Wabunge wa Zimbabwe waunga mkono kufutwa kwa adhabu ya Kifo nchini humo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1707302546797.png

ZIMBABWE: Waziri wa Habari wa Zimbabwe, Jenfan Muswere amesema Bunge la nchi hiyo limekubaliana na pendekezo la Serikali kufanya mabadiliko ya Sheria ya Adhabu yanayotaka kufutwa moja kwa moja kwa hukumu za Kifo.

Waziri huyo amesema uamuzi huo unatokanana na Maoni ya Wananchi ambapo wengi walishauri kuondolewa kwa adhabu hiyo kwa maelezo inakiuka Haki za Binadamu. Kama Bunge litaidhinisha mabadiliko yaliyopendekezwa, Kifungo cha Maisha itakuwa ndio adhabu kubwa ya mwisho.

Ikumbukwe, Rais wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa aliwahi kuhukumiwa Kifo mwaka 1965 baada ya kudaiwa kulipua Treni kwa Bomu, hukumu ambayo ilibatilishwa baadaye. Zimbabwe haijatekeleza hukumu hizo tangu mwaka 2005.

=============

Zimbabwe's cabinet has supported proposed legislation to end the death penalty, marking a pivotal point in abolishing capital punishment in the southern African country.

Information Minister Jenfan Muswere on Tuesday said that the cabinet's decision was made following countrywide consultations.

Should parliament approve the bill, life imprisonment will serve as the maximum sentence.

President Emmerson Mnangagwa has previously criticised capital punishment.

He was sentenced to death in 1965 following accusations that he bombed a train while fighting against white minority rule.

Mr Mnangagwa's death sentence was, however, commuted after his lawyers argued that he was underage.

Zimbabwe's death penalty is a remnant of a colonial-era law. The country has not carried out an execution since 2005.

BBC
 
Na Tanzania inatakiwa tufanye hilo na sisi kwa sababu kwa sheria kama hii utekelezwaji wake katika nchi kama Tanzania umekuwa mgumu sana.

Unakuta rais mwenyewe anaamuru mtu fulani auwawe kinyemela kwa fitina za kisiasa na huyu huyu rais tena unakuta katiba feki inamlinda kwamba yeye hawezi kuwajibika kwa uovu alioufanya hata anapokuwa ametoka madarakani.

Sasa kwa nini wengine wahukumiwe kunyongwa kwa uovu walioufanya na pengine unakuta sheria hii inatakiwa kutekelezwa on grounds of miscarriage of justice kwani unakuta mtu katiwa tu hatiani ila kwa ukweli wa mwenyezi Mungu wala hajaua kabisa mtu.

Uingereza waliamua kuifuta hii sheria katika karne ya 19 baada ya mtuhumiwa kunyongwa kwa hukumu ya mahakama na baadaye mtu aliyedaiwa kuuawa kupatikana akiwa hai
 
Mimi ni mfuatiliaji sana wa documentaries, series na podcast kuhusu serial killers, ktk case zote nilizofatilia na kutizama mpaka sasa hii adhabu ya kifo ni muhimu tu iwepo, kuna binadamu hawakustahili kuwa binadamu kabisa.
 
Back
Top Bottom