14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

nikiwa kijijini shambani

nakumbuka Sauti ya Mheshimiwa Raisi Benjamin W Mkapa ikitoka katika spika za radio PANASONIC A.K.A "RADIO MBAOooo" yaaani siku nzima nilihuzunika
 
Ilikuwa siku ya graduation. Tuliahirisha shamrashamra
Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.

Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?

Kumbuka.
 
ebwana dah ! Hiyo siku ndiyo nilikua naenda kuvamia bank ila nikasitisha zoezi kwa heshima ya mzee
 
**** primary school Mtwara,tumeshapiga paper ya standard seven tunafanya mazoezi ya mahafali,mara paap kengele ya dharula inagonga muda huo mi nipo juu ya mnazi wa shule naangusha madafu,wahuni wenzangu wapo chini wanayafua hahahaa basi tukakusanyika fasta assembly shule nzima,mwalimu mkuu Mama Mwangata anatangaza kwamba nyerere kafariki,wanafunzi wa madarasa ya chini wanalia kwa sauti,walimu wanawatuliza kwamba hakutakua na vita tulieni,that was 14/10/1999...

Hata sisi pia tulikua kwenye mahafali disco likakatishwa
 
Nilikuwa Mafinga sec! Siku hiyo tulikuwa ziara ya kimasomo Kalenga kuona fuvu la Mkwawa! Nakumbuka nyimbo za Kapten Komba, sijui alizitunga muda gani?
Ndo hapo utajua vifo vya watu muhimu huwa havitangazwi ovyo so kuna uwezekano alikufa tarhe za nyuma kabla lakini mpaka waweke vitu flani saw a... Hivyo hata komba hakutunga usiku mmoja zile nyimbo na hata Kama angetunga ndani ya usiku huo bado recording siyo rahisi kiiivyo (according to my experience)
 
Nilikuwa shule ya msingi, hakuna wakati shule ilikuwa ngumu kwangu kama wakati ule...nilikuwa nachukia sana shule na kikitokea kitu chochote cha kunifanya nisiende shule nafurahi sana. Nasikitika kusema hata taarifa za kifo cha baba wa taifa zilikuwa za kufurahisha masikioni mwangu
 
Nilikuwa drs la 4 s/msingi Uhenga huko MAKAMBAKO Njombe,kiukweli sitaisahau ile siku maana ilikuwa ni ALHAMISI na jioni jioni hivi ndo nilizikia hizo taarifa tukiwa tunashiriki maandalizi ya sherehe ya mahafali ambayo ingefanyika kesho yake.

Lakini siku hiyohiyo tena pale bush kwetu palitokea msiba wa mzee mmoja aliyekuwa anatuhumiwa kuwa bonge la mchawi na alikuwa hapendwi na watu kbs,watu walishangilia balaa kiukweli.
 
Huyu mzee Nyerere alipendwa sana na Taifa hili hatakama kuna mabaya aliyafanya ila hakutaka ubinafsi.

Kila Raia wa nchi hii alimlilia,Daaah mimi nakumbuka nilikuwa Yombo makangarawe kipindi hicho nyumbani kulikuwa na Redio mbao,yani kila stesheni ilikuwa inamtangaza

Yaani mtaa mzima ulipoa daah,Kweli Mwl hatosaulika
 
Nilikuwa drs la 4 s/msingi Uhenga huko MAKAMBAKO Njombe,kiukweli sitaisahau ile siku maana ilikuwa ni ALHAMISI na jioni jioni hivi ndo nilizikia hizo taarifa tukiwa tunashiriki maandalizi ya sherehe ya mahafali ambayo ingefanyika kesho yake.
Lakini siku hiyohiyo tena pale bush kwetu palitokea msiba wa mzee mmoja aliyekuwa anatuhumiwa kuwa bonge la mchawi na alikuwa hapendwi na watu kbs,watu walishangilia balaa kiukweli.
kwa hivyo kijij kiliondokewa na mzee Wa busara
 
Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.

Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?

Kumbuka.
nilikuwa juu yakiuno cha mke wangu
 
Nilikiwa kiwanda cha chai Mbeya nakumbuka nilikiwa na zoez la kusindika kwa siku ya nne mfululizo SAA nne na nusu habari mbaya ikatanda taifa
 
Back
Top Bottom