Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
WAPI ALIPO RAIS WETU?
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema kimeitaka serikali ya nchi hiyo kujitokeza na kueleza alipo rais John Magufuli na hali magufuli na yuko katika hali gani.
Kauli ya Chadema inakuja wakati ambapo kuna siutafahamu juu ya alipo rais Magufuli.
Mara ya mwisho kwa kiongozi huyo wa Tanzania kuonekanaka ilikuwa Jumamosi ya Februari 27.
Katika mkutano na wanahabari leo Ijumaa Machi 12, Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika amesema kuwa wananchi wana haki ya kupata taarifa rasmi kutoka serikalini juu ya kiongozi wa nchi yao.
Viongozi wa chama tulikaa kikao na kujadili baada ya kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya kimataifa vikihoji yuko wapi rais Magufuli na baadhi vikienda mbali zaidi na kusema ni mgonjwa na yuko nchi jirani kwa matibabu... Kabla ya tamko hili kumekuwa vuta nikuvute mtandaoni baina ya watu binafsi na baadhi ya viongozi mtandaoni juu ya swali hilo," ameeleza Mnyika.
Juhudi za kumpata Msemaji wa Serikali ya Tanzania kuelezea suala hilo bado zinaendelea.
Akijibu baadhi ya maswali hayo mtandaoni, Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Mwigulu Nchemba amesema kuwa: "Kiongozi wa nchi sio Mzee wa Kanisa kwamba alipangiwa zamu na hakuoneka...Kiongozi wa nchi sio mtangazaji wa TV kwamba alikuwa na kipindi na hakuonekana... sio kiongozi wa jogging club anatakiwa kuwa tu mtaani kila siku..."
Awali kabla yake pia waziri wa habari Sanaa utamaduni na michezo Innocent Bashungwa alionya watu kusambaza taarifa ambazo si za kweli mitandaoni na kwamba wangeshughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Reuters, Balozi wa Tanzania nchini Namibia ameliambia Shirika la habari la mchi hiyo kuwa rais Magufuli ni mzima wa afya na anaendelea na shughuli zake nchini Tanzania.