Mapema baada ya kupata matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Zambia nikasema ngoja nifuatilie nini kimesaidia chama hichi kuanguka baada ya wananchi wa nchini Zambia kuamua , nimefuatilia chanel mbalimbali za mitandao na Tv za ndani ya Afrika na nje ya Afrika kwa lengo la kujua kulikoni chama tawala nchini Zambia kimepinduka miguu juu kichwa chini
Waandishi wengi walikuwa na maswali mbalimbali kwa wazambia ikiwa pamoja na kuwapa fursa ya kuzungumza juu ya demokrasia yao katika uchaguzi ambapo wale wote waliozungumza hasa umri wa vijana ni kama vile walikuwa wameambiana majibu ambapo kila mmoja alisema kuwa Serikali ya Edgar Lungu haikujali mambo mengi ndani ya wazambia huku wakitoa mifano mbalimbali kutoka katika serikali iliyoanguka:
Yangu ni hayo tu.
Picha ya Rais Mpya ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu nchini Zambia ndugu Haikenda Hichilema , kwa mbalii alitaka kufanana na Majaliwa Kassim Majaliwa

- Serikali ya Lungu ni kama jina lenyewe yaani Lungu kwa maana haikuwa na demokrasia kwa wazambia unyanyasaji ulikuwa mkubwa sana kwa wazambia kupitia jeshi la polisi.
- Tatizo la Ajira, Serikali haikujenga mazingira yoyote ya ajira kwa vijana hivyo wakaamua kuiondoa.
- Mifumuko ya bei hasa katika bidha za chakula . Serikali iliyopita Ilikuwa na mifumuko mingi ya bei ambayo haikujali uchumi wa mzambia hata kidogo hii ni kwasababu binafsi za serikali ya Lungu, wananchi wakasema tunakusubiri katika uchaguzi ujao.
- Sababu nyingine ni kodi za bidhaa nchini zambia. Nchini Zambia asilimia kubwa ya population ya vijana wamejiajiri , lakini chama kilichoanguka kilikuwa na kodi nyingi ambazo hazikuwa na manufaa yoyote kwa maendeleo ya taifa na wananchi kwa ujumla.
- Sera nzuri za chama pinzani ambacho kwasasa ndio chama tawala japokuwa serikali kupitia jeshi la polisi walimzuia Rais mteule katika mikutano yake mingi lakini sera za maendeleo zilizokuwa zikitolewa na Hichilema zilikuwa na matumaini makubwa kwa wazambia.
Yangu ni hayo tu.
Picha ya Rais Mpya ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu nchini Zambia ndugu Haikenda Hichilema , kwa mbalii alitaka kufanana na Majaliwa Kassim Majaliwa