Adhabu ya Kunyonga Hadi Kufa imepitwa na wakati?

nameless girl;

1. Kunyonga mtu kwa kwa kosa la kuua ni sawa na kurudia kosa la huyo aliyeua na kujificha nyuma ya mgongo wa sheria. HAKI NA UHURU UTOLEWA NA SHERIA WALA HAIJI BY NATURE, KWA IYO SHERIA IKISTATE, BASI HAPO HAKUNA KUJIFICHA NYUMA YA SHERIA BALI NDO SHERIA INAVOELEKEZA. KAMA MNASEMA HAKUNA SABABU YA KUONDOA UHAI WA MTU ALIYEUA , IYO HAKI INATOKA WAPI?KWA NINI ANAYEUA KWA UPANGA ASIFE KWA UPANGA??

2. Hakuna usawa wa haki nchini kwetu so watu watakaokuwa wananyongwa ni wale watakaokua wanashindwa kutoa corruption so kwa hili, tutapaswa kuita haki au mauaji? HII NI ASSUMPTION, JE NA KWA KWA MAHAKAMA INAYOFUATA HAKI NA KUTOKUWA NA CORRUPTION? JE CORRUPTION INAONDOLEWA KWA KUTONYONGA WAUAJI??

3. Nchi yetu ni masikini sana. Kumpoteza mtu mmoja katika taifa letu ni sawa na kupoteza nguvukazi ya taifa letu. Hao wanaopaswa kuuwawa wanapaswa kupewa kazi tofauti waweze kucontribute chochote kwa taifa lao. MTU AUE THEN AOMBE KUPEWA KAZI NYINGINE??KWA NINI ASINGEMUACHA MWENZIE AISHI THEN WAJENGE TAIFA PAMOJA?? TANZANIA SIO MASKINI ILA WATU WAKE NDO MASKINI

4. Nadhani art 13 inaongelea right to life. Kuwa na hii adhabu ni sawa na kufundisha jamii jinsi ya kukiuka sheria zilizowekwa.KUKIUKA SHERIA ZILIZOWEKWA NI PAMOJA NA KUKIUKA SHERIA YA KUNYONGA WAUAJI NA WENGINE WANAOSTAHILI ADHABU IYO. ARTICLE 13(1) inakataza ubaguzi, iweje mtu aue then yeye aone ana haki ya kuishi?
ibara ya 14 inasema kila mtu anayo haki ya kuishi....je kwa nini mtu aue wakati yeye anatambua haki ya mwenzie kuishi??anayekiuka haki iyo apewe tuzo au adhabu kama iyo?? Ukitetea haki ya kuishi, basi utetee na haki ya kutofungwa kama ibara ya 15 inavyoelekeza....
5. Hao watu wanaonyongwa, l believe wana watu wanaotegemewa, so killing a hero wa familia its like you kill more than one person.
...... HERO WA FAMILIA ANAYEANGAMIZA FAMILIA ZINGINE ANAFAA KUITWA HILO KATIKA ILO TAIFA?? HERO AWE NA UHALALI WA KUUA WENGINE ILA YEYE AISHI??

Hata ivo nakupongeza kwa kutumia haki yako uliyopewa na Jamhuri chini ya ibara ya 18(a)
 
Last edited by a moderator:
Gsana;

Siku zote ukitaka kujibu swali, kitu cha kwanza unapaswa kuelewa hicho kilichozungumzwa/kuandikwa.

Tell me something, kwa mawazo yako wewe, unadhani kwanini capital punishment haitekelezwi inavyotakiwa?

Ninaposema corruption, simaanishi as sababu ya kuiondoa corruption. Ninachomaanisha ni equality in the eyes of the law. Ni lazima kuwe na usawa kwenye kutekeleza adhabu hii either kwa mwenye pesa ama asiye na pesa, endapo itabase upande mmoja then its useless.... icho ndicho nilichokiongelea hapo.

Niambie kitu rafiki, Kama watu wangekua matajiri, unadhani ni kwa grounds zipi tungesema taifa ni masikini? Taifa linajengwa na nani?

Swali langu la mwisho kwako Mheshimiwa, Unadhani ni kwanini sheria zimeundwa?
 
Last edited by a moderator:
Siku zote ukitaka kujibu swali, kitu cha kwanza unapaswa kuelewa hicho kilichozungumzwa/kuandikwa....
Tell me something, kwa mawazo yako wewe, unadhani kwanini capital punishment haitekelezwi inavyotakiwa?
Ninaposema corruption, simaanishi as sababu ya kuiondoa corruption. Ninachomaanisha ni equality in the eyes of the law. Ni lazima kuwe na usawa kwenye kutekeleza adhabu hii either kwa mwenye pesa ama asiye na pesa, endapo itabase upande mmoja then its useless.... icho ndicho nilichokiongelea hapo...
Niambie kitu rafiki, Kama watu wangekua matajiri, unadhani ni kwa grounds zipi tungesema taifa ni masikini? Taifa linajengwa na nani?
Swali langu la mwisho kwako Mheshimiwa, Unadhani ni kwanini sheria zimeundwa?

rafiki msitari wako wa mwisho unajibu la swali ulilouliza kwenye msitari wako wa pili.
Msitari wako wa mwisho ni jibu kwa mada unayoitetea...Unadhani ni kwanini sheria zimeundwa?[/QUOTE]

Tatizo kuu ninaloliona kwako unaongelea Haki kwa wenye pesa na wasio na pesa , apo nadhani ni mada tofauti na si sababu za utekelezwaji wa adhabu ya kunyonga/ kunyongwa!!

....Kama watu wangekua matajiri, unadhani ni kwa grounds zipi tungesema taifa ni masikini? Taifa linajengwa na nani?....mkuu sipendi kukurudisha shule, unataka kueleza kuwa haujui kuwa uchumi unaweza kumilikiwa na state ila watu wakawa poor?? unataka kueleza kuwa haujui kuwa watu wachache wanaweza kumiliki uchumi wa nchi na wengine wengi wakawa mafukara? au unataka kusema haujui kuwa taifa linaweza kuwa tajiri ila watu wake hawamiliki uchumi?? unataka kusema haujui kuwa panaweza kuwapo na foreign investments ambazo zinadrain uchumu kwenda mataifa ya nje ula watu wake wakawa maskini?? mfano mdogo nenda nyamongo ujionee barabara, huduma za jamii na elimu ilivoduni kisha uulizie madini yaliyochimbwa pale yana thamani gani? au tusiende mbali, una habari kuna watanzania wanamiliki traillers zaidi ya mia nane mtu mmoja wakati kuna mtanzania anakosa elfu 24,000 karo ya sekondari mwaka mzima??
Unayo habari watu wanamiliki nyumba moja hapa nchini ya milioni elfu moja mia tano kama bilioni pointi wakati mwenzie anaishi nyumba ya matete??

Una habari kuna mtu anaenda kufanya check up india wakati mtwara mzazi anakosa vifaa vya kujifungua anakufa kwa kukosa izo dhana?? au tunapoongelea taifa tajiri ila watu wake maskini , haraka wewe unafikiria nini??
Per capita income imekaa kisiasa, ya kugawanya pato la taifa kwa kila mtu wakati uyo mtu mwingine kawekea figure ambayo hata iweje hawezi kuimiliki!!

Unasema....Ni lazima kuwe na usawa kwenye kutekeleza adhabu hii either kwa mwenye pesa ama asiye na pesa, endapo itabase upande mmoja then its useless.... icho ndicho nilichokiongelea hapo...
Mkuu kumbe shida yako sio uwepo wa adhabu hii, bali ni uwepo wa usawa katika utekelezaji/??
Ungekuwa straight ungeeleweka lakini mada hakuhusiana na uwepo wa usawa bali kutokuwepo kwa adhabu hii.

Kwa aya....Niambie kitu rafiki, Kama watu wangekua matajiri, unadhani ni kwa grounds zipi tungesema taifa ni masikini? Taifa linajengwa na nani?..... mkuu taifa linakuwepo 'stand alone' na halijengwi, taifa/state ni political area na watu ugawanywa kwenye misingi ya mipaka iyo ya kisiasa, labda taifa uwa linawekwa na watawala, ndio maana Sudani imegawanywa kuwa Kusini na Kaskazini na likewise mataifa mengine. Je huo ndo ujenzi?? au unaongelea maendeleo ndo ujenzi?

Mkuu sijui unanipata apo??

Gsana.
 
rafiki msitari wako wa mwisho unajibu la swali ulilouliza kwenye msitari wako wa pili.
Msitari wako wa mwisho ni jibu kwa mada unayoitetea...Unadhani ni kwanini sheria zimeundwa?

Gsana.[/QUOTE]

Uchumi wa aina yoyote unapotikisika nchini lazima kuwe na negative effect kwa taifa letu....
Unequallity ya kwenye capital punishment ni kuonyesha madhara ya adhabu hiyo na si kutaka watu wanyongwe.
Ivi wewe umemaliza kusoma?
 
Binafsi napenda iendelee kuwepo,tena mtu auliwe taratiiiiibu huku akiyahisi maumivu makali kabla ya kufa (guys wa Human Rights nyamazeni!!!!)...yaani mhukumiwa kifo ateswe mpaka kufa (tortured to death) kabla ya kuuliwa.

Msingi wa hoja yangu ni kuwa, hata kama mhukumiwa kifo ni chizi ni wazi kuwa huwa ana hisia za maumivu kama binadamu wengine tunapodhuriwa miili yetu,pia afe ili siku nyingine asijerudia kosa lilelie na iwe funzo kwa wengine.

Vivyo hivyo kwa wabakaji (wa kiume), zitengenezwe mashine (za vyuma zenye ncha kali na za kuchoma,za moto, zenye kuumuka kuongezeka upana) nao waingiziwe kwenye a.nus zao...waharibiwe kiasi kwamba akitembea tu anajulikana yule aliwahi kubaka na akaadhibiwa ipasavyo.
Wabakaji(wa wa kike) vivyo hivyo pia,ili akimgawia mtu ke yake anakutana na ocean iliyopitiwa na earthquakes zikaharibu kabisa.
 
Doppleganger
umeenda mbali sana.

kila jambo lina mipangilio na kanuni zake sisi duniani tulikuja na manifesto yetu.ktk kitabu cha Leviticus mungu ndio aliamrisha atakaeua auwawe! sipendi kuwa quotted lakini chunguza au wanaopenda kusema waseme Nyerere, Mzee Ruksa, Mzee wa uhakika Ben nani aliua? na kwa nini? Swahiba wetu anaondoka keshokutwa tu,Je ameua au ataua? why?

hukumu ya kifo msiseme imepitwa na wakati it is the right purnishment for one who kills or rapes. Na unapo msomea mtu sentence ya kufa, after all his appeals sioni marais wanawaweke wa nini, They would kill them soon after that! whem you pardon him amd lessen his sentence to that of life term my learned brother you are not linient to the culprit you are giving him more hardship and just wasting govt money to tame a useless person.
 
Ni vema adhabu iwe ni funzo kwa alietenda kosa, haina maana kumaliza kabisa nafasi ya mtu kubaadilika adhabu ya kifo sio uamuz sahihi hata kidogo... mwisho wa kuteekelezwa kwa adhabu ya kifo ni awam ya pili.. awamu nyingine zilizofata haijatekelezwa
 
Adhabu ya kunyongwa ni matunda ya mtu aliye vunja she ria ya mauaji.she ria IPO ili ifuatwe so vyombo vya kusimamia khaki vifuatwe na hekima pia itumike
 
Adhabu ya kuua ana hukumiwa mtu aliye ua tu na lengo ni kumfanya muuaji aweze kupata malipo yalele kutokana na alicho kifanya mwana pholosophia BETHAM ame elezea vizuri kuhusu adhabu hii na adhabu nyingine
 
Inasaidia sana kuwepo kwake kuliko kutokuwepo,adhabu sio kifo Kwa maana ya kuwa mhusika akiwa ameshakufa, lakini ni adhabu kabla na wakati wa kufa.

Faida zake ni kuwa mtu huyo ataacha somo(funzo) kwa wengne wenye tabia kama yake,lakini pia yeye kama tatizo anakuwa hayupo tena,kwa maana hio hawezi kusababisha tatizo jigne kwani anakuwa hayupo tena.

so bora iwepo kuliko kutokuwepo kwake na hasa kwasababu watu wamekuwa wakihofu kuua wakijua watauawa pia kulilo kama wakijua watafungwa kifungo cha maisha tu.
 
Doppleganger
umeenda mbali sana.
kila jambo lina mipangilio na kanuni zake sisi duniani tulikuja na manifesto yetu.ktk kitabu cha Leviticus mungu ndio aliamrisha atakaeua auwawe! sipendi kuwa quotted lakini chunguza au wanaopenda kusema waseme Nyerere,Mzee Ruksa, Mzee wa uhakika Ben nani aliua? na kwa nini? Swahiba wetu anaondoka keshokutwa tu,Je ameua au ataua? why?

hukumu ya kifo msiseme imepitwa na wakati it is the right purnishment for one who kills or rapes. Na unapo msomea mtu sentence ya kufa, after all his appeals sioni marais wanawaweke wa nini, They would kill them soon after that! whem you pardon him amd lessen his sentence to that of life term my learned brother you are not linient to the culprit you are giving him more hardship and just wasting govt money to tame a useless person.

Hawatekelezi kwa kuwa wao wenyewe ni wauwaji, hivyo dhamira zinawatesa.
Kifo sio adhabu Bali ni taarifa ya kwamba jamii haikuhitaji kwa kitendo ulichotenda.

Inaitwa adhabu ili kuipunguzia heshima yake, ukweli ni kwamba binadam anayeua mwenzake kwa makusudi hafai kuwa miungoni mwa wanajamii anafaa kuondolewa kwenye jamii kwa kukatishwa uhai wake.
Ni vigumu kuelewa uzito wa mtu kutwaa uhai wa mwingine hadi pale MTU atapotwaa uhai wa mpendwa wako.
Ingekuwa mjadala uwe limited kwa wale ambao wapendwa wao wamewahi kuuliwa na wale ndugu wa wauaji. Lakini wengi wetu hstujui thamani ya uhai hivyo tunafikiri hakuna sababu ya kutoa uhai wa mtoa uhai kwa kuwa uhai wake Una thamani kubwa kuliko wa yule aliyemtoa.

Kwangu kuondolewa uhai kwa muuaji wa makusudi ndiyo njia pekee ya kupunguza wauaji katika jamii.
Hakuna sababu ya kuchelewesha kumuua muuaji unless kuna hoja au utata katka uendeshaji wa kesi.
Watawala hawatekelezi kwa kuwa wenyewe haeastahili kuwepo kwenye jamii hii Kama kweli sheria ingefuatwa kwa haki.
 
Maada nzuri sana, lakini majibu hayatoshelezi haja( not adequate). Whether adhabu ya kifo ni sahihi or siyo sahihi inatakiwa ichambuliwe kwa mtazamo wa kisheria na siyo kihisia (emotional).

SECTION 197 OF THE PENAL CODE OF TANZANIA (cAP 16)

Section 197 of the penal code provides inter alia that, Any person convicted of murder shall be sentenced to death:
*Hii inamanisha kwamba kila atakaye patikana na hatia ya mauaji atahukumiwa kunyongwa.

MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU ADHABU YA KIFO

Serikali inasimamia adhabu ya Kifo kwa mujibu wa sheria. kwa kuwa kosa la mauaji limeharamishwa na sheria za nchi, hivyo basi ni jukumu la Serikali kupitia sheria zilizotungwa na Bunge kuwalinda raia wake dhidi ya udharimu/Ukatili.

NINI MAANA YA MAUAJI (MURDER)

Sheria ya adhabu(penal code, Cap 16) particularly on section 196 provides for the difinition for murder, it provides that ,
Any person who of malice aforethought causes the death of another person by an unlawful act or omission is guilty of murder.

MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA ADHABU YA KIFO

(1) MAUAJI (MURDER) Contrary to section 196 of the penal code

(2) UHAINI (treason) contrary to section 39 (1) of the penal code

Note: watu waliopiga mawe msafara wa Rais Kikwete huko mbeya wangeweza kushitakiwa kwa uhaini na wangeweza kunyongwa kwa mujibu wa sheria inavyosema.

ADHABU YA KIFO NI SAHIHI OR SIYO SAHIHI

Kumekuwebu mjadala mkubwa kuwa adhabu ya kifo siyo sahihi kwani inakinzana na Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 14 kwamba kila mtu ana haki ya Kuishi. na hoja ni kwamba sheria ni mbaya, inatoa Haki kwa mkono wa kulia na kuichukua kwa mkono wa kushoto.

KESI ZENYE HISTORIA (LANDMARK) KUHUSU ADHABU YA KIFO

Kesi iliyohusisha serikali dhidi ya Mbushuu, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilitoa Hukumu ya Kifo. ni Kesi yenye umaarufu wa aina yake kwani ilileta kutunishiana Misuli kwa Majaji wenyewe na Serikali kwa Upande Mwingine.

AGNES DORIS LIUNDI VS. REPUBLIC(1979)

Aliyekuwa mke wa Jaji Liundi ambaye ni mama Mzazi wa Taji Liundi (Mtangazaji wa TBC1) alihukumiwa Kunyongwa na mahakama Kuu ya Tanzania, kwa kupatikana na hatia ya Mauaji. at last, alisamehewa na Rais (Mwl. Nyerere)

DINI VS SHERIA ZA NCHI

Kwa mtazamo wa dini siyo sahihi kuhukumu mtu kwa kuwa mwenye mamlaka hayo ni mwenyezi Mungu Pekee. However, kwa kuwa serikali haina dini, adhabu hiyo inaendelea kuwa sahihi, until otherwise amended to suffice the interest of the ruling class...!!

POINT TO NOTE:

Dunia ya leo sio sehemu salama ya kuishi. changamoto ni nyingi sana. uharifu wa kutisha na binadamu amekuwa katili kumshinda hata shetani.hivyo basi adhabu za kifo haziwezi kufutwa, mpaka jamii inakapostarabika na itachukua muda mrefu sana kufika huko.

Wasalaam
 
Anyway...uwepo wa sheria ni kitu kingine na enforcement yake ni kitu kingine! Hukumu ya kifo kwa tz ipo tu kwenye vitabu nadhani! Kutekelezeka ni kugumu. Silent Actor kaeleza kiasi hapo juu! Sasa kuliko wahukumiwe kifo ilhali wanarundikwa tu huko, bora watafutiwe adhabu nyingine kali ambayo itawaumiza na kuwafanya wajutie kosa lao maisha yao yote!

Kuhusu kufuta hukumu nyingne mbadala mm nahc haitowezkana. . na kuhusu kurundkana jela sheria inasema hata baada ya mtuhumiwa kuhkumiwa adhabu ya kifo mpka Rais wa jamhuri azihirishe na adhabu hiyo na baadae atie saini kwenye utkelzaji wake.. Shida inakuja wapi maraisi wetu hawki kusaini..

Hiyo ndo sabbu ya hao watu kujaa tu gerezani na kunnepea hovyo...
 
Back
Top Bottom