Afadhali ushike jembe ukalime, kuliko kuomba sala hii

Wewe dada/kaka usipochanganyikiwa mwaka huu, bs uchanganyikiwi tena!! Kuongea au kumuomba Mungu hakuitaji kanuni, sio hesabu wala fizikia,.
Mungu anajua yale yaliyomo kwenye mioyo yetu...
 
Wanafunzi wa Yesu walimuomba Yesu awafundishe kusali. Akawaambia salini hivi..."Baba yetu..."

Salini hivi...ni sawa na kusema fuateni kanuni au misingi hii ya maombi ili maombi yenu yajibiwe. Hujiulizi kwanini watu wanaomba sana lakini wanaojibiwa ni wachache? Wengi hawazingatii vigezo na masharti. Kwa mfano, Yesu alisema: tukimuomba Mungu kwa Jina lake, atafanya. Sasa mtu badala ya kufuata agizo hilo anamuomba Maria amuombee!!
 
Unataka kusema usipoomba hivyo Mungu ajibu?
 
Yohana 2: 1-12 , Yesu anamsikiliza mama yake, mama yake Yesu anasaidia kufikisha maombi yetu kwa Mwanae.
 
Unahangaika wewe dada mlokole. Wakatoliki wanamuomba Maria, na wewe mlokole unaomba kwa namna yako; ni mambo yale yale tu. Wote mnamuomba Mungu wa Waisraeli ilhali ninyi ni wanyalukolo na wazaramo hapo kisiju.

Wote mmekazana na kitabu cha Biblia mlicholetewa na wakoloni; kikawapumbaza mababu, wazazi, na sasa ninyi. Nanyi, pengine, mnarithisha ngano na uzushi wa Biblia na Kurani kwa watoto wenu.

Hamna tofauti; wote mko chungu kimoja cha watumwa wa imani za kuja. Hamna haja ya kuchekana.

Zaidi ya hayo, dunia hii ina maelfu ya imani za mambo ya kusadikika; wewe unatoa wapi ujasiri wa kujiona uko sahihi sana kurekebisha Waafrika wenzio kuhusu utumwa wako wa kidini? Yaani mtumwa anamfundisha mtumwa mwingine jinsi ya kuwa mtumwa bora? We! Ninyi nyote ni walewale tu.
 
Kwahiyo mwanamke akishazaa bado anaendelea kuwa bikra,we ulisikia wapi.?
 
Unataka kusema usipoomba hivyo Mungu ajibu?
Sala ya BWANA ni kama mwongozo tu wa jinsi ya kuomba. Ndani ya sala hiyo kuna mengi tunayopaswa kufanya wakati wa maombi. Kwa mfano: kumsifu Mungu, kusamehe nk. Soma Biblia kwa makini utaona maandiko mengi yanayotufundisha jinsi ya kuomba na kupata majibu.
 
Kama una hitaji lolote, omba kwa kufuata mwongozo huu, utapata majibu ya maombi yako:

1. Omba kwa Jina la Yesu
“Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, nitalifanya.” — Yohana 14:14

2. Omba kwa imani
Yakobo 1:6
"Ila na aombe kwa imani, pasipo mashaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari linalochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.”

3. Omba sawasawa na mapenzi ya Mungu
1 Yohana 5:14
"Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia..”

4. Kabla hujaomba, wasamehe waliokukosea. Usiombe huku una kinyongo
Marko 11:25
"Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu”

5. Omba kwa bidii na kwa uvumilivu
Yak 5:16
"...kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii."

Luka 18:1
Kisha Yesu akawapa wanafunzi wake mfano ili kuwaonesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa.

Na usisahau, kabla ya kuomba, hakikisha umetubu dhambi zako zote.
Isaya 59:2
"Lakini maovu yenu yamewatenganisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia..”

Zaburi 66:18
"Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia."

Methali 28:9
"Anayekataa kuisikia sheria, huyo hata sala yake ni chukizo kwa Mungu."
Crap
 
You are very smart....!
Kuna nyama kidogo hujaijazia ila uko perfect....
Aliekuumba Na Akubariki...!
 
Utapoteza muda wako bure ukisali hivi: "Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi ya asili, Mlinzi wa Taifa letu. Utuombee." Sala hiyo haina mashiko kwa sababu zifuatazo:

Kibiblia, hakuna sehemu inayoonyesha kuwa Bikira Maria amepewa jukumu la kuwa mlinzi wa taifa lolote. Mungu pekee ndiye anayeweza kuwa Mlinzi wa taifa, iwapo taifa hilo linamwamini na kumkubali.
Zaburi 33:12
"Heri taifa ambalo Mungu wake ni Mwenyezi-Mungu.”

Je, Bikira Maria ana uwezo wa kuwaombea watu huko aliko? Biblia haitufundishi popote kwamba wafu wanaweza kuwaombea walio hai. Badala yake, Biblia inaeleza kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea(Warumi 8:26). Ukisoma pia Ebr 7:25 imeandikwa kuwa Yesu anatuombea.
Naye[Yesu], kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Ingawa Maria aliheshimiwa na Mungu kwa kuchaguliwa kumzaa Yesu, hana mamlaka ya kuombea watu baada ya kifo chake.

Bikira Maria hakuwa Mkingiwa dhambi ya asili. Kuna watu wanafundisha kwamba Bikira Maria "alikingiwa" dhambi ya asili(the dogma of the Immaculate Conception); yaani kwamba alizaliwa bila dhambi ya asili.

Mafundisho hayo sio sahihi kwa sababu Maandiko yanasema:
“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” — Warumi 3:23

Andiko hilo halibagui. Watu wote wanahitaji wokovu kwa njia ya Yesu, hata Maria mwenyewe alisema:
“Roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu.” — Luka 1:47

Bikira Maria alimtambua Mungu kuwa ndiye Mwokozi wake, hivyo naye pia alihitaji neema ya Mungu kama wengine.

Bikira Maria anastahili heshima kama mama aliyemzaa Bwana Yesu, lakini kama tulivyoona, hatupaswi kumwita mlinzi wa taifa. Kwahiyo ukifunga na kumsihi Bikira Maria akuombee, utapoteza muda wako bure. Afadhali ushike jembe ukalime!

Kama hukubaliani na hoja hizo, weka hapa Maandiko yanayokuambia kwamba "Bikira Maria ni Mlinzi wa Taifa lako, na kwamba yeye ni Mkingiwa dhambi ya asili."

Na kuhusu Maria kwamba anaweza kukuombea, usijitetee kwa kutaja lile tukio la arusi ya Kana ambapo Maria alimwambia Yesu "hawana divai" kisha Yesu akatenda muujiza divai njema ikapatikana. Hilo tukio lilifanyika Maria alipokuwa hai duniani. Sasa hivi Maria hayupo tena. Waliofariki hawasikii wala hawajui chochote kinachoendelea kwa walio hai duniani. Soma Mhubiri 9:6
"lakini wafu hawajui chochote...upendo wao, chuki yao na wivu wao vimetoweka tangu kitambo, kamwe hawatakuwa tena na sehemu katika lolote linalotendeka chini ya jua."
Yaani usiku wote huo unahangaika na Roman catholic badala UMPE mme wako kitumbua!
 
Ukipata fulsa ya kufanya maombi katika imani ya Kikatoriki, bila kimtaja Maria unaweza kufukuzwa kwenye jumuiya hiyo na ukaambiwa ni msaliti:
Bado natafakari, hii nguvu kubwa ya Maria katika Kanisa Katoriki inatoka wapi...!
Maria ni kama Mungu wa Wakatoriki:
 
Kwanza kabisa.Jua kuwa Bibilia ni Kitabu cha Kikatoliki( Wakatoliki ndo waliokusanya maandiko yote yaliomo kwenye Bibilia na pia Wana maelfu ya nyaraka mbalimbali za wakati wa manabii na wakati wa Yesu ambayo mpaka Leo wapo vijana wanayasoma na kuyachambuwa)- akuna mfalme ambae atamwacha mama yake katika hali ya kawaidia bila ya kumtumza,kumremba na mengineyo.kwa kufupi Yesu alikuwa karibu sana na mama yake ata pale aliposurubiwa.
Ni Yesu aliekabidhi Mama yake kwa Baba Mtakatifu wa kwanza mwanzilishi wa kanisa Katoliki.Kuwa Toka sasa Maria atakuwa mama wa Yule Mtume ambae Yesu anaanzisha kanisa lake takatifu.Toka hapo Bikira Maria ni Mama wa mkatoliki yeyote duniani na hakika akuna aliekosa kitu akiomba kupitia yeye.MARIA MTAKATIFU MAMA WA MUNGU UTOMBER SISI WAKOSEFU.

Mama tazama mwanao​

Yohana 19:26-27 “Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.”
 
Asante sana, umeeleweka vzr mtoa mada.

1: Lengo lako ni nini?
2: Imani ya mwingine inakusumbua nini?🤣, natamani sana kujua yaani kwa nini jambo la watu limekuchukulia muda wakati halikuhusu? Mbona hukufikiria kuchukua jembe ukalime?
3: Kuna watu pia huwa hawailewi imani yako na huwa wanawaza wakwambie kuliko kupoteza muda the way unaabudu, ni bora ushike jembe ukalime, lkn kwa sababu jambo lako haliwahusu waliamua kukaa kimya.
 
Ukipata fulsa ya kufanya maombi katika imani ya Kikatoriki, bila kimtaja Maria unaweza kufukuzwa kwenye jumuiya hiyo na ukaambiwa ni msaliti:
Bado natafakari, hii nguvu kubwa ya Maria katika Kanisa Katoriki inatoka wapi...!
Maria ni kama Mungu wa Wakatoriki:
Ipo siku wewe na Mimi tutakutana na Mungu alietuumba.na Kila mmoja atahesabiwa ameishije Duniani.Usiwe wa kufarahisha watu! Wakatoliki awamlazimishi yeyeote kufanya kitu kwa Shuruti.muda wa ibada ukifika utasikia kengere.ukienda sawa usipoenda sawa.Ata Dini ya Kiislam japo inapinga mengi katika ukristu.... Kitabu chao kitakatifu kina aya mzima juu ya huyu mama yetu mwema aliepalizwa Mbiguni
 
Attachments

  • 20250620_160053.jpg
    20250620_160053.jpg
    46 KB · Views: 22
  • 20250618_053230.jpg
    20250618_053230.jpg
    175.9 KB · Views: 28
  • 20250617_143616.jpg
    20250617_143616.jpg
    69.2 KB · Views: 19
  • 20250616_220950.jpg
    20250616_220950.jpg
    191 KB · Views: 24
  • 20250616_164258.jpg
    20250616_164258.jpg
    49.9 KB · Views: 21
Utapoteza muda wako bure ukisali hivi: "Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi ya asili, Mlinzi wa Taifa letu. Utuombee." Sala hiyo haina mashiko kwa sababu zifuatazo:

Kibiblia, hakuna sehemu inayoonyesha kuwa Bikira Maria amepewa jukumu la kuwa mlinzi wa taifa lolote. Mungu pekee ndiye anayeweza kuwa Mlinzi wa taifa, iwapo taifa hilo linamwamini na kumkubali.
Zaburi 33:12
"Heri taifa ambalo Mungu wake ni Mwenyezi-Mungu.”

Je, Bikira Maria ana uwezo wa kuwaombea watu huko aliko? Biblia haitufundishi popote kwamba wafu wanaweza kuwaombea walio hai. Badala yake, Biblia inaeleza kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea(Warumi 8:26). Ukisoma pia Ebr 7:25 imeandikwa kuwa Yesu anatuombea.
Naye[Yesu], kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Ingawa Maria aliheshimiwa na Mungu kwa kuchaguliwa kumzaa Yesu, hana mamlaka ya kuombea watu baada ya kifo chake.

Bikira Maria hakuwa Mkingiwa dhambi ya asili. Kuna watu wanafundisha kwamba Bikira Maria "alikingiwa" dhambi ya asili(the dogma of the Immaculate Conception); yaani kwamba alizaliwa bila dhambi ya asili.

Mafundisho hayo sio sahihi kwa sababu Maandiko yanasema:
“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” — Warumi 3:23

Andiko hilo halibagui. Watu wote wanahitaji wokovu kwa njia ya Yesu, hata Maria mwenyewe alisema:
“Roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu.” — Luka 1:47

Bikira Maria alimtambua Mungu kuwa ndiye Mwokozi wake, hivyo naye pia alihitaji neema ya Mungu kama wengine.

Bikira Maria anastahili heshima kama mama aliyemzaa Bwana Yesu, lakini kama tulivyoona, hatupaswi kumwita mlinzi wa taifa. Kwahiyo ukifunga na kumsihi Bikira Maria akuombee, utapoteza muda wako bure. Afadhali ushike jembe ukalime!

Kama hukubaliani na hoja hizo, weka hapa Maandiko yanayokuambia kwamba "Bikira Maria ni Mlinzi wa Taifa lako, na kwamba yeye ni Mkingiwa dhambi ya asili."

Na kuhusu Maria kwamba anaweza kukuombea, usijitetee kwa kutaja lile tukio la arusi ya Kana ambapo Maria alimwambia Yesu "hawana divai" kisha Yesu akatenda muujiza divai njema ikapatikana. Hilo tukio lilifanyika Maria alipokuwa hai duniani. Sasa hivi Maria hayupo tena. Waliofariki hawasikii wala hawajui chochote kinachoendelea kwa walio hai duniani. Soma Mhubiri 9:6
"lakini wafu hawajui chochote...upendo wao, chuki yao na wivu wao vimetoweka tangu kitambo, kamwe hawatakuwa tena na sehemu katika lolote linalotendeka chini ya jua."
Bila shaka wewe ni msabato
 
Ukipata fulsa ya kufanya maombi katika imani ya Kikatoriki, bila kimtaja Maria unaweza kufukuzwa kwenye jumuiya hiyo na ukaambiwa ni msaliti:
Bado natafakari, hii nguvu kubwa ya Maria katika Kanisa Katoriki inatoka wapi...!
Maria ni kama Mungu wa Wakatoriki:
Nguvu alikuwa nayo na akili zake ni zaidi ya kwako wewe na inatoka kwa Mungu baba.
 
Attachments

  • 20250620_160053.jpg
    20250620_160053.jpg
    46 KB · Views: 25
  • 20250620_100344.jpg
    20250620_100344.jpg
    133.9 KB · Views: 19
  • 20250617_143616.jpg
    20250617_143616.jpg
    69.2 KB · Views: 20
Ibada ya Maria ya Nevena ni balaa kubwa:
Ukichelewa tu muda wa kuamka saa tisa ya usiku, unatakiwa kuianza upya:
Ukikosea tu kidoti cha Lozari unatakiwa kuianza upya:
Inadumu kwa muda wa wiki moja kesh:
Ina masharti kama ya waganga wachawi:
 
Utapoteza muda wako bure ukisali hivi: "Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi ya asili, Mlinzi wa Taifa letu. Utuombee." Sala hiyo haina mashiko kwa sababu zifuatazo:

Kibiblia, hakuna sehemu inayoonyesha kuwa Bikira Maria amepewa jukumu la kuwa mlinzi wa taifa lolote. Mungu pekee ndiye anayeweza kuwa Mlinzi wa taifa, iwapo taifa hilo linamwamini na kumkubali.
Zaburi 33:12
"Heri taifa ambalo Mungu wake ni Mwenyezi-Mungu.”

Je, Bikira Maria ana uwezo wa kuwaombea watu huko aliko? Biblia haitufundishi popote kwamba wafu wanaweza kuwaombea walio hai. Badala yake, Biblia inaeleza kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea(Warumi 8:26). Ukisoma pia Ebr 7:25 imeandikwa kuwa Yesu anatuombea.
Naye[Yesu], kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Ingawa Maria aliheshimiwa na Mungu kwa kuchaguliwa kumzaa Yesu, hana mamlaka ya kuombea watu baada ya kifo chake.

Bikira Maria hakuwa Mkingiwa dhambi ya asili. Kuna watu wanafundisha kwamba Bikira Maria "alikingiwa" dhambi ya asili(the dogma of the Immaculate Conception); yaani kwamba alizaliwa bila dhambi ya asili.

Mafundisho hayo sio sahihi kwa sababu Maandiko yanasema:
“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” — Warumi 3:23

Andiko hilo halibagui. Watu wote wanahitaji wokovu kwa njia ya Yesu, hata Maria mwenyewe alisema:
“Roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu.” — Luka 1:47

Bikira Maria alimtambua Mungu kuwa ndiye Mwokozi wake, hivyo naye pia alihitaji neema ya Mungu kama wengine.

Bikira Maria anastahili heshima kama mama aliyemzaa Bwana Yesu, lakini kama tulivyoona, hatupaswi kumwita mlinzi wa taifa. Kwahiyo ukifunga na kumsihi Bikira Maria akuombee, utapoteza muda wako bure. Afadhali ushike jembe ukalime!

Kama hukubaliani na hoja hizo, weka hapa Maandiko yanayokuambia kwamba "Bikira Maria ni Mlinzi wa Taifa lako, na kwamba yeye ni Mkingiwa dhambi ya asili."

Na kuhusu Maria kwamba anaweza kukuombea, usijitetee kwa kutaja lile tukio la arusi ya Kana ambapo Maria alimwambia Yesu "hawana divai" kisha Yesu akatenda muujiza divai njema ikapatikana. Hilo tukio lilifanyika Maria alipokuwa hai duniani. Sasa hivi Maria hayupo tena. Waliofariki hawasikii wala hawajui chochote kinachoendelea kwa walio hai duniani. Soma Mhubiri 9:6
"lakini wafu hawajui chochote...upendo wao, chuki yao na wivu wao vimetoweka tangu kitambo, kamwe hawatakuwa tena na sehemu katika lolote linalotendeka chini ya jua."
Sasa kwanini wakatoliki wanaishi maisha mazuri kuliko nyie mnaosali hizo sala zenu?
 
Back
Top Bottom