Katika ziara ya Rais wa Zambia nchini Tanzania, Mh Hakainde Hichilema July 2, 2022, yeye na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania walikubaliana kufufua ujenzi wa reli ya kihistoria ya TAZARA kwa kiwango cha ‘Standard Gauge Railway’ (SGR). Reli ya TAZARA ina urefu wa kilomita 1,860...