14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

Nilikua darasa la tatu, nilikua tu nashangaa shangaa na shulenikafungwa mpaka nyerere alipomaliza kuzikwa
Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.

Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?


Kumbuka.
 
Mkuu si useme kijiji gani?au unaogopa?
Siogopi. Huko ndo kwetu nilikozaliwa na kukulia.
Mwalimu mimi nikiwa mdogo nasoma shule wilayani Bunda, nikiwa nimeenda likizo kwa babu yangu nilikuwa napenda sana shambani kwake kumwona maana ni karibu tu na kwa babu yangu. Wakati huo naona fahari sana kumwona mtu ninaemsoma kwenye vitabu shuleni.
 
**** primary school Mtwara,tumeshapiga paper ya standard seven tunafanya mazoezi ya mahafali,mara paap kengele ya dharula inagonga muda huo mi nipo juu ya mnazi wa shule naangusha madafu,wahuni wenzangu wapo chini wanayafua hahahaa basi tukakusanyika fasta assembly shule nzima,mwalimu mkuu Mama Mwangata anatangaza kwamba nyerere kafariki,wanafunzi wa madarasa ya chini wanalia kwa sauti,walimu wanawatuliza kwamba hakutakua na vita tulieni,that was 14/10/1999...
Same trend kweli mwl alikua jabali graduation ya shule ya msingi iliahirishwa hivi hivi michango ilirudishwa
 
Najiuliza wale vijana waliokimbia toka Uwanja wa ndege hadi mikocheni sijui wapo wapi?

Nakumbuka walikuwa wamevua mashati yao huku wakiimba " Nyerere kafaaa...mtuteseee"
Sasa hivi wengi wao watakuwa 40's.
 
Ndio mkuu! Baadae alikuja kuwa HP
Bila shaka wewe tutakuwa tunafahamiana kwa uzuri, hebu cheki kumbukumbu zako vizuri nadhani alikuwa PM kwa Vyeo vya Kipindi kile ambavyo vilikuwa vinashabihiana na Mfumo wa Kiungozi wa URT..,
 
Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.

Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?


Kumbuka.
Inanikumbusha hapo hapo Iyunga wazee tumejipanga na calculation za Pcm ,paper la O level likahahirishwa wazee tukabaki na madifinition yetu kichwani
 
Nilikuwa shule ya msingi, hakuna wakati shule ilikuwa ngumu kwangu kama wakati ule...nilikuwa nachukia sana shule na kikitokea kitu chochote cha kunifanya nisiende shule nafurahi sana. Nasikitika kusema hata taarifa za kifo cha baba wa taifa zilikuwa za kufurahisha masikioni mwangu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] huku uki pretend una huzuni
 
Nilikuwa naumwa nipo IST clinic tukawa tunaongea na daktari wangu akasema nadhani ameshafariki nikakubaliana nayeye. Alinichoma sindano ya kuondoa maumivu maana lumber yangu ili trip nikiwa mdogo. Kufika home nakuta habari kuwa mwalimu katutoka. Nililia saana. Nilikumbuka fadhila tulizopewa sisi watoto wa maskini, nikakumbuka elimu bure mpaka chuo kikuu, vichere,

kila kitu na chakula cha hali ya 5 star tukiwa secondari!!! Mwalimu ulikuwa dikteta mzuri ambaye ulijali watu wako wa chini hasa sisi walala hoi ila wahindi na waarabu watakulaaani mpaka kesho. Nyumba zao ulizitaifisha, wenzio wakaja kuziuza kama maandazi na kuzihonga kwa hawara zao. RIP teacher.
 
Bila shaka wewe tutakuwa tunafahamiana kwa uzuri, hebu cheki kumbukumbu zako vizuri nadhani alikuwa PM kwa Vyeo vya Kipindi kile ambavyo vilikuwa vinashabihiana na Mfumo wa Kiungozi wa URT..,
Nilikuwa nakaa Faru Mkuu, tunapigia msuli kule Kakunyu ya Faru Wing namba 4 juu labisa karibu na kwa Mwalimu Kasongo na Mwakanyamale kabla hajawa Headmaster
 
Back
Top Bottom