Watatu wakamatwa kwa tuhuma za kujeruhi na kupora watu vitu mbalimbali katika maeneo ya daraja la Selandar eneo la mikoko

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewakamata watu watatu kwa tuhuma za kujeruhi na kupora watu vitu mbalimbali katika maeneo ya daraja la selandar eneo la mikoko.

Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia ufuatiliaji mkubwa wa wahalifu wanao jihusisha na matukio ya namna hiyo.

Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linaendelea na ufuatiliaji wa wahalifu wanaopora kwa kutumia pikipiki katika maeneo mbalimbali ya jiji, na jeshi la polisi litawakamata na baadae kuwafikisha katika vyombo vingine vya kisheria kwa hatua zaidi.

1691801601050.jpeg

1691801620230.jpeg

1691801639003.jpeg
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewakamata watu watatu kwa tuhuma za kujeruhi na kupora watu vitu mbalimbali katika maeneo ya daraja la selandar eneo la mikoko...
Mwambieni RPC wenu Muliro kuwa Uwizi wa Simu kwa kutumia Pikipiki umeshika Kasi sana kuanzia Kituo cha Basi cha Mwenge hadi Daraja la Mlalakuwa mita chache tu kutoka Ukumbi wa 361 Mlalakuwa Makongo.
 
Mwambieni RPC wenu Muliro kuwa Uwizi wa Simu kwa kutumia Pikipiki umeshika Kasi sana kuanzia Kituo cha Basi cha Mwenge hadi Daraja la Mlalakuwa mita chache tu kutoka Ukumbi wa 361 Mlalakuwa Makongo.
Asante kwa taarifa mkuu
 
IMG-20230811-WA0442.jpg
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu watatu kwa tuhuma za kujeruhi na kupora watu vitu mbalimbali katika maeneo ya daraja la salenda eneo la mikoko.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muliro J. Muliro amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia ufuatiliaji mkubwa wa wahalifu wanao jihusisha na matukio ya namna hiyo.

IMG-20230811-WA0441.jpg

IMG-20230811-WA0440.jpg
Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na ufuatiliaji wa wahalifu wanaopora kwa kutumia pikipiki katika maeneo mbalimbali ya Jiji, na Jeshi la Polisi litawakamata na baadae kuwafikisha katika vyombo vingine vya kisheria kwa hatua zaidi.
 
Back
Top Bottom