Zanzibar: Wakamatwa wakiendesha mtandao wa kuingilia watoto wa kiume, kurekodi na kufanya udalali

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Zanzibar: Wakamatwa wakiendesha mtandao wa kuingilia watoto wa kiume, kurekodi na kufanya udalali.

"Kuhusu ule mtandao nimejua kupitia walewale ambao wamo kwenye mtandao na kuanza kuwakamata watuhumiwa. Simu zao ndio zikawa zinatuonesha nini kipo na wao wenyewe wakawa wanatueleza nani dalali, nani mnunuzi, tunauza kwa kima gani, yaani watu wanazunguka wanachukua watoto wanawaharibu na kuwarekodi (lengo ni) kuzituma sehemu husika ili wao wapate pesa zao ambazo wameahidiwa kulipwa.

"Watoto wanafichwa mbali na kama mtu (au) hajatoka kijana humu ndani ya nyumba kuja kukupa taarifa basi huwezi kujua mtoto yuko wapi (hata) miaka sita. Ila madalali wengi wapo Forodhani, kwasababu haw ani Watoto wadogo na Watoto wengi watukutu wanaokimbia nyumbani wanakimbilia kucheza Forodhani” - Mpambanaji wa udhalilishaji

Wadau hawa wanaopambana na udhalilishaji walipata taarifa ya kijana mmoja mwenye umri wa miaka 18 kupotea kwa wiki 3, ndipo walipogundua alikuwa amewekwa kinyumba na dalali ambaye anamuuza kwa wanaume wengine.

Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusika katika matukio haya.

“Hao watu niliwajulia Kisauni, walinichukua Forodhani. Walinipa kuna soda inaitwa ‘energy’, siku nyingine ndio wamekuja kunionesha video, washanifanyia mara ya pili. Anaanza kukufanya yeye halafu ndio anamuuzia mwenzake.

“Akiuzwa kama anataka (anasema) nina Tsh. 60,000/-, (dalali) anakataa anamwambia ongeza dau, jamaa anasema mimi nina Tsh. 100,000/-. Wanazidiana Dau kila mtu na pesa yake, wapo wengi”
Mhanga 1

“Nilikerana na mama kidogo, alinigombeza nikaamua kuondoka nyumbani. Nilivyoondoka nyumbani nikaenda zangu Forodhani. Siku ya kwanza tulipokwenda kwake alinipa chakula, akaniambia choo kile pale kaoge uje ulale, hajanifanyia kitu siku ya kwanza.

“Akaja na soda aina ya ‘energy’, ile siku alinifanyia, nilipoamka nilihisi maumivu makali tu. Ile siku alinifanyia akanichukua na video. Wao wenyewe binafsi walikuwa wananipa Tsh. 3,000/- au 5,000/-“ – Mhanga 2

Mwaka 2022 Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar ilionesha kuwa, katika kipindi cha Januari hadi Disemba jumla ya vitendo 1,361 vya udhalilishaji viliripotiwa. Hukum waka 2023 kuanzia Januari hadi Septemba jumla ya vitendo vya 1,421 vya udhalilishaji vimeripotiwa.

“Mwanangu alipotea wiki tatu na nusu nikawa namtafuta, nikawa napiga simu mule mote anapopajua, sehemu anazokwenda, juzi Jumamosi ndio nikapigiwa simu kwentu wakaniambia wamemkamata. Kumuhoji ndio akasema alipokuwa na alivyofanyiwa. Kujisikia, najisikia vibaya sana na najisikia uchungu mkubwa sana, nilikuwa namtegemea kwasababu najua hii ni zawadi amenipa Mwenyezi Mungu, leo hii zawadi yangu kwanini inaharibiwa? – Mama wa mhanga
 
Back
Top Bottom