uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Q

    JamiiForums Tanzania James Mbatia: Kwa sasa Rais Samia hawazi matatizo ya wananchi anawaza uchaguzi wa 2025 tu

    “@ChademaTz , @ACTwazalendo , #CUF na sisi @nccrmageuzihq hebu tuondoe viburi vyetu tukae pamoja tuzungumze kuhusu nchi yetu, kwann tukose furaha kwenye nchi yetu? Tuoneshe mshikamano wetu katika kupigania haki katika nchi yetu”. - M/kiti Taifa Ndugu #JamesMbatia #KongamanoLaCUF “Samia Suluhu...
  2. K

    JamiiForums Tanzania CCM, picha za umwagaji damu Uchaguzi 2020 zinazosambazwa mitandaoni na wanachama wenu kupongeza waliomwaga damu, si dalili njema

    Tuna vyombo vya dola na chama dola, wenzenu kuanzia jana wanatoa makovu yaliyotokana na uchaguzi wa mwaka jana. Zipo tuhuma za kupigwa Risasi kukatwakatwa na kulazimishwa kwa watu kurejea CCM na walipokataa walimwagwa damu. Wakati Taarifa hizi zikisambaa kwa kasi zikiwa na majina na maelezo...
  3. Poppy Hatonn

    JamiiForums Tanzania Najikumbusha kuhusu Uchaguzi was 2015

    It was the dream that . I had. Niliota sayari zinazunguka jua na miezi inazunguka sayari,like watching inside a clock. Halafu all those celestial bodies started rotating backwards. After rotating backwards for some time,again they started going forward . Ndipo hapo kati ya watoto watatu wa...
  4. jitombashisho

    JamiiForums Tanzania Mwanza, Shinyanga na Musoma: CCM ikishinda uchaguzi ujao naahidi kujiondoa JF

    Kwa upepo unavyovuma kanda ya ziwa itakuwa ni vigumu mno kwa CCM kushinda Majimbo ya uchaguzi ya Ubunge na hata kura kwa Rais zitapungua mno 2025! Nawashauri wana Chadema na hata vyama vingine vya upinzani wekezi nguvu zenu Kanda ya ziwa hakika hamtojuta 2025. Ukweli ni kwamba Samia anachukiwa...
  5. R

    JamiiForums Tanzania CHADEMA ni muhimu kujipanga kwa uchaguzi

    Lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola. CHADEMA kipindi hichi inapitia wakati mgumu kwa mwenyekiti wake kuwa kizuizini. Jambo hili ni kubwa na mko wamoja katika kupigania haki ya mwenyekiti wenu, jambo hili ni kubwa ila nashauri lisiwatoe kwenye reli katika maandalizi ya...
  6. B

    JamiiForums Tanzania Maandalizi ya uchaguzi 2025 yazingatie mikakati ya 2020 maana hakuna miujiza ya sisi wana CCM kupenya sanduku la kura

    Dalili ya mvua ni Mawingu, na ukweli usiposemwa adharani utasema sirini. Hali ni ngumu, miyoyo ya watu imekunjamana, wanacheka na wewe ukiondoka wanakung'ong'a. Inshort huna watu nyuma yako na hakutatokea miujiza ukawa na watu nyuma yako Hadi pale utakaruhusu maridhiano ndani ya chama. Ni...
  7. peno hasegawa

    JamiiForums Tanzania Ushauri: ~ Makatibu wa CCM wa wilaya na Mikoa wabadilishiwe vituo vya kazi kabla ya uchaguzi wa chama 2022

    Kuna makatibu wa CCM wilaya na Mikoa wasipobadilishiwa vituo vya kazi. Mapema na ksbla ya ichaguzi mkuu wavchama CCM 2022 watachagua mamluki na watu wasio na sifa. Pili wamekuwa miungu watu kwa chama na kwa wananchi. Ninashauri waondolewe mapema na kuweka wengine wapya na waadilifu.
  8. Wakusoma 12

    JamiiForums Tanzania Wakurugenzi wote wa halimashauri na majiji waliohujumu uchaguzi wetu 2020 washughurikiwe.

    Napendekeza sheria ichukuwe mkondo wake na wala asiwepo wa kupona. Kila mmoja wetu anafahamu what happened October 2020 ambapo watumishi Hawa wa umma waliharibu mfumo wa uongozi na misingi ya demokrasia bila uoga wowote. Kwa kuwa makosa waliyotenda ni jinai basi hakuna aliye salama wote...
  9. K

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi Mdogo Ushetu. Waliopiga kura 106,000+. Ambao hawakupiga kura ni wangapi?

    Lipo tatizo la tume ya uchaguzi kuacha kuendesha uchaguzi na kubaki na taarifa za copy and paste kwa kiwango Cha data wanachoamua wao. Huko Ushetu CCM na ACT pekee wamepigiwa kura zaidi ya laki moja na elfu sita. Kwa tuliokuwa tunafuatilia kampeni na baadaye siku ya kupiga kura lazima tujiulize...
  10. Meneja Wa Makampuni

    JamiiForums Tanzania Kama kweli Magufuli aliletwa na Mungu basi uchaguzi wa 2025 utakua ni patashika nguo kuchanika

    Hicho ndicho kilichonijia kichwani leo nikiwa natafakari mwenendo wa siasa za Tanzania kwa sasa. Maswali ni je nani atakubali kusimama na ni nani atakubali mwenzake kusimama. Itakua nipatashika nguo kuchanika ndani ya vyama na nje ya vyama.
  11. technically

    JamiiForums Tanzania CHADEMA acheni kujiingiza kwenye siasa za chuki kuelekea uchaguzi 2025

    Unamsema vipi mtu ambaye hawezi kujitetea Kama Hayati Magufuli, Mkapa au Nyerere? Mimi binafsi Hawa watu siwadai Kama Mungu kashafanya hukumu yake waachwe wapumzike!! Natoa angalizo tu kwa chadema kuelekea uchaguzi 2025 hasa Tundu Lissu na Mbowe wajitaidi kuepuka Mambo yafuatayo. 1: Acheni...
  12. M

    JamiiForums Tanzania Katambi avunja ngome ya Upinzani Ushetu amwombea kura mgombea wa CCM Comred Emmanuel Peter Cherehani

    Katambi avunja gome ya Upinzani Ushetu " Tunahamia CCM hatuwezi kubaki kwenye chama kinachosusia kila Uchaguzi " Je Nani ni Nani leo kati ya ACT-Wazalendo na CCM-Tanzania "Tutampa Rais Samia ushindi mnono kama shukrani yetu kwake -wapigakura " Katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Hayati Elias...
  13. J

    JamiiForums Tanzania SHAKA: Tuko tayari kupokea matokeo yoyote ya uchaguzi CCM

    Chama cha Mapinduzi chini uongozi wa Rais Samia kitaendelea kusimamia demokrasia ya kweli na kwa vitendo, tuko tayari kupokea matokeo yoyote ya uchaguzi katika jimbo la Ushetu Kahama, Konde Pemba na kata 3 tunazofanya uchaguzi wa marudio 10 Oktoba 2021. Shaka Hamdu Shaka Katibu wa Halmashauri...
  14. Fundi Madirisha

    JamiiForums Tanzania Siioni imani ya CCM kushinda uchaguzi mkuu 2025

    Kila nikitazama maisha yanavyozidi kua magumu, watu wanavyolia na ugumu wa maisha na hali inazidi kua mbaya kuliko siku za nyuma, siioni imani ya CCM kushinda uchaguzi 2025. Ugumu wa maisha hua ni sababu tosha kukiondoshea mapema chama ukombozi. Mtapiga watu, wagombea kupitia vyama vya...
  15. P

    JamiiForums Tanzania Nafasi ya muamuzi katika mashindano!

    "Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu" Mithali 18:18 Mara nyingi kumekuwa na kawaida kwa vyama vikuu vya pinzani na Chama kinachotawala kuvutana na kutokukubaliana kabla au baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa, iwe Tanzania bara au Tanzania visiwani. Mara zote hizi lawama...
  16. B

    JamiiForums Tanzania Utesaji wa Dola - Agenda kubwa Uchaguzi ujao

    Habari hii iwafikie wote wanaokodolea macho nafasi za uongozi. Ifahamike kuwa bila tume huru hakuna uchaguzi. Hatutaangalia mgombea ni mwanamke au mwanaume. Haki zetu za binadamu hazitakuwa na mbadala. Kama ni mtarajiwa atuambie atafanya nini kuondoa kadhia kama hizi: Kama alikuwamo...
  17. M

    JamiiForums Tanzania Ujerumani: Mbunge mwenye asili ya Senegal ameshinda jimbo la uchaguzi

    Karamba Diaby alishinda jimbo la Halle (Saale) kwenye uchaguzi mkuu nchini Ujerumani tarehe 26 Septemba. Dk Karamba alizaliwa Senegal akafika Ujerumani akiwa mwanafunzi mnamo mwaka 1986. Baada ya kuhitimu shahada ya uzamivu ya kemia alianza kujihusisha na siasa akajiunga na Chama cha...
  18. Nyankurungu2020

    JamiiForums Tanzania Hivi mmesahau kuwa genge lenu lilichafua CCM na kiongozi aliyefariki akainusuru CCM uchaguzi wa mwaka 2015

    Mliichafua Ccm kwa kashfa nzito amabazo mlihusishwa kuzitenda. Mlihusishwa na kashfa za kila namna kuanzia Escrow, Lugumi Kagoda na kila aina ya ufisadi uliotokea. Mwaka 2015 Ccm ilichafuka kwa sababu ya uchafu na ufisadi mliouzoea. Ndipo ikaonekana kiongozi aliyefariki angalau asimame ili...
  19. OMOYOGWANE

    JamiiForums Tanzania Lowassa angeshinda uchaguzi 2015 sera yake ya ELIMU, ELIMU, ELIMU ingeimarisha vipi uchumi wa Mtanzania mmoja mmoja?

    Tangu uchaguzi wa mwaka 2015 upite huu ni mwaka wa 6 sasa, wagombea wa nafasi ya urais walikuwa ni JP. Magufuli na E.Lowassa, Swali langu je kama ingetokea Lowasa akashinda uchaguzi sera yake kuu ilikuwa ni kutoa elimu bure kwa wote mpaka chuo kikuu (ELIMU, ELIMU, ELIMU), kwa elimu yetu hii...
  20. F

    JamiiForums Tanzania Rais hapatikani kwa tukio la uchaguzi, anaandaliwa tangu shuleni

    Matukio mengi makubwa yaliyowahitukia, ama katika maisha ya mtu wa kawaida au katika maisha ya ziada ya mtu mwenye historia, yametukia katika muda usio muafaka wa maisha yake. Kwa mfano, kanuni ya jumla ya sheria ya mvutano (Universal Law of Gravitation) ilizaliwa kwenye akili ya Isaac Newton...
Back
Top Bottom