14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

Nilikuwa nakaa Faru Mkuu, tunapigia msuli kule Kakunyu ya Faru Wing namba 4 juu labisa karibu na kwa Mwalimu Kasongo na Mwakanyamale kabla hajawa Headmaster
Ha aha a.., Mkuu Mm nilikuwa Tembo house opposite na Chui, chini ya Jemedari Samwel Mattias Teti aka Mswahili, Mwl wa Bweni alikuwa Zubeir!
 
Nilikuwa nachunga mbuzi kupitia kiredio changu ndio nikapata habari
 
Nilikuwa darasa la sita,enzi hizo ilionekana kama nchi haiwezi songa mbele tena na kulikuwa na story kwamba vita itatokea
 
Naikumbuka sana maana graduation ya four niliishia kutokuwa kumbukumbu. Mwaka 1999 graduation zote ziliahirishwa ili tukamlilie mwanzilishi wa chama kibovu kuliko vyote Africa kwa wakati huu.

Sisi tulifanya. Maana yetu kawaida ilikuwa inakuwa after exams, pia kawaida hamna disco. Ni ibada,kwaya, vyeti na misosi.
 
Nilikuwa Tabora Shule Moja Maarufu Kidato Cha Sita Nakumbuka Nilirudi Home Dar Kwa Muda Maana Shule Hakuna Kilichokuwa Kikiendelea Baada Ya Kutangazwa Siku Kadhaa Za Maombolezo."
Utakuwa Ulisoma MILAMBO HIGH SCHOOL nami pia nilikuwa hapo Form six. Milambo tulifiwa na Mwalimu wetu(Nyerer alifundisha hapo sometime years back) Siku ile zilitafutwa some documents za Nyerere
 
Nilikuwa tumboni mwa mama bize na mishe zangu ila siku nne baadae ndo nikazipata hizo habari.
 
Nilikuwa napenda kula boko boko sana niliposikia tu naka anza kula ugali mwekundu
 
Nilikuwa nasubiria matokeo ya Darasa la saba. Tena nakumbuka matokeo yetu yalichelewa sana kwa ajili ya maombolezo.
 
Nakumbuka nilikua kijijini kwetu moshi nipo shamban nachunga mbuzi
 
Nilikuwa napiga mzigo musoma na msibani niliudhuria.
 
Daaah! Nilikua Drs la 6 nakumbuka tumetoka skul kurud home namkuta bmkubwa analia KINOMA!! ITV nyimbo za komba "taifa lahuzunika" "kwaheri mwalimu" zinapigwa!
Tuliishudiaa kuagana na baba yetu Nyerere afrika na dunia twahuuzunika kwa pamooja tunasemaa Nyerere kwaheriiiix 2
 
Mi nilikuwa nachuma kahawa kiredio changu cha national nimekining'iniza kwenye tawi na betri zake kama 8 hivi pembeni nimezisokotea kwenye box
 
Back
Top Bottom