Tanzania itapata faida gani kama TAZARA itajengwa kwa kiwango cha SGR?

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Apr 26, 2022
259
353
Katika ziara ya Rais wa Zambia nchini Tanzania, Mh Hakainde Hichilema July 2, 2022, yeye na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania walikubaliana kufufua ujenzi wa reli ya kihistoria ya TAZARA kwa kiwango cha ‘Standard Gauge Railway’ (SGR). Reli ya TAZARA ina urefu wa kilomita 1,860.

Binafsi nina mtazamo na maono chanya sana kuhusu uamuzi wa serikali hizi mbili kujenga reli hii. Mimi kama Mtanzania, naiona reli hii kama fursa kubwa katika kuchochea maendeleo katika sekta zifutatazo nchini, nazo ni, usafirishaji, kilimo, utalii pamoja na sekta ya bandari.

KILIMO
Kupita bajeti ya Wizara ya Kilimo 2022/23 Serikali imeazimia kujenga viwanda vikubwa vitatu vya kuchakatia nafaka mbalimbali nchini. Viwanda hivyo vitajengwa Mbeya, Dar es Salaam na Mwanza. Mbeya ni eneo ambao reli ya TAZARA imepita, hii ni fursa kwa Tanzania kwani itaweza kusafirisha bidhaa kwa shehena kubwa zaidi kupitia reli kwenda katika mikoa mingine na nchi jirani, hivyo kuliongezea taifa mapato. Usafirishaji kwa reli hubeba shehena kubwa zaidi kuliko usafirishaji wa mabasi.

Viwanda cha Chunya-Mbeya ambacho kazi yake ni kukoboa mpunga, kitanufaika sana kutokana na urahisi wa usafiri wa bidhaa hiyo kwenda nje ya nchi, na pia mikoa ya jirani.

Kupita reli hii, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kupunguza bei za usafirishaji hivyo kuimarisha kilimo pembezoni na katika mikoa/sehemu zinayopitiwa na reli kama Iringa, Mbeya, Tunduma, Makambako ambako kote huku, bidhaa zinaweza kusafishwa kwa muda mfupi na kwa wingi zaidi hivyo kuliongezea taifa mapato maradufu zaidi.

Reli hii inaweza kutumika kusafirisha shehena za mbolea kwa wakulima ndani ya muda mfupi, kwa urahisi na kwa gharama nafuu zaidi.

UTALII
Sekta ya Utalii inakuwa kwa kasi sana chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Hii hasa ukizingatia na kufunguliwa kwa mipaka ya nchi nyingi baada ya kupungua kwa janga la UVIKO-19 duniani.

Reli hii itatumika kusafirisha watalii kwenda Udzungwa, Selous na Mikumi kwa Urahisi zaidi na kupunguza gharama za usafiri hasa kwa watalii. Usafiri wa treni hutoa burudani ya tofauti na fursa ya kipekee ya kuona vivutio vingi kwa kutokana na uhalisia kwamba reli imekatiza katika maeneo mbalimbali yenye mabonde yenye maporomoko yakuvutia, milima, mabonde pamoja na mapori mazuri.

USAFIRISHAJI
Abiria waendao mikoa ya Mbeya, Morogoro, Iringa na kadhalika watapata mbadala wa usafiri kutokana na usafiri unaotumika sasa kwa sasa ni mabasi tu. Kutumia treni kama njia kuu ya usafirishaji kutapunguza muda idadi ya magari barabarani hivyo kupunguza uharibifu wa barabara na kuzifanya zidumu muda mrefu zaidi.

BANDARI
TAZARA haitohudumia Tanzania na Zambia pekee, kuna mataifa kama Malawi, Zimbabwe na kadhalika ambayo yanaweza kupitisha mizigo yao kupitia bandari ya Dar es Salaam na shehena za mizigo hiyo kusafirishwa kwa reli ya TAZARA kuelekea nchi hizo. Haina maana reli inafika hadi kwenye hizo, ila ni rahisi shehena hizo kusafirishwa kwa reli hadi Zambia, kisha kufaulishwa na kupelekwa kwenye mataifa hayo. Hii italiingizia taifa mapato yakutosha na kuimarisha sekta ya Bandari nchini.

Itoshe tu kusema kwamba hakuna wakati ambao tunamuhitaji sana Rais Samia Suluhu kama wakati huu. Hakika haya ni maono ambayo pengine, tuliyahitaji miaka 10 nyuma, lakini Mungu alitupima subira zetu kwa wakati wote huo, akijua kwamba wakati sahihi utafika, na wakati wenye ndio huu, chini ya Mama, Rais Samia Suluhu Hassan.
 
Naungana nawe mkuu, nchi yetu tunahitaji tuchukue mizigo ya DRC even for 45%,tutatengeneza fedha nyingi mno, DRC (the future economic giant ya Africa)mizigo yake mingi inakwenda Walvis bay, Durban ambako ni mbali sana, inatakiwa ije Dar
 
Wanajenga tazara kua sgr ya nini wakati hawataki kuitumia?

Wataalam wanafuatizia mawazo ya wanasiasa hawajui kwamba hiyo cape gauge ya tazara ilichaguliwa ili kuingiliana na mtandao wa reli za afrika ya kusini?

Reli ya tazara inaingiliana na afrika ya kusini, congo angola, zimbabwe, zambia, botswana, na mozambique. Ndio maana tunaona safari za treni ya tazara zikitokea afrika kusini hadi dar.

Mwaka jana au juzi kulikua na safari ya kitalii kutoka dar hadi benguela angola.

Ubinafsi na ufisadi umefanya tushindwe kuendesha tazara kwa faida na kusaidia uchumi wa nchi zetu mbili.

Itakua ujinga kuingia mradi kufanya tazara sgr bila nchi zote za sadc kukubali mradi huo.

Reli ya tazara inafanya vibaya kutokana na ujinga na ubinafsi wa viongozi wa tanzania na zambia. Wanachofikiria ni matumbo yao.

Wanafikiria malori yao na washikaji wao. Hawajali uhai wa barabara ambazo zinagharamiwa ujenzi na umma.
 
Katika ziara ya Rais wa Zambia nchini Tanzania, Mh Hakainde Hichilema July 2, 2022, yeye na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania walikubaliana kufufua ujenzi wa reli ya kihistoria ya TAZARA kwa kiwango cha ‘Standard Gauge Railway’ (SGR). Reli ya TAZARA ina urefu wa kilomita 1,860.

Binafsi nina mtazamo na maono chanya sana kuhusu uamuzi wa serikali hizi mbili kujenga reli hii. Mimi kama Mtanzania, naiona reli hii kama fursa kubwa katika kuchochea maendeleo katika sekta zifutatazo nchini, nazo ni, usafirishaji, kilimo, utalii pamoja na sekta ya bandari.

KILIMO
Kupita bajeti ya Wizara ya Kilimo 2022/23 Serikali imeazimia kujenga viwanda vikubwa vitatu vya kuchakatia nafaka mbalimbali nchini. Viwanda hivyo vitajengwa Mbeya, Dar es Salaam na Mwanza. Mbeya ni eneo ambao reli ya TAZARA imepita, hii ni fursa kwa Tanzania kwani itaweza kusafirisha bidhaa kwa shehena kubwa zaidi kupitia reli kwenda katika mikoa mingine na nchi jirani, hivyo kuliongezea taifa mapato. Usafirishaji kwa reli hubeba shehena kubwa zaidi kuliko usafirishaji wa mabasi.

Viwanda cha Chunya-Mbeya ambacho kazi yake ni kukoboa mpunga, kitanufaika sana kutokana na urahisi wa usafiri wa bidhaa hiyo kwenda nje ya nchi, na pia mikoa ya jirani.

Kupita reli hii, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kupunguza bei za usafirishaji hivyo kuimarisha kilimo pembezoni na katika mikoa/sehemu zinayopitiwa na reli kama Iringa, Mbeya, Tunduma, Makambako ambako kote huku, bidhaa zinaweza kusafishwa kwa muda mfupi na kwa wingi zaidi hivyo kuliongezea taifa mapato maradufu zaidi.

Reli hii inaweza kutumika kusafirisha shehena za mbolea kwa wakulima ndani ya muda mfupi, kwa urahisi na kwa gharama nafuu zaidi.

UTALII
Sekta ya Utalii inakuwa kwa kasi sana chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Hii hasa ukizingatia na kufunguliwa kwa mipaka ya nchi nyingi baada ya kupungua kwa janga la UVIKO-19 duniani.

Reli hii itatumika kusafirisha watalii kwenda Udzungwa, Selous na Mikumi kwa Urahisi zaidi na kupunguza gharama za usafiri hasa kwa watalii. Usafiri wa treni hutoa burudani ya tofauti na fursa ya kipekee ya kuona vivutio vingi kwa kutokana na uhalisia kwamba reli imekatiza katika maeneo mbalimbali yenye mabonde yenye maporomoko yakuvutia, milima, mabonde pamoja na mapori mazuri.

USAFIRISHAJI
Abiria waendao mikoa ya Mbeya, Morogoro, Iringa na kadhalika watapata mbadala wa usafiri kutokana na usafiri unaotumika sasa kwa sasa ni mabasi tu. Kutumia treni kama njia kuu ya usafirishaji kutapunguza muda idadi ya magari barabarani hivyo kupunguza uharibifu wa barabara na kuzifanya zidumu muda mrefu zaidi.

BANDARI
TAZARA haitohudumia Tanzania na Zambia pekee, kuna mataifa kama Malawi, Zimbabwe na kadhalika ambayo yanaweza kupitisha mizigo yao kupitia bandari ya Dar es Salaam na shehena za mizigo hiyo kusafirishwa kwa reli ya TAZARA kuelekea nchi hizo. Haina maana reli inafika hadi kwenye hizo, ila ni rahisi shehena hizo kusafirishwa kwa reli hadi Zambia, kisha kufaulishwa na kupelekwa kwenye mataifa hayo. Hii italiingizia taifa mapato yakutosha na kuimarisha sekta ya Bandari nchini.

Itoshe tu kusema kwamba hakuna wakati ambao tunamuhitaji sana Rais Samia Suluhu kama wakati huu. Hakika haya ni maono ambayo pengine, tuliyahitaji miaka 10 nyuma, lakini Mungu alitupima subira zetu kwa wakati wote huo, akijua kwamba wakati sahihi utafika, na wakati wenye ndio huu, chini ya Mama, Rais Samia Suluhu Hassan.
Na hii itakuwa dawa ya kutokuwa na double lanes Kati ya Dar hadi tunduma
 
Umesahau kutueleza reli iliyopo ilishindwaje kutimiza uliyoyataja.
 
Tuache ujinga wa kutumia Matilioni ya pesa kuwekeza kwenye reli harafu hatujaandaa uchumi wa kufanya reli zirudishe pesa badala yake tunabet kwa Nchi jirani..

Wakoloni walipojenga reli hawakutegemea Nchi jirani bali uchumi wao.

Ndio maana nawapongeza hata Kenya maana 80% ya mzigo unaopita bandari zao na kusafirishwa na reli zao unatumika ndani ya Nchi..

Huku Tanzania eti tunabeti kwa Nchi jirani,reli haichipuzi uchumi bali inuja kusaidia uchumi ulio tayari..

Kama hatujaandaa uchumi basi hakuna Sababu za kujenga hiyo reli iwe pambo kama inayojengwa sasa.
 
CCM inachekesha sana - kujenga viwanda vya kuchakata nafaka mbalimbali! Kilichopelekea waiue NMC ambayo ilikua chini ya umiliki wa serikali kwa 100% na hatimaye "kuibinafsisha" na leo wanarudi kulekule ni nini? Please, stop these nonsenses Getrude Mollel .
 
Kwenye utiaji saini mkataba na uwekaji jiwe la msingi tupo vizuri sana
 
Back
Top Bottom