Afadhali ushike jembe ukalime, kuliko kuomba sala hii

Yesu ni Mungu.Kuna watu baada ya akili zao kushindwa ungamuzi wakaandika kuwa Yesu alikimbia na jamaa wakamsurubisha mtu mwingine🤣🤣.
Kaa fikiria hii....kwenye Quran Mungu wenu anasema sisi (sisi -sio mmoja manake ni zaidi ya mtu mmoja wakitoa kauli kama mtu mmoja) Al-Hijr
Kuna vitu nikivisema hapa ambavyo ata kwa jicho na sikio la kawaidia .ntaonekana nakufuru! Nakuombea kwa Yesu akufunulie Moyo wake na roho wake akakujalie kujua Ukweli ambao huo utakuweka huru
Naomba unifafanulie haya maandiko umeyaelewa vipi =>
Yohana 14:1-6 - Yesu anasema, "Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. Katika nyumba ya baba yangu kuna makao mengi..."
Yohana 17:3 - Yesu anasema, "Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliye mtuma."
Mathayo 6:9-13 - Katika sala ya Baba Yetu, Yesu anafundisha jinsi ya kuomba na kumwomba Mungu.
Kuhusu Mungu kusema sisi =>Hakika ni kuwa hakuna utata wowote katika hilo kwani ni tabia ya utumizi wa lugha nyingi ikiwemo Kiarabu, Kiingereza na hata Kiswahili. Wingi huu katika Lugha ya Kiarabu unaitwa Jam’u Litta’dhwiym (wingi wa utukufu na ukubwa). Wingi umegawanyika sehemu mbili – wingi kama wingi na wingi wa utukufu. Wingi unaotumika katika Qur-aan kwa Allaah Aliyetukuka ni huu wingi wa utukufu na ukubwa.

Katika lugha ya Kiingereza inaitwa The Majestic We. Mara nyingi wakubwa na watukufu kama Raisi, Mfalme, Malkia, Waziri mkuu anapoandika barua au anapohutubia watu husema sisi ilhali makusudio ni yeye peke yake. Sasa hawa sisi ni kina nani na ilhali ni yeye peke yake? Bila shaka ndiyo hayo hayo matumizi ya kutumia wingu wa utukufu. Kwa urefu na kujifunza zaidi=>Kwa Nini Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anatumia Neno ‘Sisi’, Au ‘Tuta...’ Na Hali Yeye Hana Mshirika? | Alhidaaya.com kama unamengine naomba uyalete ili tupate kujifunza.
 
Baadhi ya makanisa huwaga wanaweka kibanda kuna sanamu ya Maria. Ndio huwa wanafanya nini pale?
 
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako amebarikiwa.

Maria mtakatifu, Mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina
 
Sisi wana wa dunia tukumbuke maneno aliyosema Bikira Maria, Alipowatokea watoto wa Fatima, Lucia, Franciska na Yasinta. Alisema tusali, Tusali Rozari, Tupate Amani. Na pia tuwaombee wakosefu na walegevu mwasiomuamini Yesu kristu 🎵🎶
 
Kuna watu wana vismat wakiomba tu apo apo ila ndo hawana time na kusali kabisa
 
Kuna Kanisa moja maarufu kusali bila kumtaja Maria basi sala haijakamilika:
Yaani kila kusanyiko la sala ni lazima Maria atajwe:

Sasa huwa najiuliza huyo Maria ni nani ?
Maana Mama wa Yesu anaitwa Mariamu:
Sijawahi jibiwa hili swali

Mathayo (Mat) 1:18
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Mariamu, Mary, Maria nk. Yote ni majina yake katika lugha tofauti
 
Wewe kama mpentekoste ni sawa wala hatuna haja unasali vip na kwanamna gani

Tutasali hivyo hivyo utake usitake Mkuu
Na sala itajibiwa na yeye akiwemo! Kama yeye ni msabato ninamwelewa kwa sababu hata wakati wa Yesu wayahudi waliheshimu sabato kuliko mafundisho ya Yesu
 
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako amebarikiwa.

Maria mtakatifu, Mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina
Hii sala nilisali juzi nipo hosptali kwa matibabu. Tunaomuamini na kumuomba mama Maria tuendelee kumuamini na kumuomba.
 
Utapoteza muda wako bure ukisali hivi: "Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi ya asili, Mlinzi wa Taifa letu. Utuombee." Sala hiyo haina mashiko kwa sababu zifuatazo:

Kibiblia, hakuna sehemu inayoonyesha kuwa Bikira Maria amepewa jukumu la kuwa mlinzi wa taifa lolote. Mungu pekee ndiye anayeweza kuwa Mlinzi wa taifa, iwapo taifa hilo linamwamini na kumkubali.
Zaburi 33:12
"Heri taifa ambalo Mungu wake ni Mwenyezi-Mungu.”

Je, Bikira Maria ana uwezo wa kuwaombea watu huko aliko? Biblia haitufundishi popote kwamba wafu wanaweza kuwaombea walio hai. Badala yake, Biblia inaeleza kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea(Warumi 8:26). Ukisoma pia Ebr 7:25 imeandikwa kuwa Yesu anatuombea.
Naye[Yesu], kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Ingawa Maria aliheshimiwa na Mungu kwa kuchaguliwa kumzaa Yesu, hana mamlaka ya kuombea watu baada ya kifo chake.

Bikira Maria hakuwa Mkingiwa dhambi ya asili. Kuna watu wanafundisha kwamba Bikira Maria "alikingiwa" dhambi ya asili(the dogma of the Immaculate Conception); yaani kwamba alizaliwa bila dhambi ya asili.

Mafundisho hayo sio sahihi kwa sababu Maandiko yanasema:
“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” — Warumi 3:23

Andiko hilo halibagui. Watu wote wanahitaji wokovu kwa njia ya Yesu, hata Maria mwenyewe alisema:
“Roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu.” — Luka 1:47

Bikira Maria alimtambua Mungu kuwa ndiye Mwokozi wake, hivyo naye pia alihitaji neema ya Mungu kama wengine.

Bikira Maria anastahili heshima kama mama aliyemzaa Bwana Yesu, lakini kama tulivyoona, hatupaswi kumwita mlinzi wa taifa. Kwahiyo ukifunga na kumsihi Bikira Maria akuombee, utapoteza muda wako bure. Afadhali ushike jembe ukalime!

Kama hukubaliani na hoja hizo, weka hapa Maandiko yanayokuambia kwamba "Bikira Maria ni Mlinzi wa Taifa lako, na kwamba yeye ni Mkingiwa dhambi ya asili."

Na kuhusu Maria kwamba anaweza kukuombea, usijitetee kwa kutaja lile tukio la arusi ya Kana ambapo Maria alimwambia Yesu "hawana divai" kisha Yesu akatenda muujiza divai njema ikapatikana. Hilo tukio lilifanyika Maria alipokuwa hai duniani. Sasa hivi Maria hayupo tena. Waliofariki hawasikii wala hawajui chochote kinachoendelea kwa walio hai duniani. Soma Mhubiri 9:6
"lakini wafu hawajui chochote...upendo wao, chuki yao na wivu wao vimetoweka tangu kitambo, kamwe hawatakuwa tena na sehemu katika lolote linalotendeka chini ya jua."
W.a.j.i.n.g.a nyinyi, Romana causa finita lucuta
 
Sisi wana wa dunia tukumbuke maneno aliyosema Bikira Maria, Alipowatokea watoto wa Fatima, Lucia, Franciska na Yasinta. Alisema tusali, Tusali Rozari, Tupate Amani. Na pia tuwaombee wakosefu na walegevu mwasiomuamini Yesu kristu 🎵🎶
Na wewe unasemaje
Hii sala nilisali juzi nipo hosptali kwa matibabu. Tunaomuamini na kumuomba mama Maria tuendelee kumuamini na kumuomba.
Yesu amekufundisha umuombe mama yake, hivi huogopi kukataliwa na Yesu kwa kuacha mafundisho yake, mwenzenu anawapenda ndiyo maana anawakumbusha , hayo ni mafundisho ya Yesu au nani.
 
Ndiyo, Ni mafundisho ya Yesu
.
 
Nikomboe mtumishi wa bwana - napenda sana wake za watu, Cha ajabu hawakatai 🙏🏿
 
Naomba unifafanulie haya maandiko umeyaelewa vipi =>
Yohana 14:1-6 - Yesu anasema, "Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. Katika nyumba ya baba yangu kuna makao mengi..."
Yohana 17:3 - Yesu anasema, "Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliye mtuma."
Mathayo 6:9-13 - Katika sala ya Baba Yetu, Yesu anafundisha jinsi ya kuomba na kumwomba Mungu.
Kuhusu Mungu kusema sisi =>Hakika ni kuwa hakuna utata wowote katika hilo kwani ni tabia ya utumizi wa lugha nyingi ikiwemo Kiarabu, Kiingereza na hata Kiswahili. Wingi huu katika Lugha ya Kiarabu unaitwa Jam’u Litta’dhwiym (wingi wa utukufu na ukubwa). Wingi umegawanyika sehemu mbili – wingi kama wingi na wingi wa utukufu. Wingi unaotumika katika Qur-aan kwa Allaah Aliyetukuka ni huu wingi wa utukufu na ukubwa.

Katika lugha ya Kiingereza inaitwa The Majestic We. Mara nyingi wakubwa na watukufu kama Raisi, Mfalme, Malkia, Waziri mkuu anapoandika barua au anapohutubia watu husema sisi ilhali makusudio ni yeye peke yake. Sasa hawa sisi ni kina nani na ilhali ni yeye peke yake? Bila shaka ndiyo hayo hayo matumizi ya kutumia wingu wa utukufu. Kwa urefu na kujifunza zaidi=>Kwa Nini Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anatumia Neno ‘Sisi’, Au ‘Tuta...’ Na Hali Yeye Hana Mshirika? | Alhidaaya.com kama unamengine naomba uyalete ili tupate kujifunza.
Kwa Wa katoliki Majini ni Malaika waliolaniwa.Aiingii akilini kuwa yapo yanaoswali
 
Attachments

  • images - 2025-06-21T184740.242.jpeg
    images - 2025-06-21T184740.242.jpeg
    11.5 KB · Views: 21
  • download (23).png
    download (23).png
    9.3 KB · Views: 20
Ni hivi akuna aneabudu sanamu kwenye Ukatoliki- wewe sio Dini yako so usijisumbuwe nayo.Pia Bibilia unayo toa vifungu na kulalamika hapa ni Kitabu cha hao Wakatoliki.Aingii akilini mtunga Sheria akavyunja adharani Sheria alizotunga mwenyewe.Lete maandishi nje ya Bibilia kutetea hoja yako.Jambo ukristo utaendelea kuwapusa kichwa milele yote kwa sababu ....una majibu yote.
Sio kuziabudu tu
Bali hata kuzisujudia sanamu na kuzitumikia imekatazwa:
Hivi unataka kuniambia sanamu za Maria hazisujudiwi na Wakatoriki ?
Sema tu ukweli brother:

Hakuna Kanisa ambalo halina sanamu la Maria ambalo waumini kama wote wanalisujudia mala kwa mala:

Mfano wewe ni mkubwa unaweza kuliona kama sanamu tu:
Vipi kuhusu watoto wanaotazama wakubwa wakipiga magoti na kusujudia hizo sanamu ?

Mimi ni Mkatoriki pia ila sithubutu kuzisujudia hizo sanamu, wala kuelekeza maombi yangu kwa Maria:

Mwisho kama muumini unajuaje hiyo sanamu ni ya Maria ?
Je aliyeitengeneza unamjua ?
Au hujui kuwa Ibirisi anaweza kuishi ndani ya sanamu na akasujudiwa na maelfu ya watu kwa kuto kujua ?

Ndio maana ikaandikwa usisujudie sanamu wala kuzitumikia:

Ushaona vinyago vya mganga wa mchawi ?
Ni vinyago vyenye roho kamili ya Shetani ndani yake:

Zamani tulikuwa tunakesha kuomba na kusujudia sanamu za Maria. Hadi watu wakawa wanashuhudia kutokewa na Maria kwenye ndoto:

Zilipigwa Novena hadi magoti yanaota sugu:

Kabla ya kupata utambuzi mimi nilikuwa mikiziabudu na kuzisujudia hizo kwa maelekezo ya viongozi wa Kanisa na wazazi:

Hivyo ninacho kiandika nakijua Brother:
Sana tu.
 
Sio kuziabudu tu
Bali hata kuzisujudia sanamu na kuzitumikia imekatazwa:
Hivi unataka kuniambia sanamu za Maria hazisujudiwi na Wakatoriki ?
Sema tu ukweli brother:
Hakuna Kanisa ambalo halina sanamu la Maria ambalo waumini kama wote wanaliaujudia mala kwa mala:

Mfano wewe ni mkubwa unaweza kuliona kama sanamu tu:
Vipi kuhusu watoto wanaotazama wakubwa wakipiga magoti na kusujidia hizo sanamu ?
Mimi ni Mkatoriki pia ila sithubutu kuzisujudia hizo sanamu, wala kuelekeza maombi yangu kwa Maria:

Mwisho kama muumini unajuaje hiyo sanamu ni ya Maria ?
Je aliitengeneza unamjua ?
Au hujui kuwa Ibirisi anaweza kuishi ndani ya ndani ya sanamu na akasujudiwa na maelfu ya watu kwa kujua ?

Ndio maana ikaandikwa usisujudie sanamu wala kuzitumikia:
Ushaona vinyago vya mganga wa mchawi ?
Ni vinyago vyenye roho kamili ya Shetani ndani yake:
Lete andiko lako usilete yaliomo kwenye Bibilia kwani sio Kitabu chako
 
Kabisa

Back
Top Bottom