Shaka: Uchaguzi wa Zambia ni ushindi kwa demokrasia ya Afrika

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
SHAKA: UCHAGUZI WA ZAMBIA NI USHINDI KWA DEMOKRASIA YA AFRIKA

"Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawapongeza wananchi wa Zambia kwa kukamilisha uchaguzi mkuu wao kwa amani na utulivu" Shaka Mwenezi Taifa

"Na kumpongeza kwa ushindi Rais Mteule Hakainde Hichilema aliyetangazwa kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika 12 Agosti, 2021 pamoja na Rais Edgar Lungu aliyekubali kukabidhi madaraka" Shaka Mwenezi Taifa

"Wameipa heshima Afrika kuwa inawezekana demokrasia ikatekelezwa na kuheshimiwa bila kuiacha nchi vipande vipande au kuingia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe" Shaka Mwenezi Taifa

"Wanaotaka kufananisha siasa za Zambia na Tanzania wanakosea kwani haziwezi kufananishwa, Zambia chama cha ukombozi UNIP kiliongoza nchi hiyo kwa miaka 27 (1964-1991) kikaondolewa madarakani na Frederick Chiluba wa MMPD (1991-2002), ambaye naye aliondolewa na Levy Mwanawasa (2002-2008) akaja Rupiah Banda (2008-2011), kisha Michael Satta (2011-2014) halafu Edgar Lungu (2015-2021) mpaka leo Hakainde Hichilema wa chama cha UPND" Shaka Mwenezi Taifa

"Siasa za nchi hiyo ni wazi kuwa upinzani wametoana madarakani wenyewe kwa wenyewe hivyo wanaofananisha siasa hizo na za Tanzania wamekosa uelewa mpana na ufuatiliaji wa siasa za kiafrika na kidunia" Shaka Mwenezi Taifa

"Ukitazama mwenendo wao utagundua ukiondoa chama cha UNIP kilichokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi hakuna chama cha upinzani kilichokaa zaidi ya kipindi kimoja ikiwa ni ushahidi kuwa upinzani hauaminiki" Shaka Mwenezi Taifa

" Uchaguzi wa Zambia umetoa somo kwa vyama vya siasa hapa nchini hususani upinzani kuwa mgombea aliyeshinda Zambia wa chama UPND alifanya siasa safi na zaidi wakati wote wa kampeni alikuwa Balozi wa amani na kuhimiza umoja miongoni mwa wananchi wa nchi hiyo akijua tunu hizo ni chachu ya maendeleo" Shaka Mwenezi Taifa

"Hichilema ametoa somo kwa vyama vya upinzani Afrika na hapa nchini kuwa demokrasia sio fujo wala vurugu bali ni mchakato wa kueleza namna unavyoweza kuwaletea wananchi maendeleo" Shaka Mwenezi Taifa

" CCM imeendelea kuaminika kwa wananchi kwa sababu kimekuwa kikiyaishi mahitaji ya umma na kuyatekeleza kikamilifu jambo ambalo daima tutaliendeleza na tunaamini watanzania wataendelea kuzidi kutuamini" Shaka Mwenezi Taifa

20210817_203006.jpg
 
We shall overcome one day. Shaka hajui kwamba Rais Mteuke wa Zambia, ndugu Hakainde Hichilema yuko very much resembled to MBOWE.

Naye alishawahi pewa tuhuma za gaidi, na pia aelewe kuwa katiba ya Zambia na ya Tanzania ni tofauti sana.

Katiba ya Tanzania imempa mamlaka makubwa sana Rais aliyeko madarakani.

Rais ndio huteua tume ya uchaguzi, huteua Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, huteua mkuu wa majeshi, huteua Kamanda Mkuu wa Polisi, huteua Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, huteua Tume ya uchaguzi, yaani kila mteule huteuliwa na Rais.

Kwenye mazingira haya upinzani unashindaje?
 
Binafsi sijawahi muelewa huyu mtu Nini anasimamia tangu ateuliwe...aliyemwelewa atuambie
 
We shall overcome one day. Shaka hajui kwamba Rais Mteuke wa Zambia, ndugu Hakainde Hichilema yuko very much resembled to MBOWE.

Naye alishawahi pewa tuhuma za gaidi, na pia aelewe kuwa katiba ya Zambia na ya Tanzania ni tofauti sana.

Katiba ya Tanzania imempa mamlaka makubwa sana Rais aliyeko madarakani.

Rais ndio huteua tume ya uchaguzi, huteua Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, huteua mkuu wa majeshi, huteua Kamanda Mkuu wa Polisi, huteua Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, huteua Tume ya uchaguzi, yaani kila mteule huteuliwa na Rais.

Kwenye mazingira haya upinzani unashindaje?
Kwa tume na katiba tuliyo nayo ccm itaongoza milele...
 
Back
Top Bottom