Baadhi ya Viongozi wa Umoja wa Makanisa ya Kitume na Kinabii Tanzania, wakiongozwa na rais wa Umoja huo Nabii Dr. Joshua Aram Mwantyala wamehimiza amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Wameeleza kuwa, Wagombea watakaoshindwa kuchaguliwa na wananchi katika Uchaguzi huo, hawana...
Mgombea ubunge wa Kawe kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Glory Tausi, leo Ijumaa, Septemba 12, 2025 ameendelea na kampeni zake kwa staili ya kupita nyumba kwa nyumba na vijiweni katika mitaa mbalimbali ya jimbo hilo. Picha na Michael Matemanga
Wasimamizi wa uchaguzi mkoani Geita wametakiwa kuhakikisha wanaweka mazingira salama na ya haki, bila vitisho, ununuzi wa kura na upendeleo kama sehemu ya wajibu wao wa kusimamia zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi...
Mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Bakari Shingo amewaahidi wakazi wa jimbo hilo kuwa atatumia fedha za mfuko wa jimbo kutatua changamoto zao kwa haraka na kushirikiana nao bega kwa bega katika shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Magharibi, Wakili Dickson Matata, ameonesha masikitiko yake kwa vyama vya siasa vilivyokubali kushiriki uchaguzi licha ya kuwepo madai ya kukosekana kwa mabadiliko ya msingi katika mfumo wa uchaguzi nchini.
Akizungumza kupitia...
Nimeona video ya mgombea urais Zanzibar kupitia AAFP, Said Soud Said akifurahia kukabidhiwa gari na Tume ya Uchaguzi Zanzibar. Kasahau kama nae ni mgombea Urais kaanza kumnadi mgombea urais kupitia CCM.
Kwa maoni yangu naona hii si aina ya ushindani ambao tunahitaji kwenye uchaguzi, ni ujinga...
Mgombea urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Gombo Samandito Gombo amevitaka vyombo vya dola Nchini kutenda haki kwa vyama vyote vya siasa kwakuwa vipo kwajili ya kuwahudumia watanzania wote.
Kauli hiyo ameitoa kwenye mkutano wa hadhara iliofanyika Kata ya Mahembe Jimbo la Kigoma...
Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amepokewa kwa kishindo alipowasili kwenye uwanja wa Polisi,Longido kwa ajili ya kuwahutubia Wananchi kwenye mkutano wa kampeni leo Ijumaa Septemba 12,2025...
"Maendeleo tunayoyataka ni maendeleo ya watu, yaletwe na watu wenyewe, yaendelezwe na watu wenyewe, yawafuate watu kule walipo. Hii ndiyo maana halisi ya uchumi jumuishi." - Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Samia Suluhu kwenye mkutano wa kampeni Tabora Mjini
BODI YA ITHIBATI YA WAANDISHI WAHABARI UFAFANUZI KUHUSU WANAODAIWA KUWA WAANDISHI WAHABARI KUSHIKILIWA NAJESHI LAPOLISI MKOANIARUSHA
Dar es Salaam
12 Septemba, 2025
Kwa mujibu wa Kifungu cha 13(a) cha Sheria ya Huduma za Habari Sura ya 229, Bodi ina wajibu wa kutoa ithibati na vitambulisho...
Ameandika Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche kupitia ukurasa wake wa Instagram "Magari waliyopewa vyama vya mfukoni kufanyia kampeini ni rushwa.. Lengo ni kujaribu kuhalalisha uchafu huu unaoitwa uchaguzi. Bajeti ya serikali inapitishwa na bunge, Tume waseme wametoa hizo fedha wapi...
Mbunge Mstaafu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Salome Makamba apiga magoti mbele ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi(CCM) kumuombea kura mgombea nafasi ya Urais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye anaendelea na kampeni zake za kumwaga sera katika mikoa mbalimbali.
Soma pia: Salome...
Wakati ambao mchakato wa kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu ukiendelea, Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kivule, lilipo Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, Ndugu Massaburi Dougras Didas ameungwa mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na...
Ukweli ni kwamba CCM wanatumia nguvu kubwa sana ya kufanya kampeni na kushawishi umma kuhusu uchaguzi kama vile wako vitani. Wameshadhibiti miiba na mizumari sijui kwanini wanahangaika sana na tunajua kwamba hivyo vyama vingine ni kama matawi yake tu. Hadi sasa CHADEMA hawashiriki kwenye...
Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar kwa kushirikiana na Mamlaka ya usafiri na usalama barabarani pamoja na mamlaka nyingine zimefanikiwa kukamata namba zisizotambulika na mamlaka husika zilizokuwa zikifungwa katika eneo la kibati cha namba (Plate number) kwenye vyombo vya moto.
Akizungumza...
Kupunguzwa kwa kodi za vyombo vya usafirishaji kumewaletea nafuu maafisa usafirishaji mkoani hapa, hali iliyowasukuma kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwatengenezea mazingira rafiki ya kazi.
Akiwasilisha shukrani kwa niaba ya maafisa usafirishaji wenzake, Mweka Hazina wa Chama cha...
Wananchi wa Jimbo la Manonga wameeleza kuumizwa na kitendo cha aliyekuwa Mbunge wao, Seif Hamisi Gulamali, kutorejea tena kugombea Ubunge katika jimbo hilo.
Wakizungumza kupitia taarifa ya makala maalum, wananchi hao wameeleza kuwa jina la Gulamali limeacha alama kubwa ya kisiasa na maendeleo...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.