Rais Samia ameona kasoro pekee Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kuwa ni ujazwaji uliokosewa wa wagombea wa upinzani?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,479
30,144
Wakati akipokea ripoti ya Tume ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2020, hapo tarehe 21 mwezi huu, Ikulu jijini Dar, nilimsikia Rais Samia Suluhu Hassan, akielezea dosari alizoziita ndogo, zilizofanywa na Tume ya uchaguzi Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kuwa ni "kuwa-disqualify" wagombea wa vyama vya upinzani kwa kosa la kutojaza kwa usahihi, form za uchaguzi.

Nimuulize Rais Samia Suluhu Hassan, hivi hajaziona kasoro nyingine kubwa Sana, chungu mzima, zinazolalamikiwa na wapinzani, ila ameiona hiyo kasoro moja pekee??

Wapinzani wamekuwa wakilalamika Katika kipindi kirefu Sana kuwa Tume ya uchaguzi siyo huru na imekuwa ikikipendelea waziwazi chama kilichoko madarakani cha CCM wakati wa uchaguzi

Hivi Mwenyekiti huyo wa Taifa wa CCM, Samia Suluhu Hassan hajasikia malalamiko kuhusu mawakala wa vyama vya upinzani kunyimwa viapo, wakati wenzao wa CCM, wakipewa "kiulaini" viapo hivyo??

Hivi hajasikia kilio cha muda mrefu kuwa mawakala hao wa vyama vya upinzani wamekuwa wakiondolewa kwa nguvu kwenye vituo vyao, wakati wa upigaji kura, kwa msaada wa Polisi??

Hivi hajasikia malalamiko ya wapinzani kuwa mawakala wa vyama vya upinzani wamekuwa wakinyimwa form za matokeo ya uchaguzi, wakati wa chama cha CCM wakipewa??

Hivi hajasikia malalamiko ya vyama vya upinzani ya kuwaweka wakurugenxi wa wilaya, ambao ni makada wa CCM, kuwa ndiyo wasimamizi wskuu wa uchaguzi huo??

Hizo ndiyo sababu Kuu, ambazo zinawafanya vyama vya upinzani vipiganie kufa na kupona Tume ya uchaguzi iliyo huru, kusimamia uchaguzi wa nchi hii, pamoja na kupata Katiba mpya ya nchi hii, kwani Katiba ya hivi sasa ilitungwa kwa ajili ya mfumo wa chama kimoja, ambacho ni cha CCM
 
Dah..... Fitina ni kubwa.... Ila maisha ya kunyooshewa vidole ni magumu sana....
 
Dah..... Fitina ni kubwa.... Ila maisha ya kunyooshewa vidole ni magumu sana....
Ni dhahiri kuwa malalamiko ya vyama vya upinzani, kuitaka serikali ipate Katiba mpya ya nchi hivi sasa si ya kupuuzwa hata kidogo.

Hata kama serikali hiyo itafanya "delaying tactics" kwa kumfungulia mashitaka ya kubambika ya ugaidi, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe
 
Imenenwa Katika Biblia, kitabu cha Mithali sura ya 14:34 kuwa "Haki huinua Taifa na dhambi ni aibu ya watu wote"

Hivi nchi hii watawala wake wanapoona kuwa CCM ndiyo yenye hati miliki ya kuitawala milele nchi hii, pamoja na kuwatesa wananchi wa nchi hii, hawaoni kuwa hiyo ni laana kubwa na dhambi itakayowatafuna vizazi na vizazi vyao??
 
Kasoro ndogo na kubwa zote zipo kwa manufaa yao, sioni sababu ya kushughulikia kasoro ndogo wakati hata kubwa zilizobaki zitawabeba wao au hata kama ingekuwa vice versa, hakuna Tume ya maana ya uchaguzi Tanzania, hii iliyopo ni tawi la CCM.
 
Hizo ndiyo sababu Kuu, ambazo zinawafanya vyama vya upinzani vipiganie kufa na kupona Tume ya uchaguzi iliyo huru, kusimamia uchaguzi wa nchi hii, pamoja na kupata Katiba mpya ya nchi hii, kwani Katiba ya hivi sasa ilitungwa kwa ajili ya mfumo wa chama kimoja, ambacho ni cha CCM
Hawa watu hata aibu hawana tena.

Maana yake ni dharau kwa waTanzania, kuwaona kama hawana akili za kujuwa uchafu wao.

Hayo aliyoyasema yeye ya kutojaza fomu kwa usahihi ndiyo yanayostahili kabisa kuwaengua wanaozijaza fomu hizo kwa makosa, kwa sababu huo ni uzembe wa hao watu na chama chao kutosimamia ipasavyo kuhakikisha kwamba fomu zinajazwa kwa usahihi, bila ya makosa.

Kwa yeye kuona kwamba hilo sio jambo muhimu maana yake ni kwamba yeye mwenyewe hana tabia za kutovumilia makosa yaliyo wazi kwa watu anaowasimamia, na hili limekuwa tatizo kubwa ndani ya serikali na huko kwenye chama chake.

Anapoyasema haya sasa, maana yake ni kwamba yupo tayari kutumia njia zilezile walizozizoea za kunyima haki watu kuchagua viongozi wanaowataka.
 
Anajua hayo ndiyo yalikuwa maelekezo muhimu kwa Tume ya Uchafuzi, ila amesahau kuwa wapinzani nao wamesoma shule hizohizo walizosoma wao, hata hivyo kwa hali ya kawaida watanzania wengi sana hukosea majina yao na ya maeneo wanayoishi.
 
Back
Top Bottom