Wazazi wanafaidika kitu Gani wanapovunja ndoa za Watoto wao?

Shift

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
1,078
2,148
Katika pitapita zangu kwa maeneo tofauti niliwahi kukutana na hii shutuma kuwa Wazazi wamekua chanzo kikubwa Cha ndoa za Watoto wao kuvunjika.

1. Je sababu zinaweza kuwa Nini?
2. Je kama mnapendana kwa dhati 3.Wazazi wanaweza kuwa na nafasi?
4. Nini nafasi ya maandiko matakatifu kuhusu Ndoa?
5. Nini kesho ya Watoto?
6. Ninja kinaweza kufanyika kuepusha laana hii?
 
Mzazi mtoto wako akishakua mkubwa fanya kushauri tu, wazazi wengi wanapenda kuingilia na kuweka sheria zao kwenye miji ya watoto wao. Mimi tokea nakua sijawai kumiliki baiskeli zaidi ya kudoea kwa majirani mtoto wangu mdogo nimemnunulia baiskeli mzee Anashangaa na kusema natumia hela hovyo tena kwa hasira utadhani nakaa kwake.
 
. Nini nafasi ya maandiko matakatifu kuhusu Ndoa?
Tulia Sheikh nikupe Aya....hizi hata Bujibuji Simba Nyamaume hazijui.

Wakolosai 3:18-19 BHN

Enyi wake, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana. Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao.

Mwa 2:24 SUV

Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Waefeso 5:24 “Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo”

28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.

33 Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe”

Kila mtu mmoja-mmoja kati yenu na ampende hivyo mke wake kama vile anavyojipenda mwenyewe; . . . mke anapaswa kumheshimu sana mume wake.”—EFE. 5:33.

“Kile ambacho Mungu ameunganisha mtu yeyote asikitenganishe.” (Mt. 19:3-6; Mwa. 2:
Tuma sadaka yangu sasa
 
Mzazi mtoto wako akishakua mkubwa fanya kushauri tu, wazazi wengi wanapenda kuingilia na kuweka sheria zao kwenye miji ya watoto wao. Mimi tokea nakua sijawai kumiliki baiskeli zaidi ya kudoea kwa majirani mtoto wangu mdogo nimemnunulia baiskeli mzee Anashangaa na kusema natumia hela hovyo tena kwa hasira utadhani nakaa kwake.
Wazazi wa mwendokasi ni shida sana, kweli umesema ukweli mchungu, OMBA YASIKUKUTE
 
Mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.

Hata kama Kuna mashinikizo Makali ya Wazazi ili ndoa yenu ivunjike, ukiwa na mke mwenye hekima atavikwepa vikwazo vyote na chombo chenu kitafika salama.

Mimi na Kasie hatuachani Ng'oo

Wee Bujii...!

Unamjua Babu Asprin vizuri....!!!

He is my Big Sam Originale and I luuuuv him 😍.
 
Wazazi nadhani bado wanashauri,,,ila watoto kutokana na kutokuwa na AKILI ndio hufanya ule ushauri kama ndio maamuzi,,,,Kuna Dada mtoto wake alikuwa anasumbuliwa na ile ya kushtuka(mtaani huita Degedege),, sasa Mzazi wa Bwana yake alishauri mtoto apewe majani fulani hivi,,,ila Mama mkwe ni mlokole yeye alikataa....

Basi hilo lilileta ugomvi sana kwa wale Wapenzi,,,kila mtu aliamini alichosema mzazi wake ni sahihi,,,,,Wao wawili walishindwa kuchanganya na akili zao,,,,,Hasa MWANAUME....

so nadhani wanaoharibu NDOA ni wanandoa wenyewe,,,,,ila ni vile Binadamu lazima atafute wa kumtupia Lawama na wazazi ndio huangukia hapo....

But WAZAZI pia sometimes inahitaji uwe na Msimamo haswa ili uende nao sawa....
 
Back
Top Bottom