VoiceOfReason
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,194
- 1,355
"Why do we Kill People who Kill People to Show that Killing People is Wrong ?"
Je ni sawa kuwa na Hukumu ya Kifo?
Baada ya yule Chizi wa Norway kuua kadamnasi ya watu (ukizingatia Norway life Sentence ni limited kwa miaka 21 tu) Je ni muhimu kuwa na hukumu ya kifo? Ni nini hasa faida ya hukumu ya kifo?
Je hukumu ya kifo inafanya watu waogope kutenda maovu kwahiyo ni njia nzuri au ni kuonyesha hata sisi hatuna tofauti na waliofanya hayo maovu?
I can argue kwamba huenda hukumu ya kifo ni adhabu rahisi sababu badala ya kumfanya mtu ku-suffer kwa kosa lake, tunampumzisha. Je sio vema kumfunga mtu maisha na kumfanyisha kazi ngumu kwa maisha yake yaliyobaki na kila alichonacho au atakachokitengeneza kiende kwa wale aliowatenda?
What do you think?
The answer is simple, "death penalty haina maana".
Tafakari mifano hii:
1. Mtu akiuwa tunataka nasi tumtendee hivyo, yaani tit for tat (jino kwa jino, jicho kwa jicho). Hii ni tafsiri potofu make ni tabia ya kinyama tu kulipiza kuuwa kwa kuuwa, kubaka kwa kubaka. Matokeo yake vifo, ubakaji utaongezeka badala kupungua.
2. Kwa vile kuuwana ni unyama, imetokea mara kadhaa ajira ya kunyonga watu kukosa waajiriwa hasa nchi kama malawi watu hurundikana gerezani wanyongaji hawaonekani. Je wanaoshabikia adhabu hii wapo tayari kwa tenda hii?
3. Adhabu hii ni feki, make kwa kuhofia kutia saini ya kuidhinisha kifo, tangu utawala wa Mkapa, hapa tz hajanyongwa mtu. Ni Nyerere na Mwinyi tu walioidhinisha.
4. Watu wengi hushabikia adhabu hii kwa vile hawahusiki moja kwa moja kama kutia saini na kutia kitanzi shingo ya mtuhumiwa. Mifano michache hapo juu inaonesha ugumu wa jambo hili.
5. Kwa mujibu wa maendeleo na ustaarabu wa kisasa uliotukuka, Haki ya Kuishi kwa Binadamu (Right to life) haiwezi kunyang'anywa na yeyote, regardless kosa lililofanyika. Ndo maana marais wengi wenye kuheshimu hili hawaweki saini.
Hitimisho:Tutumie njia mbadala za kuwafanya wakosaji watumikie adhabu zao huku wakizalisha mali katika magereza ili tukuze uchumi badala ya kushabikia visasi vya kuuwana na kulawitiana.
Maada nzuri sana, lakini majibu hayatoshelezi haja( not adequate). Whether adhabu ya kifo ni sahihi or siyo sahihi inatakiwa ichambuliwe kwa mtazamo wa kisheria na siyo kihisia (emotional).
SECTION 197 OF THE PENAL CODE OF TANZANIA (cAP 16)
Section 197 of the penal code provides inter alia that, Any person convicted of murder shall be sentenced to death:
*Hii inamanisha kwamba kila atakaye patikana na hatia ya mauaji atahukumiwa kunyongwa.
MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU ADHABU YA KIFO
Serikali inasimamia adhabu ya Kifo kwa mujibu wa sheria. kwa kuwa kosa la mauaji limeharamishwa na sheria za nchi, hivyo basi ni jukumu la Serikali kupitia sheria zilizotungwa na Bunge kuwalinda raia wake dhidi ya udharimu/Ukatili.
NINI MAANA YA MAUAJI (MURDER)
Sheria ya adhabu(penal code, Cap 16) particularly on section 196 provides for the difinition for murder, it provides that ,
Any person who of malice aforethought causes the death of another person by an unlawful act or omission is guilty of murder.
MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA ADHABU YA KIFO
(1) MAUAJI (MURDER) Contrary to section 196 of the penal code
(2) UHAINI (treason) contrary to section 39 (1) of the penal code
Note: watu waliopiga mawe msafara wa Rais Kikwete huko mbeya wangeweza kushitakiwa kwa uhaini na wangeweza kunyongwa kwa mujibu wa sheria inavyosema.
ADHABU YA KIFO NI SAHIHI OR SIYO SAHIHI
Kumekuwebu mjadala mkubwa kuwa adhabu ya kifo siyo sahihi kwani inakinzana na Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 14 kwamba kila mtu ana haki ya Kuishi. na hoja ni kwamba sheria ni mbaya, inatoa Haki kwa mkono wa kulia na kuichukua kwa mkono wa kushoto.
KESI ZENYE HISTORIA (LANDMARK) KUHUSU ADHABU YA KIFO
Kesi iliyohusisha serikali dhidi ya Mbushuu, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilitoa Hukumu ya Kifo. ni Kesi yenye umaarufu wa aina yake kwani ilileta kutunishiana Misuli kwa Majaji wenyewe na Serikali kwa Upande Mwingine.
AGNES DORIS LIUNDI VS. REPUBLIC(1979)
Aliyekuwa mke wa Jaji Liundi ambaye ni mama Mzazi wa Taji Liundi (Mtangazaji wa TBC1) alihukumiwa Kunyongwa na mahakama Kuu ya Tanzania, kwa kupatikana na hatia ya Mauaji. at last, alisamehewa na Rais (Mwl. Nyerere)
DINI VS SHERIA ZA NCHI
Kwa mtazamo wa dini siyo sahihi kuhukumu mtu kwa kuwa mwenye mamlaka hayo ni mwenyezi Mungu Pekee. However, kwa kuwa serikali haina dini, adhabu hiyo inaendelea kuwa sahihi, until otherwise amended to suffice the interest of the ruling class...!!
POINT TO NOTE:
Dunia ya leo sio sehemu salama ya kuishi, changamoto ni nyingi sana. Uhalifu wa kutisha na binadamu amekuwa katili kumshinda hata shetani. Hivyo basi adhabu za kifo haziwezi kufutwa, mpaka jamii inakapostarabika na itachukua muda mrefu sana kufika huko.
Wasalaam!