Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.
Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?
Kumbuka.
[emoji1][emoji1][emoji1]angalia sasa hapa ndio sijataja halafu iviiiii[emoji24][emoji24]Bila shaka hata wazazi walikua bado hata hawajaplan kumpata mtoto mkorinto, usijali kuna watoto wenzio pia humu, you're not alone[emoji3] [emoji3]
Advanced level Galanos, Tanga. Tulikuwa kwenye gari Karandinga la shule tukienda tour Pangani water Falls. Tumeshikilia mabomba gari inachanja rodi, mbele yangu nilikuwa nimembana binti mrembo gari ikiyumba kidogo tunaminyana viuno daaaah, mara ikasikika redioni breaking news.... stimu ikakata pale pale
Hahaaa, nikaushie basii
Samahani mkuu, si unajua utoto tena
Hivi kipindi mile watu hasa wazima nao walikuwa na mawazo finyu sasa kufa kwa nyerere walikuwa wanahusianisha vipi na vita?**** primary school Mtwara,tumeshapiga paper ya standard seven tunafanya mazoezi ya mahafali,mara paap kengele ya dharula inagonga muda huo mi nipo juu ya mnazi wa shule naangusha madafu,wahuni wenzangu wapo chini wanayafua hahahaa basi tukakusanyika fasta assembly shule nzima,mwalimu mkuu Mama Mwangata anatangaza kwamba nyerere kafariki,wanafunzi wa madarasa ya chini wanalia kwa sauti,walimu wanawatuliza kwamba hakutakua na vita tulieni,that was 14/10/1999...
Kumbe mliosoma Galanos zamani mlifurahi sana,sisi wengine tumekuta karandinga limekufa na msocha ndio kapata moto balaaAdvanced level Galanos, Tanga. Tulikuwa kwenye gari Karandinga la shule tukienda tour Pangani water Falls. Tumeshikilia mabomba gari inachanja rodi, mbele yangu nilikuwa nimembana binti mrembo gari ikiyumba kidogo tunaminyana viuno daaaah, mara ikasikika redioni breaking news.... stimu ikakata pale pale
Pole sana mkuu.
Hii ndio ilikua ratiba yangu alafu nilikua kijijini huko kwa bibiNilikuwa bado mdogo. Tulikuwa tunaishi maeneo ya Mwananyamala Maduka matatu. Kiukweli sikuelewa sana just nilifatisha namna wakubwa walivyokuwa wanahuzunika.
Jirani alikuwa na tv so ilikuwa nakaa mbele ya tv kwa siku nzima nikiangalia nyimbo za maombolezo za Marehem Mzee Komba.
Ile week yote toka anakufa mpaka anapokelewa uwanja wa ndege anapitishwa barabarani mpaka kuagwa uwanja wa Taifa nakadhalika yote niliyashuhudia. Msina kufika Butiama nk. Yaani ilikuwa ni kuamka kunywa chai kukaa kwenye tv mpaka saa saba baada ya kula ugali tv mpaka saa 2 usiku then kula ubwabwa, halafu kwenye tv mpaka saa tano alafu kulala. Kesho tena hivyohivyo.
Don't cry babygirlNilikuwa kwenye KQ,flight #....,tukatangaziwa kuwa Baba wa Afrika, Mwl J.K.Nyerere ametutoka huko St. Thomas Hospital. I cried a bit then i thanked my God for him.