Bombabomba
JF-Expert Member
- Dec 23, 2017
- 1,864
- 2,200
Dah, siku hiyo nilikuwa Wilayani Mbinga tukinunua Kahawa. Tulitumia magari 109 landrover yakiwa na radio call. Ps wa ofisini alitupigia tuliopo field kwamba baba wa Taifa kafariki. Kimsingi REDIO call wote mnasikia fulan na fulan wanachoongea ila mnapotezea, but ile habari tukaifuatilia wote. Kimsingi SOTE tulijawa na HUZUNI sana. Ilisikitisha. Jioni kufikia Mjini tukawa tunajaa kwenye kumbi za starehe kuona habari kwenye ITV. Kikubwa msiba ule ulikuwa na msisismko ambao haujawahi tokea na sijui kama utatokea tena kwa sababu Viongozi wa sasa wana mahasimu wengi ambao TAARIFA ya KIFO kwa wengine hawajali kama vile huwa FURAHA. Lkn Mwl wananchi wote tulisikitika sana. Mara ya mwisho kumuona Ilikuwa 1995 akimfanyia kampeni Mzee Mkapa. Nilikuona live, jamaa alikuwa na confidence sana. Akanishawishi kupiga kura na nilimchagua Mema enzi hizo anarindima hatareeee!!
RIP Mwalimu!!
RIP Mwalimu!!