Mlio karibu na Rais Magufuli, naomba muulizeni swali hili na awape majibu

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
348
1,000
Wadau amani kwenu...

Kuna jambo linanitatiza na kunisumbua sana kichwa. Nimedokezwa humu JF kuna watu al-maarufu kama "vipenyo" yaani watu kutoka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ambao wana access ya kumfikia mzee baba.

Ninaomba wanisaidie kumuuliza nini faida na manufaa yaliyopatikana kufuatia maamuzi haya kama nchi.

(1). Nini faida ya kuzipiga "ban" vyombo vya habari vilivyokuwa vinakosoa Serikali na kuibua matendo ya ufisadi?

(2). Nini faida iliyopatikana kwa kukataza vyama kufanya siasa kwa miaka mitano iliyopita?

(3). Nini faida ya wazi iliyopatikana kwa kuwapiga, kuwatesa, kuwafunga wapinzani ambao nao ni Watanzania?

(4). Nini faida iliyopatikana kwa kuwatimua wale wanafunzi 8000 huko UDOM na kuitwa "vilaza"?

(5). Nini faida iliyopatikana/inayopatikana kwa kwenye kwa kuchoma nyavu za wavuvi ziwa Victoria tena kwa kupigwa wengine kuuliwa?

(6). Kuna faida gani iliyopatikana kwa kuhusisha JWTZ kuvamia na kupora fedha katika maduka ya kubadilisha fedha huko Arusha?

(7). Nini faida iliyopatikana kwa uamuzi wa kupora fedha za wafanyabiashara Benki kwa "task force" badala ya wataalamu wa kodi?

(9). Nini itakuwa faida ya kuwa na Bunge lisilokuwa na wapinzani kwa uamuzi uliofanywa na dola isiyo ya kikatiba?

(10). Nini faida ya kiuchumi tutakayopata kwa kujitenga na dunia katika vita dhidi ya Covid-19?

Ndugu zangu, tunaweza kumlaumu Rais Magufuli kumbe kuna faida nyingi tutapata kwa maamuzi haya. Hebu tujadiliane kwa hoja pengine uwezo wangu wa kuona Mambo ni mwembamba. Msalimieni.
 

Fund man

JF-Expert Member
Feb 24, 2021
506
1,000
Hawawezi kumuuliza mkulu. Ila yeye anaweza kuwaagiza atakavyo wafanye.
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
5,617
2,000
Tatizo hii nchi ina wajinga wengi hawawezi kukuelewa , anayoyafanya yalitakiwa yafanywe na msimamizi ambaye yupo chini ya kiongozi mwenye busara na hekima.

Kama ilivyokuwa Kwa kamanda Yoabu (Mtu mwenye ujasiri asiye na busara) lakini akiwa chini ya Mfalme Daudi (Mwenye akili, busara na hekima). Anayoyafanya Kwa nje ni kama mema ila yanakosa busara na hekima yakiongozwa na ukurupukaji inashangaza watu na makalio Yao wanamsifia
 

jaluo jr

JF-Expert Member
Feb 10, 2018
424
1,000
Hivi ni kweli haya maamuzi anayafanya yeye Magufuli au wasaidizi wake wanamshauri hivyo? Mbona vitu vingine anasema wasaidizi Wake wamemkataza asifanye kama vile kuendesha Gari.
 

Iboya2021

JF-Expert Member
Dec 1, 2020
903
1,000
Maswali mepesi yanajibika halafu yote ya kinafiki kabisa hivi unauliza wapinzani kupigwa wewe na akili zako unaenda kuandamana sehemu kama segerea gerezani unajua kabisa kuna wafungwa wenye makosa makubwa halafu ukipigwa unakuja kuuliza hapa JF mbona hutumii hata akili ya kuvukia barabara tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom