chanjo

Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.

Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini.

Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.

Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio, pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili

Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba.
  1. B

    Chanjo ni dhidi ya Waafrika? Namba Hazidanganyi!

    Takwimu zilizopo hadi sasa zinaonesha Bara Asia kwa idadi kuchanjwa zaidi wakati Afrika tukivuta mkia. Kwa wastani wa watu kwa bara, Amerika Kaskazini wanaongoza, wakifuatiwa na Ulaya. Sisi kama ilivyo ada tukiendelea kuvuta mkia: Si kuwa Africa wanajivuta bali nchi zilizoendelea kwa...
  2. Erythrocyte

    Zanzibar: Kila Mzanzibar anayetaka Chanjo ya COVID-19 atapata, hakuna mgeni ataingia bila cheti cha Vipimo vya Corona

    Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya wa serikali ya Mapinduzi , Mh Nassoro Mazrui , lengo ni kudhibiti maambukizi ya wimbi la tatu Bado haijafahamika kama wageni kutoka Tanganyika nao watahusishwa au la . Chanzo : ITV ==== WANAOINGIA ZANZIBAR SHURTI CHETI CHANJO YA COVID-19...
  3. Analogia Malenga

    Cuba yasema chanjo yake ya COVID-19 inayoitwa Abdala ina ufanisi wa 92.28%

    Mamlaka za Cuba zimesema majaribio ya Chanjo ya COVID-19 iitwayo Abdala yameonesha kuwa na ufanisi wa 92.28% Chanjo ya Abdala inakamilika baada ya mtu kupata jumla ya dozi tatu. Takriban Raia Milioni moja Nchini Cuba wameshapata Chanjo ====== Cuba said on Monday that its three-shot Abdala...
  4. Lavan Island

    Chanjo ya Covid19 inaletwa lini? Gharama za kupima zipo juu mno tunashindwa kusafiri nauliza

    Jamani nauliza hapa nchini kwetu ule mpango was kupewa chanjo umeishia wapi sisi wengine tunahitaji maana in wasafiri gharama za kupima zimekuwa kubwa mno kiasi kwamba kila nikipata kazi online nakwama kupima sababu sina dola mia.
  5. beth

    Rais wa Ufilipino atishia kuwafunga wananchi wanaokataa chanjo ya COVID-19

    Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino ametishia kuwafunga jela watu watakaokataa kupata Chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19 wakati Taifa hilo likipambana na mlipuko mbaya zaidi Barani Asia Kufuatia Ripoti za idadi ndogo ya wanaojitokeza katika Vituo mbalimbali vya Chanjo Jijini Manila, Rais amesema...
  6. Analogia Malenga

    Benki ya Dunia (WB) yapanga kuwapa chanjo 60% ya Waafrika mwaka 2022

    Benki ya Dunia(WB) inashirikiana na Umoja wa Afrika (AU) walikutana Juni 21 kujadiliana namna ya kupambana na wimbi la tatu la #COVID19 Mpango wa WB ni kusaidia Afrika kununua na kuzigawa dozi za Virusi vya Corona ambapo hadi sasa nchi 35 zimeshaanza mchakato, na wanatarajia kuzifikia nchi 50...
  7. L

    Chanjo ya COVID-19 kwa wafanyakazi wa Mashirika ya Kimataifa yaliyoko nchini iratibiwa na nani?

    Baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasani kuruhusu chanjo ya COVID-19 nchini baada ya kushauriwa na watalaamu wetu, na kwamba mashirika ya kimataifa yalioko hapa nchini yanaruhusiwa kufanya chanjo hiyo kwa wafanyakazi wake. Sasa kitu ambacho sijakielewa/Sikifahamuni kuwa je ni hospitali gani...
  8. Analogia Malenga

    WHO kuanzisha kituo cha chanjo za Covid19 Afrika Kusini

    Shirika la Afya Duniani(WHO) limetangaza kuanzisha kituo cha kutengeneza chanjo za #COVID19 zinazotumia mRNA Afrika Kusini Kituo hicho kitasaidia kuwapa utaalamu na leseni kampuni za Uchumi wa Kati na Chini kuzalisha chanjo hizo Hadi sasa chanjo zinazotumia mRNA ni Astrazeneca na Moderna...
  9. beth

    Qatar yasema watakaopata Chanjo pekee ndio wataruhusiwa kushuhudia Kombe la Dunia

    Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Khalid bin Khalifa bin Abdulaziz Al Thani, amesema watu waliopata Chanjo dhidi ya COVID19 pekee ndio wataruhusiwa kushuhudia Kombe la Dunia mwaka 2022. Taifa hilo limesema lipo katika majadiliano ili kupata Dozi Milioni 1 ili kutoa Chanjo kwa baadhi ya watu...
  10. beth

    Uturuki yapokea dozi Milioni 5 za Chanjo ya Sinovac kutoka China

    Uturuki imepokea Dozi Milioni 5 za Chanjo ya Sinovac inayotengezwa China huku Rais wa Taifa hilo, Tayyip Erdogan, akielezea matumaini ya kuinuka tena kwa Sekta ya Utalii Sekta hiyo imekumbwa na mdororo kutokana na vizuizi katika safari za kimataifa lakini inaweza kuimarika ikiwa kasi ya Chanjo...
  11. K

    Utaratibu wa chanjo usisubiri! Uanze sasa

    Nashauri kwa wale Watanzania watakaotaka kufanyiwa chanjo serikali iweke utaratibu na isisubiri mpaka wapate hizo chanjo. Mfano wazee wa wahudumu wa afya wako hatarini zaidi basi waambiwe mapema utaratibu mfano kama vitambulisho vya taifa vitatumika ni vizuri wakajua mapema. Lakini vilevile...
  12. M

    London: Maelfu waandamana dhidi ya chanjo ya Corona, uvaaji wa barakoa na lockdown

    Upinzani dhidi ya chanjo ya corona ñi mkubwa mno huko nchi za magharibi japo serikali zao huwa hazitangazi. Angalia maelfu wanavyoandamana mjini London. Huko watu wengi wamechanjwa na madhara yake wameyashuhudià. Halafu hapa anatokea mtu na kudai hakuna madhara!
  13. Roving Journalist

    Chanjo za Kupambana na Corona (COVID-19): Nini Maoni na Mtazamo wako?

    Je, COVID-19 ni nini? COVID-19 ni maambukizi yanayosababishwa na virusi vya Corona, virusi hivi ni sawa sawa na vile vinavyosababisha mafua ya kawaida tofauti na mafua, virusi vya corona vinaweza kuambukiza mwingine kabla hata ya huyo mtu hajaanza kuonesha dalili. Tofauti ni kwamba, watu wenye...
  14. beth

    Shirika la Afya (WHO): Kasi ya usambaaji wa Virusi vya Corona ni kubwa kuliko ya ugawaji Chanjo

    Shirika la Afya Duniani limeonya kuwa kasi ya COVID-19 ni kubwa kuliko ile ya mgawanyo wa Chanjo, ikisema ahadi ya Mataifa ya G7 kutoa dozi Bilioni moja Nchi masikini haitoshi kwani uhitaji ni mkubwa. WHO imesema zaidi ya 10,000 wanapoteza maisha kila siku na Jamii hizo zinahitaji Chanjo hivi...
  15. Mpinzire

    Ni nani aliruhusu watu wachomwe chanjo ya Ukimwi mwaka 2000?

    Ni nani aliruhusu Watanzania 64 wafanyiwe majaribio ya dawa ya Ukimwi ya Virodene kati ya mwaka 2000 na 2001 licha ya Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kutotoa kibali? Je, Watanzania hawa walipewa taarifa sahihi na za kutosha kabla ya kuruhusu miili yao itumike katika...
  16. Analogia Malenga

    CDC wakutana kujadili kesi za kuvimba moyo za waliopata chanjo ya Moderna na Pfizer

    Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) kimepanga kikao cha dharura Juni 18, 2021 ili kujadili waliopata chanjo ya ~COVID19 ya Pfizer na Moderna ambao wamevimba moyo Watu 226 wameripotiwa kuwa na tatizo la myocarditis a pericarditis baada ya kupata chanjo. Wengi wameripotiwa kupona lakini...
  17. TheDreamer Thebeliever

    Hali ni tete Uganda, Corona yashika kasi tena kupelekea shule kufungwa. Rais Samia Hassan aharakishe chanjo

    Habari wadau..! Taarifa zinasema hali ya uviko 19 nchini Uganda imezidi kushika kasi kwa siku wanareport wagonjwa 500. Shule zimeanza kufungwa tena vifo vimeongezeka maradufu katika hii phase ya pili ya Corona nchini Uganda. Kwa niaba ya watanzania wazalendo naomba mheshimiwa rais Samia Hassan...
  18. J

    Serikali: Chanjo ya Corona iliyoruhusiwa ni kwa wafanyakazi wa Balozi na taasisi za nje, kwa Watanzania bado hatujaamua

    Msemaji mkuu wa serikali Mh Gerson Msigwa ametolea ufafanuzi tangazo la serikali linalohusu chanjo ya Corona. Msigwa amesema chanjo iliyoruhusiwa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa balozi na taasisi za kigeni tu. Kuhusu chanjo ya Corona kwa wananchi serikali itafanya uamuzi baada ya kupitia kwa...
  19. Analogia Malenga

    Benki ya Dunia yajizatiti kusaidia nchi masikini kupata chanjo

    Benki ya Dunia (WB) imesema inasaidia nchi zinazoendelea katika zoezi zima la kupata na kutoa chanjo ya COVID19 Pia itasaidia kuimarisha mifumo ya utoaji chanjo na kuhakikisha utoaji chanjo kwa watu walioko katika hatari zaidi ya kupata maambukizi Wamesisitiza kuwa hakuna atakayebaki salama...
  20. Analogia Malenga

    DRC yakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi ya Virusi vya Corona

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizo ya corona, na huku kitovu kikiwa katika mji mkuu, Kinshasa, ikiwa ni moja ya miji yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, Waziri wa Afya Jean-Jacques Mbungani alisema Alhamisi. Kwa mujibu wa shirika la habari la...
Back
Top Bottom