14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

Sintasahau Nyerere mwili wa Nyerere ukiwasili ukitokea st Thomas London uingereza na maziko kijijini Butiama ndio wakati Bibi yangu nae Anafariki hospital ya KCMC Moshi. Yaaani ilikuwa ni majonzi makubwa nyumbani Moshi.
 
Nilikuwa nursey school pale kilema parish...nakumbuka nilikuwa na miaka 6 ,mida ya mchana tulikuwa tunarudi home kunywa uji ghafla nafika kichumini pale mkyashi nakuta mzee analia nilishangaa sana maana baba yangu alikuwa jemedari sana ila siku hiyo macho yalikuw mekundu mno ,ndo kuniambia kuwa baba wa taifa amefariki mimi hata siku naelewa sana ni kakimbilia chupa ya uji kwanza
 
Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.

Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?


Kumbuka.
Hapo natoka darasani form 5 nimemaliza pindi la adv maths lá mzee makunja.naenda kupata tea.mzee wa complex unzengoni Dom
 
Nilikuwa shuleni darasa LA pili nilikuwa nasikia wanasema Mara bendera nusu mlingoti ila nilikuwa siwaelewi elewi vile
 
Daah pamoja na ujumbe wako murua...kumbe kuna Watoto wengi humu. Mwaka huo niko UDSM second year napambana na Strength of Materials na Thermodymic ile mbaya....
**** primary school Mtwara,tumeshapiga paper ya standard seven tunafanya mazoezi ya mahafali,mara paap kengele ya dharula inagonga muda huo mi nipo juu ya mnazi wa shule naangusha madafu,wahuni wenzangu wapo chini wanayafua hahahaa basi tukakusanyika fasta assembly shule nzima,mwalimu mkuu Mama Mwangata anatangaza kwamba nyerere kafariki,wanafunzi wa madarasa ya chini wanalia kwa sauti,walimu wanawatuliza kwamba hakutakua na vita tulieni,that was 14/10/1999...
 
Binafsi sikua nikimfahamu Wala hata kumsikia Mwalimu mpaka nilivyosikia amekufa....Nikihuzunika kuanzia pale baada ya kuanza kusimuliwa sifa zake....Huo mwaka nilikua darasa la Kwanza Haloli primary Vwawa wilayani mbozi
 
Mi nakumbuka ndo nilikuwa darasa la nne nyakabungo primary iko mwanza na kipindi hicho ndo wazazi wangu walikuwa wametengana,bad memory!!!!!!

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Mi nilikuwa nachuma kahawa kiredio changu cha national nimekining'iniza kwenye tawi na betri zake kama 8 hivi pembeni nimezisokotea kwenye box
Dah, haya maisha ya kuunganisha betrii sitakagi nikumbuke. Zikiisha zinapangwa dirishani zichaji na jua, zikizingua zinapondwapondwa kuzibust. Yale maisha yalikuwa magumu sana
 
Daah pamoja na ujumbe wako murua...kumbe kuna Watoto wengi humu. Mwaka huo niko UDSM second year napambana na Strength of Materials na Thermodymic ile mbaya....
Iam thirty something now,nishazeeka mkuu
 
Back
Top Bottom