Chanjo ya COVID-19: Hivi wataalam hamjui ukweli au mmeamua kumpotosha Rais?

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
13,405
19,075
Habari ndugu wanaJF,

Jana kwenye mkutano wa rais na wanahabari nilimsikia akiongea confidently kuhusu kuagiza na kuanza kutumia chanjo za covid. Ieleweke kwamba hizo chanjo zilitolewa kwa dharura bila conclusive data za kitafiti na baadhi ya madhara ya muda mfupi yaliyokwishatokea ni kuganda kwa damu (blood clots), kushuka kwa kiwango cha chembechembe nyeupe za damu zinazohusika na kuganda kwa damu 'platelets' na kusababisha tatizo linalojulikana kitaalamu kama 'thrombocytopenia' matatizo ya mzio 'autoimmunity' ambapo chembe chembe za kinga zinashambulia viungo vya mwili na hii ikitokea kwenye viungo muhimu kama figo, ini na ubongo inaweza kupelekea vishindwe kabisa kufanya kazi 'organ failure'.

Hivi karibuni shirika la kuthibiti magonjwa la marekani CDC limeripoti kuongezeka kwa cases zinazoonyesha athari kwenye misuli ya moyo 'myocarditis' na hata kwenye kiwambo kinachozunguka moyo 'pericarditis' kwa vijana na watoto waliochanjwa chanjo ya korona inayotumia teknolojia ya mRNA.

Pia, uchambuzi wa kitaalamu uliotolewa hivi karibuni umeonyesha ndani ya masaa 48 kibebeo cha chanjo inapodungwa mwilini 'lipid nanoparticles' kimeonekana hasa kwenye vifuko vya mayai kwa wanawake 'ovaries' na kwenye uboho wa mifupa 'bone marrow' jambo ambalo siyo la kawaida na linaweza kusababisha shida za uzazi kwa akina mama na matatizo ya kansa za damu 'leukemias' 'lymphomas' na ukizingatia hizi shida za kansa, madhara ya uzazi na hata mzio 'autoimmunity' zinaweza kuchukua muda mrefu hata miaka zaidi ya mitatu kudhihirika.

Je, wataalamu wamemshauri rais kwa kuzingatia utaalamu na up-to-date information zinazotolewa kuhusu madhara ya hizo chanjo? au wameamua tu kutoa ushauri unaoendeshwa na upepo wa ngoma inavyochezwa huko duniani kuhusiana na huu ugonjwa wa covid.

Mimi ningeshauri zitumike zaidi njia za kujikinga badala ya kuhimiza kampeni za chanjo ambayo ipo kwenye utafiti, kwa sababu ukishachanja hakuna namna ya kuondoa hiyo chanjo mwilini, kinachobaki inakuwa ni kupambana na madhara yanayoweza kutokea ndani ya muda mfupi, muda wa kati au muda mrefu.

Nawasilisha.​
 
Umesikiwa. Una kila haki ya kukataa chanjo ili mradi usituzuie sisi ambao tunaitaka kupata.

Btw, hayo yote ulioyasema yamezungumzwa sana na majibu yake yapo humo humo ulipoyatoa. Rais amesema kama unaamini nyungu ruksa, kama hautaki ruksa na kama unataka ni ruksa.

Akili mukichwa.

Amandla...
 
Marais waliopata chanjo msisanganyike kuwa ile ni chanjo, ni danganya toto mbele ta camera ili watu waamini haina madhara.

Hakuna raisi achome haya ma chanjo yasioeleweka.wanachoma dawa nyingine kuhamasisha watu wapate chanjo ili wao watimize mashart waliopewa.
Hujalazimishwa kuchanja,nyie endeleeni kumuenzi dikteta.
 
Chanjo ni hiari , kila dawa ina side effect zake probability ya kuganda damu ukipewa chanjo ni ndogo sana kulinganisha na probability ya kufa ukibanwa mbavu ukipata maambukizi ya corona.

Walioko kwenye makundi hatarishi na watu wengine watakaoamini katika chanjo watajilinda kwa njia hiyo na pia wasiotaka hawatolazimishwa.

Hii ni nchi huru kwa nini mlazimishe tu chanjo isiletwe ?
 
Tusipotezeane muda na hiyo biology yako ya Form VI. Hakuna mtu analazimishwa chanjo. Usiwazuie walio tayari wewe endelea na maisha yako kama Mwendazake. Period

Kila mtu ashinde mechi zake
Kwa majibu kama hayo sijui hata kwanini Mama samia anasema anasubiri wataalamu wamwambie chanjo ipi inafaa? maana hao wanaotaka chanjo wao hata hawajali kuhusu chanjo ipi inafaa wao wanataka kuchanjwa tu ilimradi ni hiari basi wao washakubali kuchanjwa tu.
 
Tusipotezeane muda na hiyo biology yako ya Form VI. Hakuna mtu analazimishwa chanjo. Usiwazuie walio tayari wewe endelea na maisha yako kama Mwendazake. Period

Kila mtu ashinde mechi zake
Ukweli unaweza TOKA hata ktk kinywa cha mwendawazimu sembuse form6, tulieni mkapange foleni mchanjwe mridhishe vichwa vyenu vya panzi
 
Back
Top Bottom