chanjo

Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.

Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini.

Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.

Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio, pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili

Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba.
  1. Mstahiki Mea

    JamiiForums Tanzania Watanzania tuache uzushi dhidi ya chanjo ya COVID -19, Je mchango wetu ni upi katika kukabiliana na hili janga?

    Mlipuko virusi vya korona mwishoni mwa mwaka 2019 umebadili kabisa mifumo ya maisha duniani. Ugonjwa huu umesabababisha athari kubwa sana katika kila sekta pamoja na kugharimu maisha ya watu. Nikutokana na athari hizo ndiposa wataalamu wengi wamekuwa wakisumbua vichwa kutafuta suluhisho ili...
  2. Matanga

    JamiiForums Tanzania Serikali moja ya Dunia na chanjo ya COVID-19

    TAARIFA KWA UMMA wa na [emoji1621][emoji1241]Dr Lugendo Karibuni, SERIKALI MOJA YA DUNIA NA CHANJO YA COVID-19 Hii ni mada ndogo iliyo katika MADA kubwa isemayo “ KUNA NINI NYUMA YA CORONA ?” ndiyo tunayoendelea nayo. Hebu tutazame kidogo yanayoendelea ulimwenguni. Huko Marekani: “Juni 23...
  3. 6WaS9

    JamiiForums Tanzania Changamoto za safari nje ya nchi na covid19 | delta, chanjo, cheti mambo yako vipi?

    Habari, Kufuatia wimbi jingine la ugonjwa huu na maambukizi mapya ya covid19 delta. Baadhi ya Nchi zimeingia kwenye travelling ban , mfano nchi kadhaa zimeiban India , Kenya na nyinginezo kusafiri... Karibu uwasilishe changamoto zozote ulizokutana nazo hivi karibuni kama ulisafari kutoka tz...
  4. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania WHO: Nchi tajiri zinapaswa kugawa chanjo kwa nchi maskini

    Maafisa wa Shirika la Afya Duniani WHO wamesema hakuna ushahidi wa kutosha unaonyesha kwamba watu wanahitaji kuchomwa sindano ya tatu ya chanjo dhidi ya virusi vya corona, na hivyo kutoa wito wa chanjo zilizobakia kupewa mataifa maskini ambayo bado hayakuchanja raia wake, badala ya kutumiwa na...
  5. Erythrocyte

    JamiiForums Tanzania Watanzania waanza kujiachia na Chanjo ya COVID 19 kwenye nchi za watu

    Aliyekuwa Mgombea Urais wa TFF Aliyeenguliwa kwa fitna , Oscar Oscar na Rafiki yake ambaye sikumtambua jina lake wametangaza hadharani kwamba wamepata chanjo ya corona nchini Marekani, watu hao wawili ni raia wa Tanzania nchi ambayo miezi michache iliyopita iliamini kwamba virusi vya corona...
  6. J

    JamiiForums Tanzania Dkt. Mwigulu: Chanjo ya Corona itakayotumika Tanzania itakuwa sawa na ile inayotumika Marekani

    Waziri wa fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kipaumbele namba moja cha Rais Samia ni afya za Watanzania hivyo chanjo ya Corona itayotumika Tanzania itakuwa sawa na ile iliyoidhinishwa na Ikulu ya Marekani kwa ajili ya kuwachanja Wamarekani. Chanzo: ITV habari Nawasalimu kwa jina la JMT!
  7. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania Zanzibar: Serikali yaanza kutoa chanjo ya COVID-19 kwa wahudumu wa Afya

    Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Zanzibar Ahmed Mazrui amesema wameanza kutoa chanjo ya COVID-19 kwa wahudumu wa Afya wa hospitali za serikali, Uwanja wa Ndege wa Abeid Karume na Bandari ya Malindi. Wamechukua hatua hiyo kwa kuwa nchi kadhaa za Afrika zimeonesha...
  8. funaku

    JamiiForums Tanzania Cuba yatoa ruhusa kutumia chanjo ya Covid-19 iliyotengenezwa nchini humo

    Hatimaye mamlaka ya udhibiti wa dawa nchini Cuba imetoa ruhusa ya dharura kwa matumizi ya Chanjo iliyozalishwa locally nchini Cuba. Hongera kwa kujitambua CUBA! ===== Cuba begins mass Covid-19 vaccine inoculation before concluding trials Carmen Sesin Cuba began the mass inoculation of...
  9. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania Boris Jonson: Sheria za kuvaa barakoa na kukaa mbali hazitakuwa lazima Uingereza

    Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Jonson amesema kuwa yeye ataendelea kuvaa barakoa katika maeneo ya watu wengiImage caption: Waziri Mkuu Boris Jonson amesema kuwa yeye ataendelea kuvaa barakoa katika maeneo ya watu wengi. Waziri mkuu, Boris Johnson, alisema alitarajia kupunguza sheria za Covid...
  10. Sam Gidori

    JamiiForums Tanzania Takwimu: Mwenendo wa Chanjo ya COVID-19 barani Afrika - Julai 2021

    Baada ya kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona duniani mwanzoni mwa mwaka jana, dunia ilianza kutafuta chanjo, na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka, kampuni kubwa tano za Pfizer-BioNTech, Moderna, AstraZeneca na Johnson & Johnson zilikuwa zimetengeneza chanjo za kukabiliana na ugonjwa huo...
  11. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania Tanzania kujenga kiwanda cha kuzalisha chanjo ya Covid-19

    Serikali imeanza mchakato wa kutengeneza chanjo ya Virusi vya Corona hapa nchini ili kupunguza gharama ya kuagiza nje ya nchi na kuzifanya ziwe karibu na wananchi. Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dodoma Katibu Mkuu, Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Afya Prof. Abel Makubi amesema...
  12. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania Wizara ya Afya: Mchakato wa chanjo umekamilika, itatolewa bure

    SERIKALI imetangaza kuwa tayari mchakato wa kuingiza na kutoa chanjo ya ugonjwa COVID-19 (Corona) umekamilika huku ikisisitiza tahadhari zaidi ziendelee kuchukuliwa na wananchi. Kauli hiyo imetolewa leo Julai 4,2021 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee...
  13. FRANCIS DA DON

    JamiiForums Tanzania Tetesi: Chanjo za Corona unatikiwa uchanjwe ‘Booster’ mara 3 ndio uwe na kinga, na si mara 2 kama tulivyoambiwa awali?

    Je, ni kweli kwamba baada ya kufanya majaribio kwa watu waligundua kwamba mtu anatakiwa achanjwe mara 2 ndio awe na kinga tosha, ila baada ya utafiti sasa wamebadilika tena, wanasema unatakiwa uchanjwe mara 3 ndio uwe na kinga? Kwahiyo ile kauli ya hayati kwamba tusubiri kwanza ilikuwa na mashiko?
  14. Cannabis

    JamiiForums Tanzania Wizara ya Afya Zanzibar yataja siku za utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu

  15. J

    JamiiForums Tanzania Yajue magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kwa watoto (Sehemu ya Kwanza)

    Kifua kikuu ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya bakteria na huenezwa kwa njia ya hewa. Mtu mwenye maambukizi ya kifua kikuu akikohoa, kupiga chafya au kutema mate ovyo husambaza vijidudu hivyo hewani na huweza kumwambukiza mtu mwingine. Ugonjwa huu unakingwa kwa chanjo ya kifua kikuu...
  16. Sam Gidori

    JamiiForums Tanzania, JamiiForums Uganda Watu 800 wachomwa chanjo feki ya Corona

    Polisi nchini Uganda inawashikilia wahudumu wawili wa afya kwa madai ya kuhusika kuwachoma takriban watu 800 chanjo feki za corona mwezi uliopita. Mtu mmoja, ambaye ni daktari, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika kuwachoma watu hao chanjo katika mji wa Kampala kati ya Mei 15 na Juni 17...
  17. beth

    JamiiForums Tanzania Upungufu wa Chanjo wapelekea Serikali ya Namibia kusitisha utoaji wa dozi ya pili

    Nchi hiyo imeacha kutoa Dozi ya pili ya Chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19 ili kutoa kipaumbele kwa wale ambao bado hawajapata Dozi ya kwanza. Kutokana na upungufu, Serikali imesema itagawa Chanjo zilizobaki katika maeneo ambayo yameripoti ongezeko la maambukizi na vifo, na ambao wanasubiri...
  18. Mzee Mwanakijiji

    JamiiForums Tanzania Wazo: Tanzania Ishirikiane na Cuba kwenye Suala la Chanjo

    Mojawapo ya mijadala mikubwa si kwa Tanzania tu bali hata nchi nyingine ni suala hili la chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19. Nchi mbalimbali zimejaribu na zile tajiri zimefanikiwa kwa haraka kujitengenezea chanjo zao na kujinufaisha wao wenyewe kwanza kabla ya wengine. Cuba ni miongoni mwa nchi...
  19. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania Kuchanganya chanjo za COVID-19 kunaongeza ufanisi

    Njia ya kuchanganya chanjo za Covid -19 kwa kutumia chapa mbalimbali za chanjo ya Covid kwa dozi ya kwanza na ya pili - inatoa kinga nzuri dhidi ya virusi vya janga hilo, utafiti wa Uingereza umebaini. Majaribio yalitazama ufanisi wa dozi mbili za Pfizer, AstraZeneca na Mchanganyiko wote...
  20. N

    JamiiForums Tanzania Chanjo ya COVID-19: Hivi wataalam hamjui ukweli au mmeamua kumpotosha Rais?

    Habari ndugu wanaJF, Jana kwenye mkutano wa rais na wanahabari nilimsikia akiongea confidently kuhusu kuagiza na kuanza kutumia chanjo za covid. Ieleweke kwamba hizo chanjo zilitolewa kwa dharura bila conclusive data za kitafiti na baadhi ya madhara ya muda mfupi yaliyokwishatokea ni kuganda...
Back
Top Bottom