Adhabu ya Kunyonga Hadi Kufa imepitwa na wakati?

VoiceOfReason;

kuna mda mwingine unaweza nyonga mtu kumbe hakufanya kosa.mtu kama ushahidi unautata huyo apewe life sentence.ila mtu kafanya kosa alafu kaone kana live mfano aliekutwa anauza nyama ya binadamu huyo hakuna mjadala ni kumfanya kama alichofanya kama china
 
any person who with malice aforethougt causes death of another person is the guilty of murder, shall be punished to suffer death through hanging , PENAL CODE CAP 16 R.E 2002, mjadala uanzie hapa wakuu
 
Jukumu la jeshi la Magereza ni urekebishaji.sasa death sentence au life sentence haiendani na hiyo kauli mbiu ya Magereza ya Magereza.
 
Kufungu hicho cha Penal Code kinachoamru kifo kw mtu aliepatikana na hatia kinakinzana na Haki za binadam za umoja wa mataifa vilevile kinakinzana na ibara ya kumi na mbili ya katiba Tanzania ya mwaka 1977. Hivyo adhabu ya kifo imepitwa na wakati.
 
hapa tunaangalia unyeti wa kosa lililotendwa.
kwani hii hukumu ipo pale kama deterrent (watu wasifanye kosa kama hilo) au ipo pale kama haki kwa mtendewa au kama adhabu (na kama ni adhabu huoni kwamba sometimes kifo is an easy way out)
 
Hakuna sababu za kulumbana .she ria ni sheria ,swala la wakati sio muhimu. Hakuna wakati wowote ambao kifo cha MTU yeyote nje ya mapenzi ya Mungu kinahitaji HURUMA. Anae advocate HURUMA namwona nae Kuwa muuaji. Kwa kifupi tii amri ya "USIUE".
 
yap ni sawa kuwa na hukumu ya kifo....
(kwa watu kama mafataki na wabakaji)

(ingawa kwa upande wa Dini especially Christianity hairuhusiwi
kumuhukumu mtu)

Wapi katika Christianity hakuna hukumu ya kifo? Au umesahau sheria ya jicho kwa jicho , mkono kwa mkono.?

Sheria za biblia ndizo sheria za nchi.
 
VoiceOfReason;

Upo sawa,ila magereza yetu ni madogo however Tanzania Inahukumu watu kifo lakini hajanyongwa mtu kwa kipindi kirefu sasa.Kwahiyo ni bora ibaki ilivyo
 
ImageUploadedByJamiiForums1404285946.354885.jpg

Kutokana na uthibitisho uliopatikana katika majarida, vitabu na hata historia havijathibitisha nani au taifa lipi waasisi wa hukumu hii ,ila inathibitishwa tu kuwepo kwa hukumu hii miaka 600 kabla ya Yesu Kristo, wachunguzi wa mambo wamethibitisha hata baada ya kuzaliwa Yesu hukumu hiyo ilitumika kwani hata Yesu alihukumiwa hukumu hiyo kwa kuwambwa msalabani.

Leo hii tumeona mataifa mbalimbali yakiboresha hukumu hii kama sindano ya sumu (USA) kitanzi cha kamba(Iraq) kupigwa risasi (Libya) pia tumeona mataifa mbalimbali kuipinga na kuifuta kabisa hukumu hii.

Hii tumeona kama umoja wa nchi za ulaya EU moja ya masharti ya kujiunga na umoja huo ni kuipinga na kutotekeleza kwa hukumu hiyo , pia katika nchi za Africa nchi kama Rwanda ,South Africa hukumu hii kandamizi haitumiki na haipo.

kutotekelezwa kwa hukumu hii kwa bahadhi ya nchi hapa duniani imetokanana na kuthibitika kwamba hii hukumu kandamizi pia inakwenda kinyume na haki za binadamu vile vile inakinzana na hukumu zingine kama anaeuwa nae auwawe basi anaebaka nae abakwe!!
 
Mi naipinga hukumu ya kifo siku zote,ila tatizo mtazamo wa jamii unaonekana kuikubali,hv unaweza mwambia mtu aliyeuliwa ndugu yake albino,asitake muuaji naye asihukumiwe kifo,kinachotakiwa elimu kwanza ifanywe kampeni maalum nchin,labda watu watabadili mitazamo,tuachane na adhabu hii!
 
kwa upande wangu hukumu ya kifo bado inahitajika sana tz na tutafanya kosa kubwa sana tukiifuta.maana kutakuwa hakuna cha kuwaogohopesha wauaji tena. si mnajua tena dhumuni la adhabu ni kuonya mtenda kosa,kumfundisha mkosaji pia kuwaonya watu wengine wasifanye hivyo kama mtu akihukumiwa kunyongwa basi watu walo salia watogopa kuua.dhumuni hasa la adhabu ya kifo kuonya na kutisha wengine wasifanye lile kosa hivyo basi imeleta amani mitaani
 
kwa upande wangu hukumu ya kifo bado inahitajika sana tz na tutafanya kosa kubwa sana tukiifuta.maana kutakuwa hakuna cha kuwaogohopesha wauaji tena. si mnajua tena dhumuni la adhabu ni kuonya mtenda kosa,kumfundisha mkosaji pia kuwaonya watu wengine wasifanye hivyo kama mtu akihukumiwa kunyongwa basi watu walo salia watogopa kuua.dhumuni hasa la adhabu ya kifo kuonya na kutisha wengine wasifanye lile kosa hivyo basi imeleta amani mitaani


Kama dhumuni la kuonya na kutisha, huyo unaemnyonga atakua ametishika vipi au kuogopa vipi kwamba next time asifanye hivyo? ama kuonya huko ni kwa wale wanaobaki?
Be honest bwana... dhumuni la kunyonga ni kuua and according to them watasema wamepunguza criminals...
 
Mimi kwa mawazo yangu nadhani hukumu ya kunyongwa haitufai kwasababu zifuatazo;
1. Kunyonga mtu kwa kwa kosa la kuua ni sawa na kurudia kosa la huyo aliyeua na kujificha nyuma ya mgongo wa sheria.

2. Hakuna usawa wa haki nchini kwetu so watu watakaokuwa wananyongwa ni wale watakaokua wanashindwa kutoa corruption so kwa hili, tutapaswa kuita haki au mauaji?

3. Nchi yetu ni masikini sana. Kumpoteza mtu mmoja katika taifa letu ni sawa na kupoteza nguvukazi ya taifa letu. Hao wanaopaswa kuuwawa wanapaswa kupewa kazi tofauti waweze kucontribute chochote kwa taifa lao.

4. Nadhani art 13 inaongelea right to life. Kuwa na hii adhabu ni sawa na kufundisha jamii jinsi ya kukiuka sheria zilizowekwa.

5. Hao watu wanaonyongwa, l believe wana watu wanaotegemewa, so killing a hero wa familia its like you kill more than one person.
......
Nawakilisha.
 
mkimaliza kupinga hukumu hii ikafanikiwa, pia mpinge kufungwa maisha maana nayo iko kinyume kumnyima mtu rights and freedom....

Ikkisha pia pinga kufungwa maana ni kuondoa private liberty....
 
Back
Top Bottom