Wazo: Tanzania Ishirikiane na Cuba kwenye Suala la Chanjo

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
1625023245780.png

Mojawapo ya mijadala mikubwa si kwa Tanzania tu bali hata nchi nyingine ni suala hili la chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19. Nchi mbalimbali zimejaribu na zile tajiri zimefanikiwa kwa haraka kujitengenezea chanjo zao na kujinufaisha wao wenyewe kwanza kabla ya wengine. Cuba ni miongoni mwa nchi zinazojitegemea kwa kiasi kikubwa sana linapokuja suala la afya na utaalamu wa tiba.

Kujitegemea huku kumeifanya Cuba kuwa miongoni mwa taifa yaliyofanikiwa sana linapokuja suala la tiba na afya. Kwenye suala la corona Cuba iliamua kutumia uwezo wake wa ndani wa kupambana na gonjwa hili na hili limekuwa kweli pia katika chanjo.

Nimefuatilia toka mwanzo walipoanza kutanganza kuwa wanatengeneza chanjo yao wenyewe Soberana 2. Serikali yao imetangaza jana kuwa tayari chanzo yao inaenda kufanyiwa majaribio ili kupima usalama wake na uwezo wake (safety and efficacy) katika kupambana na virusi vya corona. Wamesema wanaenda kujaribu kati ya watu wenye umri wa miaka 2-18. Ikumbukwe hii chanjo ni kwa ajili ya vijana na watoto. Kwa watu wazima Cuba inatumia chanjo iitwayo Abdala ambayo inaonesha mafanikio ya karibu asilimia 92 (inakaribiana na zile za Pfizer, Moderna na Astrazeneca na hata Sputnik ya Warusi.

Kutokana na ushirikiano wetu na udugu wa kihistoria kati ya Tanzania na Cuba; serikali ione jinsi gani inaweza kuzungumza na Cuba kuruhusu majaribio ya chanjo yao na endapo inafanya kazi ipasavyo kutumia njia hiyo badala ya kutumia njia ya COVAX na mitego mingine ambayo inaacha maswali kama ni suala la afya au ni mtaji fulani.

Kama tuna lengo la kuwalinda Watanzania tuone namna ya rahisi na salama zaidi kwa kushirikiana na Cuba. Na nina uhakika Cuba hawatochukua muda mrefu kushirikiana naasi hata kuzalisha chanjo hiyo hapa hapa nyumbani na kuwa namna ya kusaidia chanjo kwa bara letu badala ya kuwasubiri wakubwa watuamulie.

Ni wazo tu. Hakuna kujitegemea kwa maana zaidi kama kule kwa mawazo. Vinginevyo, wakubwa hawa watatubana na hatutajua nini... si tuna msemo "rafiki wakati wa shida..." Ninajua kuna masuala ya vikwazo vya kiuchumi ambavyo vimewekwa na wakubwa uhusiana na Cuba... tuna uthubutu wa kushirikiana nao licha ya vikwazo?

Habari zaidi:

Hiyo chanjo ya Cuba (Abdala) haijathibitishwa na WHO. Hivyo hata ukichanjwa huwezi kuhesabika kama umepata chanjo. Pia hata hizo chanjo common 3 zinazotambulika Kuna ambazo zimepigwa pini kwa baadhi ya nchi. Haswa chanjo zinazotengenezwa India zimeanza kufanyiwa figisu.

Politics vaccination. Ukweli mchungu ni kwamba, hatuwezi kuwapiga "denge" itafika Mahali tu njia zitakutana na tutatii.
 
Wazo zuri,

Lakini ukifuatilia mienendo na kauli za serikali ya JMT, ni kama tayari imeshajiweka kwenye targets za 'mabeberu'.

Wameanzia mbaaaali kuwalainisha wananchi kwa kauli na vitendo kadha wa kadha ikiwemo kuunda kamati/jopo la 'wataalamu' (wale ni washauri tu)
 
Tunatakiwa kuachana na mawazo ya kijamaa-jamaa eti ndugu wa kihistoria na kupenda vya bwerere. Kubwa zima kutaka kudoea Chanjo ya mtoto, kusingizia urafiki wa kihistoria.

Ni bora kuenda na hizi chanjo za 'mabeberu' kwa sababu zipo sokoni kwa muda kidogo kuliko za Cuba hivyo tumeweza jua vizuri madhara yake na ufanyaji wao kazi kuliko kurukia kitu kigeni kabisa. Mambo mengine ya kusema mitego nk ni paranoia zisizo na mashiko.
 
Hiyo chanjo ya Cuba (Abdala) haijathibitishwa na WHO. Hivyo hata ukichanjwa huwezi kuhesabika kama umepata chanjo. Pia hata hizo chanjo common 3 zinazotambulika Kuna ambazo zimepigwa pini kwa baadhi ya nchi. Haswa chanjo zinazotengenezwa India zimeanza kufanyiwa figisu.

Politics vaccination.. Ukweli mchungu ni kwamba, hatuwezi kuwapiga "denge" itafika Mahali tu njia zitakutana na tutatii..
Huu ndo uthibitisho kuwa hii Covid-19 iko kisiasa na kibiashara zaidi.

Wamekaa kusikilizia nani yuko tayari kwa chanjo halafu wanaanza kupangana Ikulu

Wazo la kushirikiana na Cuba ni zuri sana. Lakini ili kuepuka madhara ya ushirikiano huo inatakiwa nchi nyingi kuwa pamoja

Kwa mfano, AU wakiweka azimio la pamoja kwamba nchi zao zote zijitegemee katengeneza chanjo zao na Kama ni msaada hizi nchi kubwa zitoe ufadhili kufanikisha chanjo.
 
Huu ndo uthibitisho kuwa hii Covid-19 iko kisiasa na kibiashara zaidi.

Wamekaa kusikilizia nani yuko tayari kwa chanjo halafu wanaanza kupangana Ikulu.
Tatizo hao tunaotaka kuwakwepa ndio wameweka na kushikilia misingi na mifumo ya kila kitu kwenye maisha yetu. Kuwakwepa ni impossible.

Lazima kuwa realistic kidogo ili kuelewa. Tukiwa na chanjo yetu Afrika chini ya mwavuli wa AU ni sawa, lakini vipi WHO wasipoipitisha? Tutaweza kwenda nchi hizo kubwa kwa vyeti vya chanjo ambazo hazijathibitishwa?

Tukisema watupe msaada wa kutuwezesha si ndio yale yale tu? Msaada gani utakuja bila masharti? Kuna mikataba na organization nyingi tu tumejiunga zinatumiwa kufanikisha ajenda zao. Ni ngumu sana kuwakwepa hawa.

Jambo la msingi ni kujifunza kuogelea katikati ya bwawa la nyangumi bila kuliwa, sio kukimbia maana hata ukikimbia you won't survive long.
 
Hiyo chanjo ya Cuba (Abdala) haijathibitishwa na WHO. Hivyo hata ukichanjwa huwezi kuhesabika kama umepata chanjo. Pia hata hizo chanjo common 3 zinazotambulika Kuna ambazo zimepigwa pini kwa baadhi ya nchi. Haswa chanjo zinazotengenezwa India zimeanza kufanyiwa figisu.

Politics vaccination. Ukweli mchungu ni kwamba, hatuwezi kuwapiga "denge" itafika Mahali tu njia zitakutana na tutatii.
Siumeambiwa, kutokumbaliwa ni mikakati ya kibiashara iliwekwa na mataifa makubwa.
 
Siumeambiwa, kutokumbaliwa ni mikakati ya kibiashara iliwekwa na mataifa makubwa.
Ndio hivyo mkuu, na ndio maana nikasema mfano India wanatengeneza chanjo kama hizo hizo za mabeberu lakini mabeberu wamezuia watu waliopata chanjo ya India. Hawaitambui.

Sasa jambo la kujiuliza tutaweza kuishi bila hao mabwana? Ni lazima tuombe usaidizi wa fedha au rasilimali watu ili kujikwamua.. Sasa tutaweza kupata usaidizi bila masharti? Cuba yenyewe iko strong kiuchumi kiasi cha kuweza kutusaidia 100%?
 
Hivi mfano, Africa ikaagiza chanjo kutoka India. halafu wao si hawaitambui chanjo ya mhindi, nasi useme. Umoja wa ulaya hakuna kuingia Africa, hawatalegeza masharti?
 
Hivi mfano, Africa ikaagiza chanjo kutoka India. halafu wao si hawaitambui chanjo ya mhindi, nasi useme. Umoja wa ulaya hakuna kuingia Africa, hawatalegeza masharti?
Ikitokea reciprocation unadhani upande upi utaumia zaidi? Nchi kubwa zinazojitegemea almost kwa kila kitu zikiwekewa vikwazo Zina suffer.. Vipi kwetu sisi?

Wote tunategemeana ila Kuna upande mizani imelala zaidi. Hivyo lazima kupangilia karata vizuri.
 
Nazani wao ndio wanatutegemea zaidi, ila sisi uwezo wetu wa kufikiri ndio una shida!! maana karibu kila kitu wanakitoa kwetu!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom