serikali

  1. Yoda

    JamiiForums Tanzania Serikali ya CCM ilikuwa na mpango wowote wa kujenga refinery ya mafuta?

    Kabla ya Dangote kusema anataka kujenga refinery Africa Mashariki serikali ya CCM katika kile ambacho huita ilani ilikuwa ina mpango wowote wa kujenga refinery au Dangote ndio aliwaamsha wakaona uhitaji wa refinery? Au pia ni kwa sababu jirani ana mpango wa refinery na sisi lazima tujenge...
  2. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Serikali imetenga Sh. Bilioni 1.2 kujenga daraja la kisasa la chuma (Mita 30) katika Mto Nyameni, Kata ya Ulaya - Kilosa

    Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa wameelezwa kuwa watanufaika na Shilingi Bilioni 1.2 zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu kwa ajili ya ujenzi wa daraja la kisasa la chuma lenye urefu wa Mita 30 katika Mto Nyameni, Kata ya Ulaya, mradi...
  3. F

    JamiiForums Tanzania TBC isijidanganye kwa jina la serikali

    Siku moja tulikuwa katika kikao chenye wajumbe kadhaa kwa ajili ya maandalizi ya shughuli iliyokuwa irushwe na vyombo vya habari. Mapendekezo yakaanza kutolewa kuhusu vyombo vya habari vitakavyoalikwa. Kila chombo kilitajwa kimoja baada ya kingine. Ilipofika zamu ya TBC, mjadala ukaibua swali...
  4. A

    JamiiForums Tanzania KERO Responded Serikali inahamasisha matumizi ya nishati safi lakini gharama zake zipo juu sana

    Ninaomba kufikisha kero yangu kwa Waziri wa Nishati. Serikali inahamasisha wananchi kutumia nishati safi kama gesi na umeme ili kupunguza matumizi ya mkaa na kulinda mazingira, lakini gharama za nishati hizi bado ni kubwa kwa wananchi wengi. Gesi nayo imekuwa na bei ya juu, mtungi mdogo...
  5. mwanamwana

    JamiiForums Tanzania Azim Dewji: Siamini serikali inaweza kuwa na sababu ya kumpoteza mtu; anaweza kufungwa au kutafutiwa kesi ili kumuondoa kwenye reli

    Mhoji (Charles William): Mara nyingi unapotoka kuzungumzia kuhusu masuala ya amani, utulivu na jinsi ambavyo watu hawatakiwi kuendeshwa na propaganda, kuna watu wamekuwa wakisema mzee Azim Dewji anatakiwa kuungana na Watanzania ambao wanalaani baadhi ya vitu vinavyotokea hapa Tanzania, matukio...
  6. DogoWaNjombe

    JamiiForums Tanzania Kamati ya Wamiliki wa Nyumba Sinza: Tumeazimia kusitisha ushiriki wetu kwa muda katika Mradi wa Sinza

    Kamati ya Wamiliki wa Nyumba Sinza inaendelea kusisitiza kuwa haipingi maendeleo wala uendelezaji wa eneo la Sinza. Hata hivyo, tunaamini mchakato huu unapaswa kufanyika kwa kuzingatia sheria, taratibu na mawasiliano rasmi. Baada ya Waziri kutangaza kuwa mchakato wa awali umefutwa na kwamba...
  7. Fbn

    JamiiForums Tanzania Nchi ina maigizo mengi na pesa za serikali zinavyotumika kupoteza ukweli

    Zuchu anajifungua alafu pesa zunatunzwa USD hospital. Baada mda stive Nyerere anaita wanahabari kama ana mfokea na kusema hizo pesa zisaidie hospital. Unashangaa raisi anasema wamefanya vizuri wa sanii na wemepeleka hospital sijui ya nani. Subirini muone kuanzia huu uzi mpaka mkifika 2030...
  8. Lunovar

    JamiiForums Tanzania Ni muda wa serikali kukaribisha wawekezaji kwenye barabara zetu

    Kiukweli mi naona kwenye swala la maendeleo ya barabara katika nchi hii serikali imeshindwa kabisa. Barabara nyingi nchini na muhimu kwa ustawi wa uchumi wa nchi ni mbovu kupita maelezo na cha ajabu unakuta ndio barabara ambazo hata viongozi hutumia kwenda kwenye shughuli zao. Nitolee mfano wa...
  9. Pendaelli

    JamiiForums Tanzania Norway Fund ni kitu ambacho kinapaswa kuigwa na serikali ya Tanzania kwa mustakabali wa kizazi kijacho

    Amani kwa wote. Naomba kujenga hoja yangu katika msingi wa mustakabali wa taifa kwa vizazi vinavyo tuandama. Mimi kama baba ambaye nina watoto , moja kati kitu kinacho nipa mawazo makubwa ninini nitawaachia watoto wangu, na kizazi kinacho tokana na mimi. Wazee wangu walishindwa kacha...
  10. A

    JamiiForums Tanzania KERO Miezi 11 Bila Mshahara Chuo cha Afya Mvumi (MIHS) kilichopo Dodoma, Serikali Iingilie kati

    Wafanyakazi katika Chuo cha Afya Mvumi (Mvumi Institute of Health Sciences – MIHS) kilichopo Mvumi, Dodoma tunaomba msaada na uingiliaji wa mamlaka husika kutokana na changamoto kubwa zinazotukabili kwa muda mrefu. Kwa sasa baadhi ya wafanyakazi tumekaa takribani miezi 11 bila kulipwa mishahara...
  11. DogoWaNjombe

    JamiiForums Tanzania Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuzihoji Halmashauri 39 zenye dosari za Ukaguzi

    Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeanza kuzihoji Halmashauri 39 kutoka Mikoa 15 zilizobainika kuwa na hoja mbalimbali katika Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za Mwaka wa Fedha 2023/2024 na 2024/2025. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa...
  12. DogoWaNjombe

    JamiiForums Tanzania Semu: Maridhiano ya kweli, Serikali iwaachie huru wafungwa wa Kisiasa, iruhusu uchunguzi huru wa Kimataifa wa Oktoba 29

    Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amesisitiza kuwa Tanzania haiwezi kufikia maridhiano ya kweli na ya kudumu bila kuwepo kwa misingi ya ukweli, haki na uwajibikaji. Semu ametoa kauli hiyo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu ya Madiwani wa ACT Wazalendo kutoka kata...
  13. A

    JamiiForums Tanzania KERO Serikali, TNMC tusaidieni. Watumishi hospitali ya KAMANGA-Nyegezi, MWANZA tunateseka

    Uongozi wa hospital ya KAMANGA-Nyegezi, MWANZA unatulazimisha wafanyakazi kufanya shift mbili, hii ni nje ya utaratibu rwa serikali na hupunguza ufanisi tunapokuwa kazini na huhatarisha Afya kwa wagonjwa. Malipo duni ya Muda wa ziada na tunavuliwa uongozi na kutishwa kufukuzwa kazi tunaposemea...
  14. O

    JamiiForums Tanzania Serikali yachukua hatua kumaliza mgogoro wa Mwekezaji na mwananchi kwenye fukwe Luchelele Mwanza

    Serikali yachukua hatua kumaliza mgogoro wa Mwekezaji na mwananchi kwenye fukwe Mwanza Serikali imeanza kuchukua hatua za kumaliza mgogoro wa Ardhi uliodumu kwa takribani miaka minne tangu 2022 kati ya mwekezaji, Amirali Manji na Mohamed Bakiri dhidi ya Moses Zakaria Joram ambae ni Mmiliki wa...
  15. A

    JamiiForums Tanzania HOJA Veterinary Interns Tanzania Tunaachwa Nyuma – Serikali Isikie Kilio Chetu

    Mimi ni mmoja wa wanafunzi wa Shahada ya Udaktari wa Mifugo ambao tunatarajia kufanya internship ya mwaka mmoja kabla ya kupata usajili wa kufanya kazi kama madaktari wa mifugo. Leo tumekutana na Naibu Msajili wa Baraza la Madaktari wa Mifugo Tanzania (VCT) ambaye alitueleza utaratibu wa...
  16. mrxtz2026

    JamiiForums Tanzania Muundo Bora wa Muungano ni Upi: Serikali Moja, Mbili, Tatu au Shirikisho? Lete Hoja Yako, Tuichambue Pamoja, Kisha Piga Kura

    Miongoni mwa maswali magumu zaidi katika mchakato wa Katiba Mpya ni muundo wa Muungano. Badala ya kubishana, hebu kila mmoja alete hoja yake kwa nini anaona muundo fulani ni bora, tuchambue faida na hasara kwa pamoja, kisha tupige kura kwa uzito wa hoja, si kwa hisia. Nianze mimi kwa kuweka...
  17. A

    JamiiForums Tanzania HOJA Serikali iboreshe huduma za usafiri wa anga na kushusha gharama za nauli ili Wananchi wengi wapande

    Serikali iangalie kwa karibu sekta ya usafiri wa anga nchini, hasa suala la gharama kubwa za nauli za ndege ambazo zimekuwa changamoto kwa Watanzania wengi. Kwa sasa, wananchi wengi wanashindwa kumudu usafiri wa anga kutokana na bei kuwa juu ukilinganisha na uwezo wao wa kifedha. Tunaiomba...
  18. Manyanza

    JamiiForums Tanzania Serikali ya Tanzania inapotenga bajeti ya kujenga magereza mengi ijifunze kutoka nchi ya Uholanzi

    Uholanzi ni mfano wa nchi iliyoonyesha kwamba usalama wa taifa haujengwi kwa kuongeza magereza pekee, bali kwa kupunguza sababu zinazowasukuma watu kuingia kwenye uhalifu. Kwa miongo miwili iliyopita, idadi ya wafungwa nchini humo ilishuka kwa kiasi kikubwa, hali iliyosababisha kufungwa kwa...
  19. A

    JamiiForums Tanzania DOKEZO Mamlaka za Serikali zichunguze Mradi wa Kongani la viwanda Maranje wenye thamani ya zaidi ya Sh Bilioni 300

    Serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) inatekeleza mradi wa Kongani la Viwanda vya Korosho wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 300 katika eneo la Maranje, Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara, unaolenga kuongeza ubanguaji wa korosho ndani ya nchi ifikapo Mwaka 2030. Hata...
  20. A

    JamiiForums Tanzania Responded HOJA Serikali ilitoa msamaha wa kodi kwa Wafanyabiashara wapya ila TRA bado wanakomaa nao, msamaha ulifutwa?

    Kama sikosei, mwaka huu 2026 Serikali ilitoa utaratibu wa kuwaruhusu wafanyabiashara wapya kufanya biashara kwa kipindi cha mwaka mmoja bila kutozwa kodi, ikiwa wamejisajili na kupata namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN), na suala hilo lilipitishwa na Bunge. Swali langu ni moja: kwa nini...
Back
Top Bottom