14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.

Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?


Kumbuka.
14/10/1999 Nilikuwa najiandaa kumzika Baba Mzazi Marehemu nukifanyiwa uhamisho wa shule ya msingi Mazimbu A Morogoro kwenda kusoma Mara Tarime.

Bele 9(Abednego Nyamoga, Ramadhani, Nicholas na Maneno classmates wezangu nimewakumbuka sana enzi za utotoni daaah [emoji26][emoji56]
 
But kipindi hicho ndio tunajiandaa kuingia mwaka 2000 kuna tetesi zilizagaa kuwa mwaka 2000 itakuwa mwisho wa dunia basi tukawa tunadanganywa tuchukue kamba ya mgomba tufunge vifundo saba alafu tuvae mkononi eti hili tusizulike [emoji1787][emoji1787][emoji1787] utoto shida sana, sasa cha ajabu meals 2000 ukafika tukawa tunadunda kama kawa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.

Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?


Kumbuka.
Kudato cha nne Tanga Technical Secondary School. Nilikuwa dukani nanunua peni wakati Mkapa anatangaza.
 
Hadi naona aibu kuwepo humu [emoji1787][emoji1787][emoji1787], eti mtu alikuwa darasa la pili
Aibu darasa la pili wakati wengine hata kuanza chekechea ilikua bado hata hatukumbuki kitu, tulikua tukiambiwa baba wa taifa alikufa, basi tunashangaa baba wa taifa alikua mkubwa kiasi gani, leo tumeshakua watu wakubwa
 
Nilikuwa moro. Bungo ps school. Mwalimu mwinyi pembe alitutangazia hiyo habari. Tulikuwa tunasubiri kuingia shift ya mchana tukawa tunahuzunika. By the way nilikuwa hata sijui nyerere ndio anaumuhimu gani.

Baada ya hapo sasa ilikuwa tunakusanyika kwa jirani tunajaza sebure kama kibanda umiza kuangalia kwaya na nyimbo za maombolezo yan mtaa mzima tumejazana kwa jiran mmoja.
 
Back
Top Bottom