahatarisha maadili na maisha ya kizazi kijacho.
 
ushirikina tu hapo mzee
Hilo linaweza kuwa chanzo, lakini pia tuangalie na uthabiti wa akili (mental consistency). Mihadarati nayo inachangia kwa kiasi kikubwa mtu akili yake kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha. Watu wanaotumia madawa ya kulevya kama pombe (kunywa kupita kiasi), bange, cocaine, nk, mara nyingi huwa na maamuzi ya ajabu na hivyo kupelekea kufanya vitendo vya ajabu. Hivyo, tuangalie maeneo yote haya; ushawishi unaotokana na imani za kishirikina, na madawa ya kulevya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii habari ni ya lini? Hivi mtatiro bado ni do wa tunduru?!!

Nje ya hayo, wadau kuna kazi ya kufanya.....dunia imebadirika sana!
 
Ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumnajisi mtoto wake wa kumzaa
Awali, kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa alieleza kuwa kila alipokuwa anakataa kufanyiwa kitendo hicho ,baba yake alikuwa anamng’ata na kumpiga sehemu.

Mahakama ya Wilaya Tunduru mkoani Ruvuma, imemhukumu Mohamed Ngwelekwe (25) mkazi wa kijiji cha Namiungo, wilayani humo, kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumnajisi mtoto wake wa kiume wa kumzaa mwenye umri wa miaka minne.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Honorius Kando ambaye alisema, mtuhumiwa alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti katika kijiji hicho.

Alisema mtuhumiwa ametenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 158 kifungu kidogo cha(1)(a) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Hata hivyo, mtuhumiwa wakati akisomewa maelezo ya awali, alikiri kutenda kosa hilo na kuiomba Mahakama impunguzie adhabu.

Awali, kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa alieleza kuwa kila alipokuwa anakataa kufanyiwa kitendo hicho ,baba yake alikuwa anamng’ata na kumpiga sehemu za mwili wake na kumtishia.

Shahidi mwingine ambaye ni daktari aliyemfanyia uchunguzi mtoto huyo, aliiambia Mahakama kuwa uchunguzi wa kitabibu umebaini ni kweli mtoto huyo alifanyiwa vitendo hivyo vya kinyama.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro, alipongeza jeshi la polisi wilayani humo kupitia kitengo cha cha Dawati la Jinsia kwa jitihada walizofanya tangu serikali ilipopata taarifa hizo.

Mtatiro alisema, mtoto huyo amefanyiwa kitendo hicho kwa muda mrefu na kuwaasa wananchi popote walipo kutoa taarifa serikalini kila wanapobaini kuwepo kwa vitendo vya aina hiyo ambavyo ni kinyume na maadili na vina hatarisha usitawi wa kizazi cha sasa na kijacho.

Sources Via Mwanzo Tv
 
Nmejalibu kuiona sura nikajua TU HUYU ngwelekwe Jr atakuwa na TATIZO kichwani Sasa Kama anafikia hata kung'ata TATIZO lipo, aende TU akakutane na wakuu wenzake huko gerezani
 
Back
Top Bottom