Mbeya: Wanaofanya utapeli kwa kutumia jina la Mo Dewji wakamatwa, wakutwa na Line za Vodacom (10), Tigo (2) na Airtel (3)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na oparesheni, misako na doria zenye tija kuhakikisha usalama wa raia na mali zao. Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kupitia misako na doria limepata mafanikio mbalimbali ikiwemo kukamata watuhumiwa wa kughushi na utapeli, kupatikana na silaha bila kibali na kupatikana na mali ya wizi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili wote wakazi wa Chapakazi katika Mji Mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya ambao ni SARAEL GESHON [19] na CHRISTIANI ERASTO [21] kwa tuhuma za kughushi nyaraka mbalimbali na kutapeli watu kwa kutumia jina la “Mo Dewji Foundation”.

Watuhumiwa walikamatwa Oktoba 22, 2023 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Altas iliyopo Mji Mdogo wa Mbalizi katika misako inayoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali.

Aidha, watuhumiwa walikutwa wakiwa na simu za mkononi smart phone 6, simu ndogo 3, line za simu za mtandao wa Vodacom 10, Tigo 2 na Airtel 3 zenye usajili wa majina tofauti wakizitumia kuibia watu mbalimbali kwa kutoa machapisho ya uongo kwamba wanatoa mikopo kupitia “Mo Dewji Foundation”.

Watuhumiwa wamekuwa wakighushi kwa njia ya kompyuta kitambulisho cha NIDA, Tin ya TRA, leseni ya biashara na usajili wa Brela kwa jina la mo dewji foundation na kisha kutapeli watu wakidai kutoa mikopo kwa riba nafuu. Watuhumiwa wamekiri kutekeleza matukio ya utapeli katika maeneo mbalimbali na kujipatia kipato isivyo halali.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mkazi wa Nsalala Mkoani Mbeya aitwaye JOSHUA WILLIAM [19] kwa tuhuma ya kupatikana na mali ya wizi Bajaji MC 548 TVS Kings rangi ya kijani.

Mtuhumiwa alikamatwa Oktoba 22, 2023 huko eneo la Stendi ya mabasi ya Tunduma iliyopo Mji Mdogo wa Mbalizi akiwa katika harakati za kuisafirisha Bajaji hiyo kwenda Mji Mdogo wa Tunduma Mkoa wa Songwe.

Mtuhumiwa amekiri kuhusika katika tukio la wizi wa Bajaji lililotokea Oktoba 21, 2023 majira ya saa 3:00 usiku katika Kijiji cha Shigamba - Mbalizi ambapo mhanga EMANUEL OBIMSONGE [38] Mkazi wa Shigamba aliibiwa Bajaji hiyo yenye thamani ya Tshs 9,100,000/=.
 
Polisi ikamate pia wanaotapeliwa kizembe.

Wewe unaona tangazo eti tunatoa mkopo kwa riba nafuu, Halafu unaambiwa utume riba ndio pesa iingizwe na wewe unatuma?
 
Back
Top Bottom