Siku kadhaa na hasa miaka kadhaa iliyopita, nilianza kusikia habari za 'mfumo imara' kuwa ndiyo unaofaa zaidi kuliko 'kiongozi imara'.
Mwanzoni sikutilia maanani. Lakini, siku za hivi karibuni hili fungu la maneno la 'mfumo imara' limejizolea sifa ya kutajwa mara kwa mara kwenye mitandao mingi...