Acha kujidanganya pesa sio kila kitu

Acha kujidanganya pesa sio kila kitu

Kilichomfanya awe hai wala sio pesa ni Neema ya Mungu tu,
Kumbuka alipata ajali na hakufa je pesa inaweza kumuokoa mtu na kifo cha ajali?
Wapo matajiri weeengi wameshindwa kujiokoa na kifo kwa pesa.
Pesa sio kila kitu ndo maana hata bill gate aliachana na mke wake pia jeff bezo aliachana na mkewe pesa hazikuwasaidia kwenye hilo na wanamiliki zaidi ya dollor billion 100.
Pesa inatoa tu utatuzi kwa mambo yanayoshikika( tangable things) lakini haifanyi lolote kwa mambo ambayo hayashikiki
Mfano unaweza nunua mwanamke na kufanya nae mapenzi lakini huwezi kumnunua mwanamke ali akupende utafeli
Asante nawasilisha
Kwa hiyo we mzee unaamini huyo mwamba yupo hai sio kisa pesa? Una matatizo kidogo kwenye kufikiri.

Uko sahihi kwamba kwenye ajali pale aliyemuokoa ni Mungu na si pesa, ila kinachomfanya yupo hai hadi leo ni pesa, angekuwa hana pesa angeshakufa zamaaaaaaani. Pesa ndo imemfanya hajafa hadi sasa
 
View attachment 3318502
Huyu hapa Prince Al-Waleed bin Khaled bin Talal, ambaye anafahamika ulimwenguni kwa jina maarufu la “Sleeping Prince” April 18 mwaka huu, alitimiza umri wa miaka 36, ambapo umri huo umemkuta akiwa bado kitandani ‘coma’ bila fahamu zozote.

Mwanamfalme huyo wa Saudi amekuwa kwenye hali hiyo ya kupoteza fahamu ‘coma’ tangu mwaka 2005 kufuatia ajali mbaya ya gari ambayo aliipata Jijini London, Uingereza. Kwa miaka 20 sasa, Maisha ya Prince yanategemea mashine ya kupumulia, hata kula yake ni kupitia mipira.
unamwonea huruma lakini jamaa anainjoy sana,,mimi huwa kuliachia shuka alfajir huwa ni mtihani mkubwa!! "USINGIZI RAHA SANA"
 
K

Kweli mkuu,Kuna siku tuko na Boss wangu, yeye alikuwa mtu wa kujisikia sana na kujiona MSOMI sana na kudharau watu!Siku Moja tumeeenda Singida njia ya Kwamtoro,Ambaye kapita njia hiyo ,anapajua ni mapori kwa kweli.
Tukiwa njiani gari ikapata pancha na rimu likawa limepinda na spare tyre halina upepo na hakuna magari yanayopita mara kwa mara!Kipindi hicho Hamna Hawa bodaboda,hivyo pikipiki ni za shida pia.Mimi nimekulia vijijini na nayaelewa maisha ya vijijini.Nikatafuta wanakijiji Rika langu,nikawaeleza shida yetu ya gari nk.Hali ikabadilika msaada Hakuna Basi linalopita hapo,ni Moja tuu na linaenda asubuhi na kurudi jioni.Bosi mazingira kwake haya ni mapya!Yule kijana niliyemfanya Rafiki,ndie Tukawa tunamtumia kwa dharula pale,Boss hana hata Moja hajui tunatokaje hapo ,Njaa,Njaa,Dogo akatutafutia kuku ,akasonga na ugali.Kumbuka tuna hela na tuko na Boss ila hapo hakuna Bar,Mgahawa Wala duka! Wanategemea minada ya kila mwezi kununua mahitaji Yao .Baada ya hapo asubuhi tukampa kijana ya kwenda mjini Singida na kuziba pancha na kurudi jioni na tyre!Kwa ufupi boss wangu alijifunza vitu vingi na Heshima debe!.Sure pesa si kila kitu kuna mahali haiitajiki pesa hata uwe nazo!.Mungu mwema humpa ampendaye na Humnyima ampendaye vilevile!
Somo Kali Sana. Kikubwa Tuheshimiane
 
Pesa inasaidia sana lakini haikusaidii kutatua changamoto zote. Kama pesa ingekuwa Kila kitu basi huyo mwanamfalme asingepata ajali yaani pesa zingemuepusha na ajali.

Cc Demi
Hilo lipo wazi huwezi kukwepa ajali na huwezi kukwepa kifo.
Pesa inaweza ikasaidia kusogeza siku zako za kuishi au kupona kabisa kama umepata ajali.
 
Kwa hiyo we mzee unaamini huyo mwamba yupo hai sio kisa pesa? Una matatizo kidogo kwenye kufikiri.

Uko sahihi kwamba kwenye ajali pale aliyemuokoa ni Mungu na si pesa, ila kinachomfanya yupo hai hadi leo ni pesa, angekuwa hana pesa angeshakufa zamaaaaaaani. Pesa ndo imemfanya hajafa hadi sasa
Kuna namna fulani ukweli umekuingia ila bado kidogo nikuchome sindano moja ya maadili ya kutoheshimu fikra za watu,
Narudia tena, kilichofanya aishi hapo sio pesa , inaonekana hujawahi kuumwa au kupata changamoto ambazo utaona pesa ni kama takataka tu bali Mungu ndo kila kitu,
Tambua ya kwamba Mungu ndo ameshikilia uhai wake angeamua hata ile siku ya kwanza tu angeonja mauti.

Umasikini ndio unakufanya uone pesa ni kila kitu kwa kuwa tunaona matajiri wanasitawi
Na umalaya pia ndio unaowafa ya vijaona waone pesa ni kila kitu kwa kuwa watawaonga wanawake wowote wanaowataka
Ngoja nikupe mfano mwingine , Unaweza ukawa na mwanamke ukampa mtaji ya 40m afanye biashara aitakayo, alafu ukamnunulia crown ya 25m ukamjengea nyumba ya wazazi wake ya 38m na bado pesa ya mafuta ya gari unampatia😃😃 na vizawadi vya birthdays.
Kwa haraka hapo juu ni zaid ya 100m umehudumia upande wake.
Ajabu ni kwamba utakuta bodaboda anasimamia kucha bila hata malipo yoyote.
Upendo wa kuwekeza pesa hapo utakuwa umekusaidia nini?
Nawasilisha
 
Well said mkuu.
Yote kwa yote tuombe kuwa na afya njema ili tuzi enjoy pesa tunazopata.
 
Mbona kama heading na yaliyomo haviendani? Umemwona alivyopendeza? Bila shaka anapata first class care pamoja na kwamba yuko kwenye vegetative state. Bila pesa ingewezekanaje kumtunza hivi kwa miaka zaidi ya 20?

Kauli hiyo kwenye heading haikupaswa kutolewa na wewe mwasibu CPA mzima unayeelewa umuhimu wa pesa. Hiyo ni kauli ya kujifariji tu ambayo hutolewa na watu masikini waliojikatia tamaa huko!

Na kama pesa si kila kitu; nini ni kila kitu? Usije tu ukanitajia mambo ya kiasili ambayo binadamu kama kiumbe hawezi kuepukana nayo mf. Kifo, magonjwa, huzuni/furaha, mapenzi/upendo....
New perspective nimeipata..

Tunatafuta tu kitu cha kutufanya tujihisi kama "tumetimilika" Kumbe kwa asili ya ubinadamu wa kutoridhishwa, hata ukipata A utatafuta B ambayo hauna na wengine kama wavumbuzi wanatafuta vitu ambavyo hata havipo ili wapige pesa..

Kiuhalisia hakuna cha kuwa "kila kitu" Kwenye maisha ya mtu, labda tuseme Mungu katika dini.

Na kingine. Kama pesa sio kila kitu lakini ukiikosa unaka huna kitu. Kwa hiyo kutafuta pesa muhimu
 
Nimekuelewa kuwa kama kweli pesa zinasaidia Kwa Kila kitu basi huyo jamaa angekuwa Leo hii anatembea na mzima wa afya kabisa, lakini licha ya pesa za mkojo wa mwarabu lakini Bado kalala na yeye binafsi hazifurahii hizo pesa.
 
Pesa sio kila kitu ni msemo wa kujifariji.
Bila pesa angeshakufa miaka mingi iliyopita ila pesa imefanya wapendwa wao kumuona hadi leo hata kama haongei.
Umewahi kuuguliwa? na imani angekuwa anafahamu angekuwa kashaomba afe zamani tu.
Hii ni kuendelea kuteseka tu na kutesa wenzio sasa hivi wangekuwa wameshasahau na kuendelea na mambo mengine.
 
Kuna namna fulani ukweli umekuingia ila bado kidogo nikuchome sindano moja ya maadili ya kutoheshimu fikra za watu,
Narudia tena, kilichofanya aishi hapo sio pesa , inaonekana hujawahi kuumwa au kupata changamoto ambazo utaona pesa ni kama takataka tu bali Mungu ndo kila kitu,
Tambua ya kwamba Mungu ndo ameshikilia uhai wake angeamua hata ile siku ya kwanza tu angeonja mauti.

Umasikini ndio unakufanya uone pesa ni kila kitu kwa kuwa tunaona matajiri wanasitawi
Na umalaya pia ndio unaowafa ya vijaona waone pesa ni kila kitu kwa kuwa watawaonga wanawake wowote wanaowataka
Ngoja nikupe mfano mwingine , Unaweza ukawa na mwanamke ukampa mtaji ya 40m afanye biashara aitakayo, alafu ukamnunulia crown ya 25m ukamjengea nyumba ya wazazi wake ya 38m na bado pesa ya mafuta ya gari unampatia😃😃 na vizawadi vya birthdays.
Kwa haraka hapo juu ni zaid ya 100m umehudumia upande wake.
Ajabu ni kwamba utakuta bodaboda anasimamia kucha bila hata malipo yoyote.
Upendo wa kuwekeza pesa hapo utakuwa umekusaidia nini?
Nawasilisha
Tubaki kwenye mada, unafikiri mtu anaweza kumudu kukaa hospital miaka 20 kama hana pesa ya matibabu? Hospital gani itakuruhusu ukae miaka hiyo bila malipo? Mzee, huamini kwamba pesa imemuweka hai hadi leo huyu jamaa?

katika vitu vilivyoumbwa na Mungu, hakuna chenye thamani kuzidi uhai.

Vinavyotengenezwa na wanadamu hakuna chenye thamani kuzidi pesa.
Kwa hiyo kwa binadamu baada ya uhai pesa ndo kila kitu.
 
Hii habari inathibitisha kuwa pesa ndiyo kila kitu!

Angekuwa pangu pakavu wangeshafukia na kusahau kitambo.
 
Umewahi kuuguliwa? na imani angekuwa anafahamu angekuwa kashaomba afe zamani tu.
Hii ni kuendelea kuteseka tu na kutesa wenzio sasa hivi wangekuwa wameshasahau na kuendelea na mambo mengine.
NImemuuguza baba yangu miaka 6, hakufikia hali kama ya huyo jamaa ya kushindwa kuongea lakini ameumwa. Na hata siku moja hatukutamani aondoke, tulikuwa na matumaini atapona.
 
View attachment 3318502
Huyu hapa Prince Al-Waleed bin Khaled bin Talal, ambaye anafahamika ulimwenguni kwa jina maarufu la “Sleeping Prince” April 18 mwaka huu, alitimiza umri wa miaka 36, ambapo umri huo umemkuta akiwa bado kitandani ‘coma’ bila fahamu zozote.

Mwanamfalme huyo wa Saudi amekuwa kwenye hali hiyo ya kupoteza fahamu ‘coma’ tangu mwaka 2005 kufuatia ajali mbaya ya gari ambayo aliipata Jijini London, Uingereza. Kwa miaka 20 sasa, Maisha ya Prince yanategemea mashine ya kupumulia, hata kula yake ni kupitia mipira.
unataka kunambia hata bila ya B7 za usajili za MO simba mwaka huu ingefika fainali CAF
 
Back
Top Bottom