Naomba Majibu Tafadhali: 'Mfumo imara' ni nini?

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,310
2,000
Siku kadhaa na hasa miaka kadhaa iliyopita, nilianza kusikia habari za 'mfumo imara' kuwa ndiyo unaofaa zaidi kuliko 'kiongozi imara'.
Mwanzoni sikutilia maanani. Lakini, siku za hivi karibuni hili fungu la maneno la 'mfumo imara' limejizolea sifa ya kutajwa mara kwa mara kwenye mitandao mingi ya kijamii; hata humu jamvini (www.jamiiforums.com), fungu hili la maneno limejizolea sifa hizo hizo.

Kwa msingi huo nikaanza kuvutiwa na fungu hili la maneno hasa nikitaka kujua lina maana gani. Leo asubuhi, kwa saa za Tanzania, kuna mwanabodi/mkuu mmoja ameibua hoja akiwa anasisitiza tuwe na 'mfumo imara'. Nimelazimika kumuuliza maana yake lakini mpaka sasa hajanipa majibu. Nilimuuliza kama fungu langu la maneno nilivyolinukuu hapa chini.

Nimerudi
===
Asante sana kwa bandiko lako murua.

Nina maswali kadhaa kutokana na bandiko lako hili.

1. Mfumo imara ni nini hasa? Yaani ni kitugani, jambo gani, hali gani na kiko, liko, ikoje?
2. Naomba unipe na kunifafanulia kinagaubaga tabia/desturi/tamaduni za "mfumo imara". Naomba pia katika kufafanua hili utumie mifano halisi ili kunirahisishia uelewa wa hii " mfumo imara"
===
Natanguliza shukrani kwa majibu ya maswali yangu.

Nakutakia asubuhi njema.

Nimebaki nikiwa TUJITEGEMEE.

Kwa hiyo, kwa heshima kubwa kabisa, ninaomba yeyote mwenye uelewa juu ya 'mfumo imara' na anaweza kujibu maswali yangu kama yalivyo kwenye nukuu hapo juu, afanye hivyo kwenye uzi huu.

Natanguliza shukrani kwa majibu yatakayoletwa.

Nimebaki nikiwa TUJITEGEMEE.
 

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
905
1,000
Siku kadhaa na hasa miaka kadhaa iliyopita, nilianza kusikia habari za 'mfumo imara' kuwa ndiyo unaofaa zaidi kuliko 'kiongozi imara'.
Mwanzoni sikutilia maanani. Lakini, siku za hivi karibuni hili fungu la maneno la 'mfumo imara' limejizolea sifa ya kutajwa mara kwa mara kwenye mitandao mingi ya kijamii; hata humu jamvini (www.jamiiforums.com), fungu hili la maneno limejizolea sifa hizo hizo..
Nafikiri humaanisha kwamba kiongozi awepo pale kama robot, afu nchi, taasisi na idara zake vijiendeshe automatic kulingana na sheria mama ya nchi na sheria zinginezo. Kazi ya rais iwe ni kupewa taarifa, kushauriwa na kutoa maamuzi kulingana na alivyoshauriwa.

Mashabiki wa "mfumo imara" wanapenda nchi iongozwe hivi ili wafanye watakavyo. Ni wapigaji balaa, maana ndani ya "mfumo" ni kama serikali ndani ya serikali. Hawakumpenda JPM maana alivuruga hiyo "mifumo imara" yao, akatengeneza mfumo imara wake. Stuka mtu anayekwambia hatutaki kiongozi imara tunataka mifumo imara. Ni mafisi kwenye ngozi ya kondoo.
 

Mbeya City Spurs I

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
488
1,000
Siku kadhaa na hasa miaka kadhaa iliyopita, nilianza kusikia habari za 'mfumo imara' kuwa ndiyo unaofaa zaidi kuliko 'kiongozi imara'.
Mwanzoni sikutilia maanani. Lakini, siku za hivi karibuni hili fungu la maneno la 'mfumo imara' limejizolea sifa ya kutajwa mara kwa mara kwenye mitandao mingi ya kijamii; hata humu jamvini (www.jamiiforums.com), fungu hili la maneno limejizolea sifa hizo hizo...
Wafuasi wa hicho kitu kiitwacho "mfumo imara" ni wale watu wavivu na dhaifu kiutendaji. Wasioamini katika uongozi. Watu kaliba ya yule CAG mstaafu aliyezinduka juzi akasema angalau asilimia 60 ya watumishi wa umma hawana uwezo stahiki.

Yeye kwa mfano, alitolea mfano kampuni ya Microsoft. Akasema kuwa pale hata mtu mjingamjinga tu anaweza kupewa kitengo akiongoze kwa kuwa taasisi kama taasisi ina mfumo imara!

Iko hivi. Watu au viongozi ni sehemu tu ya mfumo wa uendeshaji taaasisi. Hivyo mfumo ni kitu kipana zaidi ya watu. Yaani kama ilivyo kwa dhana ya jogoo na kuku.

Hata hivyo, kinachohakikisha mfumo imara ni watu kama ifuatavyo;

1. Utahitaji watu sahihi ili wakakuwekee mfumo imara pale ambapo taasisi ina mfumo dhaifu. Usitegemee watu dhaifu kuasisi mfumo imara. Utahitaji watu wenye utashi mkubwa ili waje na mfumo imara. Hata hizo Microsoft zilianza hivyo. Ilihitaji mtu imara (Bill Gates) kuasisi mifumo imara ndani ya Microsoft.

2. Pia ni watu imara tu watakaofanya mfumo imara ulete matokeo tarajiwa. Kuweka watu dhaifu kwa kuwa tu mfumo uliopo ni imara kutafanya mambo yafanyike kwa "business as usaual".

3. Vile vile maboresho ya mifumo husika ndani ya taasisi yatafanyika endapo tu kutakuwa na wasimamizi (watu) imara. Watu dhaifu hawatakuwa na "initiative" ya kuhuisha mfumo kadri muda unavyoenda kwani tayari akilini mwao wanaona mfumo imara tayari. Watu dhaifu ni kama robots. Wao huenda na mfumo uliopo tu. Hakuna "intuition" maana intuition kwao ni udikteta! Yaani kwamba ili mifumo ya Microsoft iendelee kuwa up to date, inahitaji watu imara wenye utashi wa kiwango cha juu ili kumudu ushindani na mabadiliko.


Bill gates anayo falsafa yake moja kuwa "kazi ngumu mpe mtu mvivu ili atafute namna rahisi ya kuifanya". Ni hii falsafa inayowachanganya watu wavivu kama huyo CAG mstaafu, mzee wa mfumo imara. Hii falsafa inalenga wafanyakazi au watendaji wa kazi (employees). Sahau kuhusu siku moja taasisi kama Microsoft kuajiri meneja au mkurugenzi "mjinga mjinga".

Nafasi za uongozi kwenye taasisi zinazojitambua hutolewa kwa watu wenye kaliba ya juu ya uongozi. Na mara nyingine huwapa mamlaka makubwa sana ya kutumia utashi wao binafsi. Hao wafuasi wa mfumo imara kazi yao huwa kusubiri ma-genius (watu) watengeneze mifumo imara kisha wao waje kuwa watekelezaji. Maana watu wa aina hii sifa zao kubwa ni uvivu na uwezo mdogo wa kufanya maamuzi.

Mifano mizuri ya namna watu sahihi walivyo muhimu kupata mifumo mizuri au taasisi imara ni teuzi kadhaa zilizofanyika kwenye taasisi kubwa za umma kati ya 2015 na 2020;

Mpango - TRA
Luoga - BoT
Kakoko - TPA
Kadogosa - TRC

Angalia namna ufanisi kwenye hizo taasisi ulivyobadilika mara baada ya kuteuliwa watu sahihi. Niambie TPA ipi ilikuwa na mfumo imara: ile ya 2018 vs ile ya 2013.

Tanesco haijabadilishiwa sheria yoyote ile lakini anagalia namna uendeshaji wake ulivyobadilika mara baada ya kuanza kuteuliwa watu sahihi badala ya wale waliokuwa wakiiuza nchi.
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,777
2,000
Siku kadhaa na hasa miaka kadhaa iliyopita, nilianza kusikia habari za 'mfumo imara' kuwa ndiyo unaofaa zaidi kuliko 'kiongozi imara'.
Mkuu TUJITEGEMEE

Obama Speech ni Ghana - July 11, 2009

Now, make no mistake: History is on the side of these brave Africans, not with those who use coups or change constitutions to stay in power. Africa doesn't need strongmen, it needs strong institutions.

========

Mfumo/Taasisi imara (Strong Instituion)

Kiongozi Imara (Strong Men)

Mkuu, sina uhakika sana na haya majibu yangu, lakini bila shaka wanamaanisha kunatakiwa kuwa na independent Judiciary, Executive and Legislation.

Wanaodai Tanzania hakuna mfumo imara wanabebwa na hoja kwamba, Executive (Presidency) inakuwa na nguvu kubwa mno kiasi kwamba inaingilia utendaji wa mihimili mingine ya dola kama nilivyokwishaitaja hapo juu.

Mimi sio mwanasiasa lakini nimejaribu kufafanua kadri ya uelewa wangu mdogo ulipofika.
 

PANAFRICA

Senior Member
Apr 2, 2012
173
250
Siku kadhaa na hasa miaka kadhaa iliyopita, nilianza kusikia habari za 'mfumo imara' kuwa ndiyo unaofaa zaidi kuliko 'kiongozi imara'.
Mwanzoni sikutilia maanani. Lakini, siku za hivi karibuni hili fungu la maneno la 'mfumo imara' limejizolea sifa ya kutajwa mara kwa mara kwenye mitandao mingi ya kijamii; hata humu jamvini (www.jamiiforums.com), fungu hili la maneno limejizolea sifa hizo hizo...
Mfumo imara ni utaratibu mahususi unaotungwa kwa mbinu shirikishi na kwa umakini wa kiwango cha juu kabisa wa uendeshaji shughuri za nchi kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi na kwa maslahi mapana ya vizazi vijavyo. Mifumo hii haitakiwi kuingiliwa wala kubadilishwa na kiongozi yeyote awae, Bali inatakiwa kuheshimiwa na kufuatwa na kila kiongozi awae.

Mfano:
Sera ya elimu ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yoyote ile,lakini kama hakuna mfumo thabiti wa kuitengeneza na kuilinda, ndo unakuta kila kiongozi wa kila awamu anafanya mabadiliko kwa maslahi yake mwenyewe na familia yake na jamaa zake.

Hii ni pamoja na Katiba ya nchi, kama katiba ya nchi inatoa nafasi ya kuthibiti mamlaka ya kiongozi wa nchi, hapo tunaweza kusema kwamba nchi ina mifumo imara.

Lakini kama kiongozi wa nchi anaweza kufanya atakavyo bila Wasiwasi wowote, basi hapo nchi inakuwa na mifumo dhaifu ya kiutawala, na ndiyo maana.

Rais Obama alipokuja hapa nchi mwaka 2014 akihutubia waandishi wa habari pale ikulu, alisema;

Afrika haihitaji viongizi wenye manguvu, Bali inahitaji mifumo yenye nguvu.

Africa doesn't need strong men. Africa needs strong institutions.

Au nadanganya ndugu zangu.
 

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
905
1,000
Mfumo imara ni utaratibu mahususi unaotungwa kwa mbinu shirikishi na kwa umakini wa kiwango cha juu kabisa wa uendeshaji shughuri za nchi kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi na kwa maslahi mapana ya vizazi vijavyo. Mifumo hii haitakiwi kuingiliwa wala kubadilishwa na kiongozi yeyote awae, Bali inatakiwa kuheshimiwa na kufuatwa na kila kiongozi awae...
Kuna commenter mmoja hapo juu aliyejibu ( na nashawishika) kwamba huwezi kuwa na mfumo imara bila kuwa na watu imara, ila inawezekana kuwa na watu imara bila kuwa na mifumo imara.

Hili si swali la kuku na yai kipi kilianza. Hili lipo wazi kabisa kwamba kiongozi imara anahitajika awepo kwanza ili kuwepo mfumo imara.
 

PANAFRICA

Senior Member
Apr 2, 2012
173
250
Kuna commenter mmoja hapo juu aliyejibu ( na nashawishika) kwamba huwezi kuwa na mfumo imara bila kuwa na watu imara, ila inawezekana kuwa na watu imara bila kuwa na mifumo imara. Hili si swali la kuku na yai kipi kilianza. Hili lipo wazi kabisa kwamba kiongozi imara anahitajika awepo kwanza ili kuwepo mfumo imara.
Unaweza ukaeleza vizuri hoja yako kwa context ya hapa kwetu kwa mfano?
 

selemala

JF-Expert Member
Feb 14, 2007
221
250
Siku kadhaa na hasa miaka kadhaa iliyopita, nilianza kusikia habari za 'mfumo imara' kuwa ndiyo unaofaa zaidi kuliko 'kiongozi imara'.
Mwanzoni sikutilia maanani. Lakini, siku za hivi karibuni hili fungu la maneno la 'mfumo imara' limejizolea sifa ya kutajwa mara kwa mara kwenye mitandao mingi ya kijamii; hata humu jamvini (www.jamiiforums.com), fungu hili la maneno limejizolea sifa hizo hizo...
Dhana ya mfumo imara


Hii inaweza saidia..
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,697
2,000
Kwanza utambue hakuna mfumo imara kama hapatakuwepo na sheria za kusimamia watakaokuwa kwenye huo mfumo watimize majukumu yao kwa mujibu wa sheria, hapa sheria lazima iwalinde bila kujali nani wa kutoka chama gani anaongoza nchi.

Ndio maana sasa hivi kila anaejielewa anapigania uwepo wa Katiba Mpya, hii itafanya watu watakaokuwa kwenye post serikalini watimize majukumu yao kwa uhuru bila hofu ya kuingiliwa na nguvu toka kwenye chama chao.

Mfano issue ya kamati iliyoundwa kuchunguza upotevu wa pesa bank kuu, kama itatokea baadhi ya watu wenye nafasi serikalini wakakutwa na hatia itakuwa nguvu kuwashughulikia kwasababu patakuwepo na muingiliano kati ya chama na serikali, neno "wenzetu" linaweza kutumika kuwaokoa.

Hizi strong institutions mfano mahakama nazo zikiwa imara bila kutegemea mhimili mwingine kama serikali kwenye issue za budget, au kuchagua mahakimu na majaji, lazima zipewe mamlaka kisheria kujiamulia mambo yao ili wakija kwenye issue za maamuzi basi maamuzi yao yawe huru yasiyolenga kumfurahisha yeyote.

Mfumo sio watu kama wengi navyoona hapo juu wanavyojaribu kuelezea, nguvu ya mfumo inaletwa na sheria bila kujali ni wakina nani wako kwenye huo mfumo, ndio maana leo hii watu wanasema kwa mfumo huu tulionao hata kama chama cha upinzani kitaingia ikulu bado kuna uwezekano wa madudu tunayoyaona leo yakaendelea kuwepo kwasababu sheria mbovu tulizonazo (katiba) ndio zimeweka mfumo mbovu tulionao, hata kama utabadilisha watu lakini madudu yatabaki palepale kwa sababu gap la sheria bado litakuwepo.
 

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
905
1,000
Unaweza ukaeleza vizuri hoja yako kwa context ya hapa kwetu kwa mfano?
Nyerere alirithi nchi kutoka kwa mkoloni (mwingereza) ikiwa chini ya mifumo ya matabaka "caste" na "tribal" systems. Kulikuwepo tabaka la wazungu, wahindi na waarabu na wazawa weusi. Kazi ya kwanza ilihitaji kiongozi imara atakayevunja hayo matabaka na kuweka mfumo wake mwingine, na ndicho alichokifanya Nyerere.

Magufuli alirithi mifumo naweza kuiita "imara" iliyoasisiwa na Mkapa na Kikwete. Mifumo hii iliyowekwa kisheria ili kumsidia rais ilikuwa hijacked na wajanja ili kutengeneza ufisadi wa kimfumo, yaani sytemic corruption. Yaani ufisadi unafanyika lakini kwa vile una vibali vyote vya kitaasisi kwa mfano watu kufanya vikao na safari safari za ndani na nje ya nchi za mara kwa mara za "kikazi" lakini watu walifanya hivyo maana ni "kazi" yao.

JPM akavivunja hivyo vimifumo vyao na kutengeneza mfumo wake. Ndio maana tunasema ni hatari sana kusema una mfumo imara kama watu ni wabovu. Tunahitaji strongmen watakaoweka strong institutions, halafu hizo strong institutions ziwe maintained na strongmen.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,697
2,000
Nyerere alirithi nchi kutoka kwa mkoloni (mwingereza) ikiwa chini ya mifumo ya matabaka "caste" na "tribal" systems. Kulikuwepo tabaka la wazungu, wahindi na waarabu na wazawa weusi. Kazi ya kwanza ilihitaji kiongozi imara atakayevunja hayo matabaka na kuweka mfumo wake mwingine, na ndicho alichokifanya Nyerere...
Unajichanganya, huwezi kusema mfumo unawekwa na mtu kama ulivyotumia mfano wa Magufuli, mfumo imara unawekwa na sheria itakayotoa miongozo ya hao watakaokuwa wanaongoza hizo taasisi waweze kuziendesha bila kuingiliwa na yeyote wakitimiza majukumu yao, na hivyo hivyo wakiharibu washtakiwe bila kuangalia wao ni wakina nani toka chama gani.

Unaposema Magufuli aliweka mfumo imara kwa kutolea mfano wa hizo safari za nje huo sio mfumo hiyo ni direction yake tu, leo Samia akiamua kurudisha zile safari hakuna popote atakapobanwa na sheria yoyote, hivyo ukizungumzia mfumo siku zote ujue ni muongozo unaotoa direction ya kuongoza jambo bila kujali ni nani anaongoza wakati huo, yeyote atakayekuja ataukuta huo muongozo na lazima aufuate, akizingua atabanwa na sheria.
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,145
2,000
Safi sana mkuu umetafsiri vema kabisa na mimi nimekuelewa vema,Welldone na kwa wale ambao sio wavivu wa kujisomea na kutafiti,someni na fanya utafiti kuona ni jinsi gani President Madiba alitengeneza serikali yake na kuacha legancy ya kuwa moja ya nchi zenye mifumo imara ya kusaidia utawala bora,aliifanya nchi iwe ya kikatiba na mahakama ya katiba ndio inayotafsiri sheria za nchi na hakuna aliyejuu ya sheria ,ndio maana sitting president au ex presidents wote wanaweza kushitakiwa mahakamani na elewa yeye mwenyewe(Madiba)alisimama kizimbani akiwa president na case ikamshinda!
 

PANAFRICA

Senior Member
Apr 2, 2012
173
250
Wafuasi wa hicho kitu kiitwacho "mfumo imara" ni wale watu wavivu na dhaifu kiutendaji. Wasioamini katika uongozi. Watu kaliba ya yule CAG mstaafu aliyezinduka juzi akasema angalau asilimia 60 ya watumishi wa umma hawana uwezo stahiki...
Binafsi mimj ni mfuasi mwaminifu wa mifumo imara, naamini kabisa kuwa tunahitaji kiongozi mzalendo, mwadilifu, mwenye maono shirikishi na utashi wa kisiasa ili kuweka mifumo imara na siyo kiongozi imara anaeweka mifumo anayoamini yeye kwa ajili ya kufanikisha malengo binafsi na washirika wake.

Waziri wa zamani wa Uibgereza Sir Winston Churchill aliwahi kusema:
"Good politician are those who plan for the best interest of the future generations,but poor politicians plan for best interest of the future elections."

Akimaanisha kuwa wanasiasa makini hupanga mipango ya nchi kwa maslahi mapana ya vizazi vijavyo.Ila wana siasa dhalimu hupanga mipango ya nchi kwa kuangalia maslahi mapana ya chaguzi zijazo.
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
10,892
2,000
Mfumo Imara katika nchi ni mfumo wenye "Checks and Balances" ambazo zinazuia mtu mmoja mwenye mamlaka kufanya anavyojisikia yeye tu badala ya vile katiba, sheria na miongozo ya nchi inavyoelekeza. Lakini pia ni mfumo ambao unahakikisha kuwajibika kwa kiongozi endapo ataweza kuwa kichwa ngumu au jiwe kuzivuka checks and balances zinazopaswa kumdhibiti.

Mfano wa Mfumo imara ni USA. Trump alishindwa uchaguzi na akatumia njia zote za kisheria na zisizo za kisheria kuendelea kubaki madarakani ila mfumo wao wenye Checks na Balances zinazolipa Bunge , Mahakama na Jeshi uhuru uliweza kuzuia uhuni wake na mfumo huo ukahakikisha anaondoka madarakani japo alikuwa ndiye mtu mwenye nguvu zaidi duniani kwa kipindi hiko.

Usije ukauliza "Checks and Balances" ni nini.
Nenda katafute mwenyewe au Tafuta mwanafunzi wa kidato cha nne anayelewa Civics vizuri akufafanulie maana ya hayo maneno.
Ni maneno matamu tu ya siasa,tafasiri yake ukiuliza wanayoisema, unaweza ukatukanwa
 

MrFroasty

JF-Expert Member
Jun 23, 2009
1,040
1,500
Siku kadhaa na hasa miaka kadhaa iliyopita, nilianza kusikia habari za 'mfumo imara' kuwa ndiyo unaofaa zaidi kuliko 'kiongozi imara'.
Mwanzoni sikutilia maanani. Lakini, siku za hivi karibuni hili fungu la maneno la 'mfumo imara' limejizolea sifa ya kutajwa mara kwa mara kwenye mitandao mingi ya kijamii; hata humu jamvini (www.jamiiforums.com), fungu hili la maneno limejizolea sifa hizo hizo...
Nimesoma machapisho mawili ya mwanzo nimeona wengi wamekimbilia kwenye siasa. Mfumo imara nadhani kwa kiengereza manaake ni strong institution (taasisi imara). Labda kifo cha Magufuli kinaweza kuwa somo tosha (najaalia kama alifanya kazi kubwa ya kupambana na rushwa, discipline ya watumishi n.k).

Kwa kutumia mfano huu (Magufuli kama kiongozi imara), sasa kafariki inamaana tumeumia vibaya. Lakini tungelikuwa na taasisi imara, basi athari ya kuondoka kwake ingekuwa ni ndogo.

Hili neno lina mahusiano na mfumo wa kuendesha nchi uliopo Tanzania, ambapo raisi ana mamlaka makubwa kuliko wafalme wa ghuba za kiarabu!

Ukimuona mtu anashangiria mfumo tulionao kama ulivyo, basi ujue anapigia chapuo tumbo lake. Kwa maendeleo ya taifa lazima tubadilishe kutoka mfumo tulionao na kupunguza madaraka ya wanasiasa akiwamo raisi na kuunda taasisi zenye kujitegemea na kufanya kazi zake bila ya kuingiliwa na hawa watu.

Mahakama, serekali za mitaa, tume ya uchaguzi n.k. Hizi zote zina mikono ya wanasiasa wakati, kiilivyo zinatakiwa zifanyiwe mabadiliko ya jinsi gani zinapatikana na uendeshwaji wake. Kwa mfumo uliopo sasa mie mmoja sidhani kama mabadiliko ya kimaendeleo tunayotaka baadhi yetu yatapatikana. Wanasiasa ambao wengi wao wana uwezo mdogo wamekuwa wakiburuza kila kitu kwa maslahi binafsi.
 

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
905
1,000
Unajichanganya, huwezi kusema mfumo unawekwa na mtu kama ulivyotumia mfano wa Magufuli, mfumo imara unawekwa na sheria itakayotoa miongozo ya hao watakaokuwa wanaongoza hizo taasisi waweze kuziendesha bila kuingiliwa na yeyote wakitimiza majukumu yao, na hivyo hivyo wakiharibu washtakiwe bila kuangalia wao ni wakina nani toka chama gani...
Si kuna sheria ya kodi? Mbona watu wanakwepa kodi kama unafikiri maana ya mfumo ni sheria?

Sheria bila uwepo wa watu makini wa kuhakikisha sheria ifuatwe sheria itabaki kuwa maandishi kwenye karatasi. Kinyume chake unaweza kuwa na kiongozi imara akaweka taratibu zake na baada ya muda wa kutosha hizo taratibu zinageuka utamaduni wa watu.
 

kabyemela95

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
791
1,000
M
Mfumo Imara katika nchi ni mfumo wenye "Checks and Balances" ambazo zinazuia mtu mmoja mwenye mamlaka kufanya anavyojisikia yeye tu badala ya vile katiba, sheria na miongozo ya nchi inavyoelekeza. Lakini pia ni mfumo ambao unahakikisha kuwajibika kwa kiongozi endapo ataweza kuwa kichwa ngumu au jiwe kuzivuka checks and balances zinazopaswa kumdhibiti....
Mfumo upo tena mzuri,Tanzania kuna mamlaka za kudhibiti kila kitu, bodi za kila aina ya kitu, mahakama zinazosikiliza kila aina ya kosa,serikali iliyojaa wizara ya kila sekta...tulichokosa ni uadilifu tu, kila mtu angesimamia kazi yake kwa usahihi na bila kuogopana ,tungekua mbali...Kwahiyo unavoniambia hakuna mfumo sikuelewi, sema kuna watu dhaifu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom