Tanzania yang'ara uchaguzi wa mabaraza ya Umoja wa Posta Duniani (UPU)

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
867
947
Abidjan, Ivory Coast, Tarehe 26 Agost,2021.

TANZANIA YANG’ARA UCHAGUZI WA MABARAZA YA UMOJA WA POSTA DUNIANI(UPU)

Tanzania imefanikiwa kupeperusha vema bendera yake kwenye Mkutano Mkuu wa 27 wa Umoja wa Posta Duniani unaoendelea jijini Abidjan, Ivory Coast, baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi wa mabaraza ya Utawala(Council of Administration) na lile la Uendeshaji Council of Operation) la Umoja huo.

Tanzania ilifanikiwa kuingia katika Baraza la Utawala kutoka kundi la Afrika lenye nchi 54 na zilitakiwa nchi 11 kuwakilisha katika Baraza hilo kutoka Afrika, pia Tanzania ilifanikiwa kuingia kwenye Baraza la Uendeshaji la Umoja huo. Hii inaifanya Tanzania kuwa na nafasi mbili muhimu katika uendeshaji wa shughuli za Umoja huo.

Hii ni hatua kubwa katika sekta ya Posta nchini Tanzania ambapo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Umoja huo mwaka 1874 Tanzania haijawahi kuwa mjumbe wa Mabaraza yote kwa pamoja.

Hongera sana Tanzania!

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania
 
Back
Top Bottom