Waigizaji wa vichekesho maarufu kama, Kicheche na Clam wamekamatwa kwa kosa la kukiuka Sheria ya Bodi ya Filamu ikiwemo kurusha maudhui pasipo kusajiliwa.
Kwa mujibu wa bodi hiyo, wasanii hao wameitwa mara kadhaa kupeleka kazi zao ili kuhakikiwa na kupewa vibali vya kufanya shughuli za uigizaji...
Zanzibar: Wakamatwa wakiendesha mtandao wa kuingilia watoto wa kiume, kurekodi na kufanya udalali.
"Kuhusu ule mtandao nimejua kupitia walewale ambao wamo kwenye mtandao na kuanza kuwakamata watuhumiwa. Simu zao ndio zikawa zinatuonesha nini kipo na wao wenyewe wakawa wanatueleza nani dalali...
Jeshi la Polisi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 26 na kufikishwa mahakamani Oktoba 26, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwepo; unyang'anyi wa kutumia nguvu na shambulio la kudhuru mili dhidi...
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na oparesheni, misako na doria zenye tija kuhakikisha usalama wa raia na mali zao. Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kupitia misako na doria limepata mafanikio mbalimbali ikiwemo kukamata watuhumiwa wa kughushi na utapeli, kupatikana na silaha bila...
Kurugenzi ya Mapato ya Ujasusi nchini India (DRI) imewakamata Raia wawili kutokea nchini Tanzania kwa madai ya kuhusika na usafirishaji wa kilo 1.5 ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine yenye thamani ya kati ya milioni 80 hadi 100 ya India (Tsh Bil 2.4 mpaka Bil 3) kwa kuzificha ndani ya miili...
Polisi Jumatano waliwakamata Wayahudi watano wa Orthodox kwa tuhuma za kuwatemea mate waumini wa Kikristo katika Jiji la Kale la Jerusalem, huku kukiwa na ongezeko la matukio yanayowalenga makasisi na mahujaji katika mji mkuu.
Wakati huo huo, Waziri wa Usalama wa Kitaifa Itamar Ben Gvir...
Wizara ya Mambo ya Ndani imewataja waliokamatwa ni Mike Mikombe, Mkuu wa Kikosi cha Walinzi na Donat Bawili, Kiongozi wa Jeshi katika mji wa Goma, wote wawili wanadaiwa kuagiza Wanajeshi kuwaua Waandamanaji.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Wizara, Vikosi vya Usalama viliingilia maandamano ya Waumini wa...
Siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutaja ubadhilifu wa fedha mkoani Mbeya, watu 40 wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma za kuhusika kwenye wizi huo wa Sh450 milioni wa fedha za umma.
Akizungumza leo Jumatatu Agosti 28, 2023 Mkuu wa Wilaya ya...
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewakamata watu watatu kwa tuhuma za kujeruhi na kupora watu vitu mbalimbali katika maeneo ya daraja la selandar eneo la mikoko.
Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro, amesema...
Habari ndugu wana JF,
Jamani hii nchi kamatakamata haijaisha. Nina kaka yangu ambae ni wa kwanza kuzaliwa, miaka 31 amekamatwa usiku wa manane yapata wiki mbili sasa na watu tunaowahisi ni Usalama wa Taifa.
Walienda wakavunja komeo la mlango wake wakaingia ndani. Walikuwa na bunduki...
Jeshi la polisi mkoani manyara linawashikilia watu wawili, mohamed said na diana lozi wakazi wa dsm kwa tuhuma za kukutwa na fedha taslimu za kitanzania wakihiswa ni za wizi na simu za mkononi 27 , katika nyumba ya kulala wageni mjini babati. Mwenye taarifa kamili tunaomba msaada.
Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa watatu wa mauaji ya aliyekuwa mfanyakazi wa mgodi wa GGM Geita Milembe Selemani yaliyotokea Aprili 26,2023 katika mtaa wa Mwatulole mkoani Geita pamoja na watu watatu waliofanya mauji ya aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kerende Dk. Isack...
Hii ni kama utapeli wa Jatu au Mr Kuku ila imetokea nchi jirani ya Zambia. Wakurugenzi watatu wa Kamono Farms wanashikiliwa na vyombo vya dola kwa makosa ya kujipatia pesa kilaghai kutoka kwa wananchi kwa kuwashawishi wawekeze fedha zao kwenye kilimo kwa ahdi ya kupata faida kubwa sana kitu...
Jeshi la polisi mkoa wa limewakamata watoto 15 ambao wanaojihusisha na makundi ya uharifu huku wakiwa na umri Mdogo ambayo yamekuwa yakijukiana kwa majina ya Damu chafu na Manyigu na kuwa tishio kwa usalama wa Wananchi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Ali Hamad Makame amesema watoto hao...
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako na doria za nguvu na zenye tija katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya na kupata mafanikio makubwa ikiwemo kukamata watuhumiwa 14 kati yao wanaume ni 11 na wanawake 03 wakiwemo watuhumiwa wa kusafirisha vipodozi vyenye viambata sumu na...
WATU sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida wakihusishwa na mauaji ya watu, ufukuaji wa makaburi na kuchukua viungo, baadhi ya vitu vya maiti katika maeneo tofauti wilayani Manyoni.
Imeelezwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa, leo Machi 28, 2023 kuwa...
Wanawake wawili wa Kijiji cha Kimana wilayani Kiteto Mkoani Manyara, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kiteto kwa kukutwa na nyara za Serikali, ambazo ni Swala na mtoto wa mnyama aina ya Digidigi ambaye yuko hai.
Wanawake hao ni Veronica Paulo (24) na Witnes Paulo (20) ambapo Machi 20.2023...
Takriban wanahabari 14 na wafanyakazi wa vyombo vya habari wamezuiliwa, kunyanyaswa, au kushambuliwa wakati wakiripoti uchaguzi mkuu wa Nigeria, akiwemo mmiliki wa tovuti binafsi ya habari ya WikkiTimes Haruna Mohammed Salisu, ambaye bado anashikiliwa na polisi bila kufunguliwa mashtaka...
Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na TAWA limewakamata watu wawili waliotambulika kwa majina ya Richard Paulo (Miaka 23) na Masiaya Lais (Miaka 19) katika kijiji cha Minjingu katika hifadhi ya Jamii ya Burunge wilayani Babati wakiwa nyara za serikali ambazo ni nyama ya Twiga...
Wanafunzi 12 wa shule ya Sekondari Handeni iliyopo wilayani Handeni mkoani Tanga wamekamatwa vichakani wakivuta bangi na kucheza kamari muda wa masomo hali iliyopelekea uongozi wa shule hiyo kuwasimamisha masomo kwa muda wa siku 14.
Wanafunzi hao wamekamatwa kufuatia oparesheni maalumu ya...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.