Watanzania wawili wakamatwa India kwa usafirishaji wa kilo 1.5 ya dawa za kulevya

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Screenshot 2023-10-20 083100.png

Kurugenzi ya Mapato ya Ujasusi nchini India (DRI) imewakamata Raia wawili kutokea nchini Tanzania kwa madai ya kuhusika na usafirishaji wa kilo 1.5 ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine yenye thamani ya kati ya milioni 80 hadi 100 ya India (Tsh Bil 2.4 mpaka Bil 3) kwa kuzificha ndani ya miili yao ikiwa ni tukio la saba ndani ya kipindi cha mwezi mmoja nchini humo.

Taarifa zinasema mwanzoni mwa mwezi October chombo hicho cha ujasusi DRI kilimnasa Mussa Mgonja (62) na Rashid Zamiru (23) ambao waliwasili kutoka Addis Ababa nchini Ethiopia kuelekea jijini Mumbai nchini India.

Ingawa utafutaji wao wa binafsi haukuzaa matunda, kwa mujibu wa ripoti walipopelekwa katika Hospitali ya JJ, Musa alionekana na vidonge 79 ndani ya mwili wake na Rashid akiwa na vidonge 33 kisha uchunguzi zaidi ulibaini kuwa wawili hao walikuwa wabebaji mahiri wa dawa za kulevya ambapo Mussa alisema hiyo ilikuwa ni safari yake ya pili na alikuwa amesafirisha vidonge kufikia 125 vya madawa huko kuelekea jijini Delhi, nchini India.

Ayo updates
 
Billion 2 mate yananitoka

Sema haya maisha sometimes ni kujilipua tu umafia umafia ukitoboa hapo unaachana kbs na hiyo biashara unanunua zako benz unaenda kujenga kajengo kadogo lushoto..unaanzisha m pesa,kamin supermarket na ka daladala kamoja na ka grocery kamoja chenye kitimoto na duka la nguo..unatulia kimyaaaaa
 
Unakuta mzigo si wako, umeajiriwa kama ajira zingine tu na malipo labda ni 10M, ndio maana alibeba mara ya kwanza akabeba tena.
 
Fanya tafiti hata wanaokamatwa hapa bongo ambao tunaowafahamu wanayofanya biashara hizo za ngada , fuatilia Imani zao, au wale wazamiaji wa Afrika ya kusini wanao uza ngada huko wapeleleze ukikuta 100 basi 90 ni WA kwenu
Acha kubatiza watu dini jina sio kigezo cha kujua dini ya mtu kwa mfano mimi ni mkristo ila jina jina langu sio la kikuristo kabisa
 
View attachment 2786999

Kurugenzi ya Mapato ya Ujasusi nchini India (DRI) imewakamata Raia wawili kutokea nchini Tanzania kwa madai ya kuhusika na usafirishaji wa kilo 1.5 ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine yenye thamani ya kati ya milioni 80 hadi 100 ya India (Tsh Bil 2.4 mpaka Bil 3) kwa kuzificha ndani ya miili yao ikiwa ni tukio la saba ndani ya kipindi cha mwezi mmoja nchini humo.

Taarifa zinasema mwanzoni mwa mwezi October chombo hicho cha ujasusi DRI kilimnasa Mussa Mgonja (62) na Rashid Zamiru (23) ambao waliwasili kutoka Addis Ababa nchini Ethiopia kuelekea jijini Mumbai nchini India.

Ingawa utafutaji wao wa binafsi haukuzaa matunda, kwa mujibu wa ripoti walipopelekwa katika Hospitali ya JJ, Musa alionekana na vidonge 79 ndani ya mwili wake na Rashid akiwa na vidonge 33 kisha uchunguzi zaidi ulibaini kuwa wawili hao walikuwa wabebaji mahiri wa dawa za kulevya ambapo Mussa alisema hiyo ilikuwa ni safari yake ya pili na alikuwa amesafirisha vidonge kufikia 125 vya madawa huko kuelekea jijini Delhi, nchini India.

Ayo updates
Kama walitokea Tanzania, ichunguzwe ndege waliyoondoka nayo ilikuwa wakkati gani, askari, usalama wa taifa, watu wa forodha waliokuwepo siku hiyo wote ni wahusika. Waliowasindikiza pia waytaonekana kwenye cctv, wote wamo hao.
 
Back
Top Bottom