14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

Nilikuwa form three Itope secondary School Kyela. Taarifa ya kifo Cha baba wa Taifa tuliisikia kupitia redio Malawi ( MBC) ikitamka kwa kitumbuka kwa maneno haya Mwl. Nyerere the former president of the republic of Tanzania alowa. Ilikuwa jioni lakini tuliendelea na shule mpaka kesho yake tukapewa mapumziko.
 
Wengine tunaogopa kusema tulikuwa wapi maana dharau nyingi sana humu[emoji53][emoji53][emoji53][emoji53][emoji849][emoji849][emoji45]
 
Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.

Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?

Kumbuka.
Nilikuwa shuleni darasa la pili baada ya kengele kugongwa na kutangaziwa tulirudi nyumbani.
Mtaani kulikuwa na taharuki kwamba huenda vita ikatokea na hofu za kila namna
 
Nilikuwa form three Itope secondary School Kyela. Taarifa ya kifo Cha baba wa Taifa tuliisikia kupitia redio Malawi ( MBC) ikitamka kwa kitumbuka kwa maneno haya Mwl. Nyerere the former president of the republic of Tanzania alowa. Ilikuwa jioni lakini tuliendelea na shule mpaka kesho yake tukapewa mapumziko.
Itope Sec, alisomaga dingi enzi hizoo
 
Wengine tunaogopa kusema tulikuwa wapi maana dharau nyingi sana humu[emoji53][emoji53][emoji53][emoji53][emoji849][emoji849][emoji45]
Bila shaka hata wazazi walikua bado hata hawajaplan kumpata mtoto mkorinto, usijali kuna watoto wenzio pia humu, you're not alone[emoji3] [emoji3]
 
**** primary school Mtwara,tumeshapiga paper ya standard seven tunafanya mazoezi ya mahafali,mara paap kengele ya dharula inagonga muda huo mi nipo juu ya mnazi wa shule naangusha madafu,wahuni wenzangu wapo chini wanayafua hahahaa basi tukakusanyika fasta assembly shule nzima,mwalimu mkuu Mama Mwangata anatangaza kwamba nyerere kafariki,wanafunzi wa madarasa ya chini wanalia kwa sauti,walimu wanawatuliza kwamba hakutakua na vita tulieni,that was 14/10/1999...
Aisee, very interesting, yaani mliamini vita naweza tokea?? Nakumbuka 1983 wazee walichimbishwa mashimo ya kujifisha kaburu akitushambulia. Sisi tuliyatumia sana kujificha tukicheza kombolela.
 
Nilikuwa shule ya msingi, hakuna wakati shule ilikuwa ngumu kwangu kama wakati ule...nilikuwa nachukia sana shule na kikitokea kitu chochote cha kunifanya nisiende shule nafurahi sana. Nasikitika kusema hata taarifa za kifo cha baba wa taifa zilikuwa za kufurahisha masikioni mwangu
Daaaa mama kweli ulifurahia kifo cha mwl mwenzangu ?
 
Dah! Kweli noma. Siju hz wajisikiaje
Nilikuwa shule ya msingi, hakuna wakati shule ilikuwa ngumu kwangu kama wakati ule...nilikuwa nachukia sana shule na kikitokea kitu chochote cha kunifanya nisiende shule nafurahi sana. Nasikitika kusema hata taarifa za kifo cha baba wa taifa zilikuwa za kufurahisha masikioni mwangu
 
nimesoma comment zote nimeamini kweli watu walikuwa wanampenda sana Nyerere,,,,
ngoja sisi millennia tukae pembeni.........
kuna wale waliofanya sherehe sijawaona bado........
 
Tulikanyagana sana pale tulipokuwa tukiangalia tukio la mazishi live kwenye runinga, Runinga zilikuwa mbili tu mtaa mzima
 
Back
Top Bottom