Afadhali ushike jembe ukalime, kuliko kuomba sala hii

Afadhali ushike jembe ukalime, kuliko kuomba sala hii

Utapoteza muda wako bure ukisali hivi: "Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi ya asili, Mlinzi wa Taifa letu. Utuombee." Sala hiyo haina mashiko kwa sababu zifuatazo:

Kibiblia, hakuna sehemu inayoonyesha kuwa Bikira Maria amepewa jukumu la kuwa mlinzi wa taifa lolote. Mungu pekee ndiye anayeweza kuwa Mlinzi wa taifa, iwapo taifa hilo linamwamini na kumkubali.
Zaburi 33:12
"Heri taifa ambalo Mungu wake ni Mwenyezi-Mungu.”

Je, Bikira Maria ana uwezo wa kuwaombea watu huko aliko? Biblia haitufundishi popote kwamba wafu wanaweza kuwaombea walio hai. Badala yake, Biblia inaeleza kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea(Warumi 8:26). Ukisoma pia Ebr 7:25 imeandikwa kuwa Yesu anatuombea.
Naye[Yesu], kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Ingawa Maria aliheshimiwa na Mungu kwa kuchaguliwa kumzaa Yesu, hana mamlaka ya kuombea watu baada ya kifo chake.

Bikira Maria hakuwa Mkingiwa dhambi ya asili. Kuna watu wanafundisha kwamba Bikira Maria "alikingiwa" dhambi ya asili(the dogma of the Immaculate Conception); yaani kwamba alizaliwa bila dhambi ya asili.

Mafundisho hayo sio sahihi kwa sababu Maandiko yanasema:
“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” — Warumi 3:23

Andiko hilo halibagui. Watu wote wanahitaji wokovu kwa njia ya Yesu, hata Maria mwenyewe alisema:
“Roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu.” — Luka 1:47

Bikira Maria alimtambua Mungu kuwa ndiye Mwokozi wake, hivyo naye pia alihitaji neema ya Mungu kama wengine.

Bikira Maria anastahili heshima kama mama aliyemzaa Bwana Yesu, lakini kama tulivyoona, hatupaswi kumwita mlinzi wa taifa. Kwahiyo ukifunga na kumsihi Bikira Maria akuombee, utapoteza muda wako bure. Afadhali ushike jembe ukalime!

Kama hukubaliani na hoja hizo, weka hapa Maandiko yanayokuambia kwamba "Bikira Maria ni Mlinzi wa Taifa lako, na kwamba yeye ni Mkingiwa dhambi ya asili."

Na kuhusu Maria kwamba anaweza kukuombea, usijitetee kwa kutaja lile tukio la arusi ya Kana ambapo Maria alimwambia Yesu "hawana divai" kisha Yesu akatenda muujiza divai njema ikapatikana. Hilo tukio lilifanyika Maria alipokuwa hai duniani. Sasa hivi Maria hayupo tena. Waliofariki hawasikii wala hawajui chochote kinachoendelea kwa walio hai duniani. Soma Mhubiri 9:6
"lakini wafu hawajui chochote...upendo wao, chuki yao na wivu wao vimetoweka tangu kitambo, kamwe hawatakuwa tena na sehemu katika lolote linalotendeka chini ya jua."
The spirit behind of all these nonsense is to suit your political interest (Your Religion Defacto) and not spiritual awakening.
 
Hata Chizi Huwa Hajui Kuwa Yeye ni chizi Jitahidi Kuwaelewa Watu Kwa Jinsi Walivyo
 
Pilipili usiyoila inakuwashia nini? Kama sio kuchanganyikiwa itakuwa nini?

The best way ni kukaa na dini na sala zako kimya kimya. Unapoanza kulazimisha kuwa wewe ni bora zaidi, ujue hamna kitu....ni kama debe tupu linavyopiga kelele.

Kwangu mimi, nasali sana tu...Bikira Maria mama yake Yesu, utuombee
 
Lete andiko lako usilete yaliomo kwenye Bibilia kwani sio Kitabu chako
Ha..ha...ha
Badala ya kusoma na kuelewa nilicho kiandika wewe unajimilikisha Biblia:

Biblia ni Neno la Mungu kwa ajili ya kila Kiumbe:
Tatizo madhehebu mengi yana chagua maandiko ya kuyazingatia:

Swala la kusujudia sanamu Wakatoriki wengi hata uwa wekee andiko wanajitoa ufahamu:

Neno la Mungu ni Upanga Ulao
na Uchomao kwa makali kuwili:

Halichagui nani anapenda au hapendi: Neno Linasimama kama lilivyo:
Hebu soma tena kwa kutulia na kwa umakini hapa;

Kumbukumbu la Torati 5:8

1.👉Usijifanyie sanamu ya kuchonga,
2: 👉mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi.

9 👉Usivisujudie wala
👉kuvitumikia;
👉Kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wako,
👉ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

10 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
...................
Hapo hata neno kuabudu halipo:
Unapo isujudia Sanamu ambayo humjui aliye itengeneza, utawezaje kujua roho iliyo ndani ya hiyo sanamu?
...
Mwenye masikio amesikia:
 
Baadhi ya makanisa huwaga wanaweka kibanda kuna sanamu ya Maria. Ndio huwa wanafanya nini pale?
Hakuna ushahidi wowote kuwa hizo sanamu ni za Maria, na hakuna andiko Maria alisema wachonge sanamu yake na kuisujudia:

Kuweka hizo sanamu na kuzisujudia ni kumdhalilisha Mariamu mama wa Yesu:

Huko aliko Mariamu atakuwa anasikitika sana kwa wanachomfanyia Wakatoriki:

Unatengeneza sanamu kwa mchanga na simenti halafu unasema ni Maria...!
Hii ni Kufru kama Kufru nyingine mbele za Mungu:
 
The spirit behind of all these nonsense is to suit your political interest (Your Religion Defacto) and not spiritual awakening.
Unamchokoza kwa kimombo chako cha kuunga unga huyo Binti sio ?
Usije ukamkimbia humu akianza kukushushia Slang ya Malkia:
Huyo kimombo ni kama amekitengeneza yeye, wewe jiumeume tu mwenzako anakuangalia tu:
 
Wazungu na warabu walijua kuwapotezea wazeee wetu mda. Waliiba nguvu zao, waliiba watoto wao utumwani, waliiba wanawake wao wazuri na wakagongelea msumari kuwaibia mda wa kufanya kazi ili wawe masikini na yote waliyafanikisha.

Hila zimebaki kwenye vitabu walivyoviacha , misikiti na makanisa. Ila naona dalili za waaafrika kuanza kutupilia mbali nadharia za wakoloni.
Siku hizi wakiristo ana mke pembeni ana ndoa yake ya siri na watoto.
Kamari wanacheza, riba wanakula na fungu la 10 hawapeleki. Juma pili wanaenda kanisani na kuopoa pisi kali za kufumua jioni ya wiki. Wanateka na kuua wenzao kwa malipo ya fedha, Kwa waganga wanaenda na kutoa kafara mbali mbali. Huu mda wa uchaguzi kila mgobea ataenda kwa mganga wake kung'arisha nyota na ataongea kila uongo kwenye majukwaaa ya kisiasa kuzushia wapinzani wao wa nafasi. Wanaiba pesa za miradi, dawa hospitalini, rushwa mahakamani, kupiga wenzao wanapokuwa polisi na kunyang'anya kila aina ya fursa.
Wanapokuja kununua mazao vijijini wanatumia madebe feki, wanapunguza bei halisi na ku.lalia mkiristo mwenzao.
Mashambani hakuna anaepandaazao bila kufukia dawa kwenye pembe za shamba.
Kwa hio hizo dini zimebaki kama vikundi vya kufa5ijiana wala usidanganywe.
Kama huniamini nenda kanisani jpili ya leo katafute demu mle, ukikosa hamia malawi.
Kama huniamini nenda leo kanisani kaseme mtoto hana ada wala hujui utapata wapi , wakikuchangia milioni ya ada basi utamuona yesu live.
Mnaosali endeleeni kusali ila tunawajua vizuri sana. Wapo wanaosali na hawana mambo niliyoyata juu vile vile wapo wasiosali na hawana huo ushetani.
Ukipinga basi weka hoja yenye mashiko kupinga niliyoyasema pale.
 
Mitume 12 wa Yesu walifundisha baada ya Yesu kuondoka
Je wajua walifundisha Nini? Kwani biblia haituambii chochote zaidi ya machache kwenye matendo ya mitume na nyaraka za mitume
Kwamfano mtume Filipo, au Batholomayo alifundisha Nini?

Paulo alianzisha makanisa kadhaa, lakini yote yalikufa likabaki lile la Roma na kusambaa dunia yote
Kwanini Yesu aliachilia makanisa yafe na kuliacha moja?

Je, Paulo na mitume wengine walifundisha kwa kutumia biblia gani? Na je waliofundishwa walidai ushahidi wa maandiko?

Katika biblia tunaona mtu anaamua kushika vazi la Yesu ili apone! Na kweli alipona
Yule aliambiwa na Nani kuwa vazi la Yesu linaponya?
Alitumia maandiko gani kujifunza?

Mungu hafungwi na maandishi ya biblia!
Mungu anafungwa na Imani ya nafsi. Je Imani yako unakusukuma kuamini Nini kuhusu Mungu wako?
Tuonyane juu ya matendo ya dhambi.
Ila Imani tuziache! Maana Mungu humtendea mtu kadri ya Imani yake ili mradi tu awe amefungamana naye kiroho
 
Hizo sanamu ni za Mchanga na Simenti:
Na hazina uhusiano wowote na Mariamu mama wa Yesu:
Waliozitengeneza wanajua waliko zitoa:
 
Madam - Bwana yesu asifiwe.

Naomba kujua wewe ni Continuanist au Cessationist?

Pia unaamini katika sheria au Unaamini kukombolewa kwa Neema?
 
Back
Top Bottom