Kwa namna yoyote ile Tanzania ianzishe kiwanda cha chanjo

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Ni muhimu kumuenzi Hayati Dr John Pombe Magufuli kwa kuharakisha mchakato na utekelezaji wa kuanzisha kiwanda cha chanjo.
Third wave ya covid 19 ipo around ni vyema wataalamu wetu waje na mpango wa haraka/ dharura wa kuanzisha kiwanda cha chanjo hasa tukianza na chanjo ya covid 19.


Kwa hisani ya mtu wa Tanzania.
 
Endapo tungefanikiwa kuanzisha vile mia kwa Kila mkoa,hiyo ingekuwa kama kumsukuma mlevi tu,ila kwa sababu longo longo ilikuwa mingi mingi, sie tusubiri miaka mia mbili ijayo tutakuwanauwezo huo.
 
Endapo tungefanikiwa kuanzisha vile mia kwa Kila mkoa,hiyo ingekuwa kama kumsukuma mlevi tu,ila kwa sababu longo longo ilikuwa mingi mingi, sie tusubiri miaka mia mbili ijayo tutakuwanauwezo huo.
Kila mkuu wa mkoa anaendekea na kufanikisha zoezi hilo na litafanikiwa bila shaka
 
Itapingwa sana sana sababu itakuwa haijathibitishwa na WHO, Nadhani umesikia Chanjo ya China Juzi ilivyopigwa Kipapai na Nchi z aMagharibi kuwa haifai ina Sijui toxic nk nk!

Ili Chanjo yetu kama ikianzishwa basi Some Ingridients zitoke Kwao Western! Mi hapo Simo Mkuu!

Nenda Kapambane Mwenyewe hilo

Hio Vita Yake si ya Mchezo!
 
Kuhusu Bandari ya Bagamoyo una maoni gani Mkuu?

Kuna Mada moja Nimeona Umetajwa kuna Jamaa eti anasema anakiri eti alikuwa anadanganywa kuhusu mradi,Na Blaa blaa kibao sasa wakakutaja eti na wewe unaomba Msamaha kwa kuukataa mradi Mwanzoni.

Unasemaje kuhusu Hilo Kaka jingalao
 
Itapingwa sana sana sababu vItakuwa haijathibitishwa na WHO,
Nadhani umesikia Chanjo ya China Juzi ilivyopigwa Kipapai na Nchi z aMagharibi kuwa haifai ina Sijui toxic nk nk!..
Uwezo wa kuanzisha kiwanda hiko tunao by all means necessary.Tuwekeze nguvu huko na tuachane na display za kuvaa barakoa ambazo hata sio N95 ambazo hazikingi dhidi ya corona.
 
Kila mkuu wa mkoa anaendekea na kufanikisha zoezi hilo na litafanikiwa bila shaka
Kujipa faraja ni jambo ,la heri,wakati ule propaganda ziliwezekana kutona na mazingira wezeshi yaliyoandaaliwa na kusimamiwa, udhamini umekoma na uwazi unaonekana ukirejea taratibu. Kwa kuanzi tuhoji watuonyeshe viwanda vipya ndani ya mikoa.
 
Itapingwa sana sana sababuvItakuwa haijathibitishwa na WHO,
Nadhani umesikia Chanjo ya China Juzi ilivyopigwa Kipapai na Nchi z aMagharibi kuwa haifai ina Sijui toxic nk nk!
Ili Chanjo yetu kama ikianzishwa basi Some Ingridients zitoke Kwao Western!
Mi hapo Simo Mkuu!
Nenda Kapambane Mwenyewe hilo
Hio Vita Yake si ya Mchezo!
Hayo mawazo unayotanguliza ndio kushindwa kwetu,bora ukakubali uwezo huo bado hatunao hata hatuhitaji kufikiria mambo makubwa makubwa,zaidi ya kuwaona wenye mawazo kinzani ama yenye maono ndio sababu ya kushindwa kwetu.
 
Itapingwa sana sana sababuvItakuwa haijathibitishwa na WHO, Nadhani umesikia Chanjo ya China Juzi ilivyopigwa Kipapai na Nchi z aMagharibi kuwa haifai ina Sijui toxic nk nk!..
Chanjo yetu kwa ajili yetu, wachina walitaka chanjo yao iingie sokoni ili wapige ela, wazungu hawataki Wachina wapige ela kwa Ugonjwa waliouanzisha wao katika maabara.
 
Kuhusu Bandari ya Bagamoyo una maoni gani Mkuu?
Kuna Mada moja Nimeona Umetajwa kuna Jamaa eti anasema anakiri eti alikuwa anadanganywa kuhusu mradi,Na Blaa blaa kibao sasa wakakutaja eti na wewe unaomba Msamaha kwa kuukataa mradi Mwanzoni
Unasemaje kuhusu Hilo Kaka jingalao
Kuhusu bandari ya bagamoyo ...mimi ni muumini wa kuanzishwa kwa bandari hiyo na sikuanza jana.Ila ni muhimu mkataba uwe na mashiko.

Bagamoyo ndio strategic city toka enzi za mjerumani Dar ikaja kuharibu. Nimeishi na kuvua samaki bagamoyo nimekula uduvi kamba kochi kaa ,kolekole ,pweza,mkizi na changuchangu.

Nimewashwa na ulumba na nimekula kasa, kaa na pia hapo inapotakiwa kujengwa bandari nimesali kwenye msikiti uliopo karibu kabisa. Isitoshe nimeshuhudia sukari ya brazil na madawa ya kulevya yakipitishwa na majahazi kutokea zenji na pia pale mbegani kuna mkondo wa maji baridi unaoleta viboko kutoka sadani na kuingia baharini.

Zaidi nimetengeneza mitego ya ndege wanaitwa membe hapo hapo eneo linapotakiwa kujengwa bandari.hadi mganga wa Timu ya Yanga aliopo hapo eneo la bandari inapotakiwa kujengwa namjua. Itoshe kusema I know the place in and out.

maoni yangu ni kuwa mradi ufanyike lakini atakeyetuingiza cha kike katika mikataba lazima tumnyooshe huko mbeleni.

pia utekelezaji wa mradi utoe kipaumbele cha makusudi kwa wazawa wa bagamoyo na sio kwa sababu wachaga wachache waliowahi kuhodhi maeneo kupitia mikopo ya CRDB ndio wanufaike tu. By the way mimi ni mzanzibari na mbara na nitasema ukweli tupu.

siku nyingine ukiniuliza swali hili ujipange sana na nitafunguka zaidi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Mzee wako alienda pale Muhimbili akajipeleka kwenye lile banda akajishindilia mvuke kumbe ndo anajipeleka kibra hivyo! Ila tuliwaambia mkawa wabishi sana.
 
Nchi zenye msimamo wa kimapinduzi hazikubali chanjo za nchi za nje hasa nchi za magharibi. Ona cuba wamekuja na chanjo yao. Ona urusi ona china. Wote wamekuja na chanjo yao. Chama cha mapinduzi chini ya samia wanatishia usalama sasa. Bora ccm ya samia ibadili jina maana samia inaelekea anatupeleka hatarini kuamini nchi za magharibi za kibeberu.

Huko ulaya na marekani hofu inaonyeshwa kuhusu chanjo na wataalam kwamba watu wanakufa kutokana na chanjo ila hii serikali ya samia wanaonyesha kila dalili kutaka kuingia kichwakichwa. Samia inaelekea hana uwezo wa kuhoji kama magufuli au anampango na ni mshiriki kwenye hizi hila za ubeberu wa covid 19.

Tuwe na chanjo yetu vingine tujikinge kama tulivyofanya kwa mafanikio hadi sasa.
 
Kwani bupiji sauna haifanyi kazi ? No retreat no surrender ndio njia pekee ya kumuenzi tukomae na kujifukizisha achana na hizo habari za chanjo🤣🤸🐒
20210627_212342.jpg
 
Nchi zenye msimamo wa kimapinduzi hazikubali chanjo za nchi za nje hasa nchi za magharibi. Ona cuba wamekuja na chanjo yao. Ona urusi ona china. Wote wamejuja na chanjo yao. Chama cha mapindizi chini ya samia wanatishia usalama sasa. Bora ccm ya samia ibadili jina maana samia inaelekea anatupeleka hatarini kuamini nchi za magharibi za kibeberu. Huko ulaya na marekani hofu inaonyeshwa kuhusu chanjo na wataalam kwamba watu wanakufa kutokana na chanjo ila hii serikali ya samia wanaonyesha kila dalili kutaka kuingia kichwakichwa. Samia inaelekea hana uwezo wa kuhoji kama magufuli au anampango na ni mshiriki kwenye hizi hila za ubeberu wa covid 19.
Tuwe na chanjo yetu vingine tujikimge kama tulivyofanya kwa mafanikio hadi sasa.
Hao wanafanikiwa kwakuwa wanajua nini wanacho kihitaji,nao huwa siasa ni siasa,taaluma ni taaluma,na sayansi ni sayansi na wamewekeza kwa jasho na damu.Sio siye kila kitu siasa tena ile isiyokuwa safi.
 
Hayo mawazo unayotanguliza ndio kushindwa kwetu,bora ukakubali uwezo huo bado hatunao hata hatuhitaji kufikiria mambo makubwa makubwa,zaidi ya kuwaona wenye mawazo kinzani ama yenye maono ndio sababu ya kushindwa kwetu.
Kwani uwezo huo upoje?ni sh ngapi kuanzisha kiwanda hiko?
 
Back
Top Bottom