14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

Nilikuwa nasimamia usafi kwenye nyumba niliyokuwa nimeuziwa kama mtumishi tayari.kwa kuhamia eneo fulani hivi la Tz yetu
 
Nilikuwa Tabora Boys Special School! Ilikuwa huzuni kubwa!
Endelea kupumzika kwa Amani Schoolmate!
 
Majira ya saa nne asubuhi au niseme saa tano kasoro hivi nikiwa katika viunga vya mabweni ya Shule ya Sekondari Iyunga baada ya purukushani za kupata chai kwa maandazi ya mafuta ya mawese, taarifa ya kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwa dhahiri.

Je wewe ulikuwa wapi ukifanya nini?


Kumbuka.
Kumbe tulikuwa wote mkuu pale Iyunga wakati Anko Ben akitangaza habari hyo by then ITV ndio ilikuwa pekee super bland na inaendelea kuwa
 
Mimi nilikua bwa mdogo tena tumehamia Nyumba yetu baada ya kutoka nyumba za Kupanga.

Nakumbuka tulikaa chini ya mti mzee tunaskiliza Radio.
 
Nikiwa Shuleni Moshi Vijijni ilikuwa bad news baada ya kusikia radio rtd Ikiimba wimbo wa taifa ghafla Sauti ya Benjamin Mkapa ikasikika
Ikitangaza msiba wa Mwalimu Nyerere.
Wanafunzi tukatangaziwa kurudi nyumbani kwa huzuni kubwa.
 
Nilikuwa bado mdogo. Tulikuwa tunaishi maeneo ya Mwananyamala Maduka matatu. Kiukweli sikuelewa sana just nilifatisha namna wakubwa walivyokuwa wanahuzunika.
Jirani alikuwa na tv so ilikuwa nakaa mbele ya tv kwa siku nzima nikiangalia nyimbo za maombolezo za Marehem Mzee Komba.
Ile week yote toka anakufa mpaka anapokelewa uwanja wa ndege anapitishwa barabarani mpaka kuagwa uwanja wa Taifa nakadhalika yote niliyashuhudia. Msina kufika Butiama nk. Yaani ilikuwa ni kuamka kunywa chai kukaa kwenye tv mpaka saa saba baada ya kula ugali tv mpaka saa 2 usiku then kula ubwabwa, halafu kwenye tv mpaka saa tano alafu kulala. Kesho tena hivyohivyo.
 
Nilikua nauza duka manzese kwa mfuga m'mbwa,
Tukio nalokumbuka zaidi siku maiti yake imeletwa dar inapitishwa mtaani nilifunga duka nkaenda kushuhudia tukio, kurudi dukani km saa 10 jioni hivi ili nkafungue nkapata taarifa ya kifo cha boss wangu, ndio ilikua mwisho wa duka kufunguliwa hadi leo.
 
Back
Top Bottom