14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

inchaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
2,664
Reaction score
5,468
Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.

Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?

Kumbuka.
 
**** primary school Mtwara,tumeshapiga paper ya standard seven tunafanya mazoezi ya mahafali,mara paap kengele ya dharula inagonga muda huo mi nipo juu ya mnazi wa shule naangusha madafu,wahuni wenzangu wapo chini wanayafua hahahaa basi tukakusanyika fasta assembly shule nzima,mwalimu mkuu Mama Mwangata anatangaza kwamba nyerere kafariki,wanafunzi wa madarasa ya chini wanalia kwa sauti,walimu wanawatuliza kwamba hakutakua na vita tulieni,that was 14/10/1999...
 
Nilikuwa darasa la pili kipindi hicho tunaenda shuleni saa nne wakati nakaribia kifika shule nakutana na wanafunzi wanalia wanarudi nyumbani nami nikaunga trela kurudi home hapo ni mwendo kucheza njiani mpaka kufika home hueleweki
 
Daah nilikua darasa la pili pale Shule ya msingi Yombo Dovya, ninachokumbuka zaidi siku hii ni kwenye maombelezo , bibi yangu alilia sana na kipindi hicho home hakukua na tv hivyo alienda nyumba jirani kuangalia maombelezo....
Zamani chakula tulikua tunakula pamoja, nilienda kumsihi twende tukale akasema nitangulie, nilimaliza chakula chote bibi akalala njaa
Mola amrehemu huko aliko
 
Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.

Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?

Kumbuka.
Nilikuwa Darasa la pili Shule ya msingi.

Miaka kadhaa baaadae nikajiunga shule yako Iyunga.

Nashukuru kukuona Schoolmate wangu, ingawa hizo purukushani za chai na Maandazi hatukuzikuta, siye tulikuta purukushani za uji[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119]
 
Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.

Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?

Kumbuka.
99 ulikuwa Iyunga shikamoo bradha
 
Back
Top Bottom