Majibu niliyopewa Wiki Mbili na Leo pia na Mtabibu wa zamu juu ya Mpwa wangu yamenichanganya naombeni Msaada wa Kuyaelewa tafadhali

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,734
Alilazwa Wiki Mbili zilizopita All - Rounder nikaambiwa kuwa Mpwa wangu HE IS IN COMA hivyo nitulie tu Wahangaike nae waweze kuona kama wataokoa Maisha yake japo Daktari Mmoja aliniuma Sikio na kuniambia nijiandae Kisaikolojia kwa lolote lile.

Leo muda mfupi tu nimetoka Kumtizama Mpwa wangu huyo na All - Rounder nimeambiwa kuwa HE IS STABLE BUT IN CRITICAL CONDITION hivyo nimeshindwa kabisa Kuyaelewa Kitabibu haya maneno mawili.

Na nakumbuka hata wakati nawaaga Matabibu kuna Mmoja akaja Kunisisitiza kuwa hata ikitokea Mpwa wangu akarejea katika hali yake ya kawaida sitakiwi Kumuongelesha sana, hatakiwi Kuongea mno, hapaswi kuonana hovyo na Watu.

Lakini pia atahitaji angalau mwaka Mmoja au hata Miwili ili aweze Kujitambua hasa hivyo nikiweza niende tu Ofisini Kwake nikawaambie kuwa hawezi kufanya Kazi na kama huko Ofisini alikokuwa Boss kuna Kaimu (Naibu) wake basi ashike tu Hatamu ili Utendaji wa Ofisi uendelee na Ufanisi upatikanaji.

Kifupi nimechanganyikiwa ndiyo maana nimeona niwashirikishe nanyi mnielimishe zaidi japo kuna Mpwa wangu mwingine alienda Kumsabahi mchana huu kaniambia kuwa Mpwa aliweza Kuamka na hata Kuomba Simu atume Salamu Kwetu ila nimemkatalia kwani kwa hali aliyonayo Mpwa wangu si wa Kuongea au hata Kupiga Simu au Kutuma Meseji.
 
wewe nakujua,Jana situlikuwa hosptl acha kumchulia ndg yako,mkeo alitaka amletee chakula ww ukamkatalia,kisa dogo ana asset za kutosha na yuko peke yake.acha roho mbaya,tafuta vya kwako.
 
Stable but in Critical condition alimaanishaa mgonjwa hali yake imehimarika lakini sio ya Uhakika means muda wowote unaweza kubadilika. Mliambiwa anaugua nini mpaka now anaweza Kupiga simu but hatakiwi kufanya interaction yoyote??? Kama alipata mshtuko then stroke means Dr anaogopa akipata tena mshtuko inaweza kuwa for Good.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Sasa Mkuu kinachokuchanganya ni kipi hapo? Au una wasiwasi kuwa Mpwa wako atakujakuwa tegemezi kwako kwa kuwa hatojiweza tena kwa miaka ijayo?

Mwache Mpwa apumzike bado mgonjwa.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom