SI KWELI Odemba apokea fungu la fedha kuichafua CCM

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
UOVU WA ODEMBA WAMBAINIKA!

Anatumika na Ubalozi wa Marekani nchini kutaka kuchafua taswira ya Viongozi wa CCM.

Odemba ameweka mapenzi ya upinzani mbele kuliko kazi yake!

Wachambuzi wadai odemba anapaswa kuomba radhi kwa jamii kutokana na uongo aliozusha juu ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi.

1725351772319-jpeg.3085645

Tunachokijua
Edwin Odemba Maarufu kama Chief Odemba ni Mtangazaji wa kipindi cha Medani za Siasa(Kuu) kupitia Star TV.

Mnamo 27, 08, 2024, Chief Odemba aliweka chapisho mtandaoni lililoeleza kuwepo kwa mdahalo wa Makatibu wakuu wa vyama vya Siasa Tanzania (Soma hapa) ambao ulipangwa kufanyika 31,08,2024 saa 3:30 mpaka saa 5:30 usiku siku ya jumamosi katika ukumbi wa New Library ya chuo kikuu cha Dar es salaam mjadala.

Ilipofika 31, 08, 2024 muda ambao ulipangwa kunza kwa mdhalo Odemba alitangaza kuwa katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Emmanuel Nchimbi hakuwa amefika kwenye ukumbi wa Mdahalo hali iliyopelekea makatibu wengine wa vyama vya siasa nao kuamua kutoendelea na mdahalo huo.

Mara baada ya tukio hilo limeonekana gazeti mtandoni linalodaiwa kuwa ni gazeti la Mwananchi la 03/09/2024 ambalo linadaiwa kuchapisha taarifa inayosomeka, SIRI YA ONDEMBA, MAREKANI KUMCHAFUA NCHIMBI YAVUJA.
1725351772319-jpeg.3085645

Je, ukweli ni upi?
Jamiicheck imefuatilia taarifa hiyo na kubaini haina ukweli kwani gazeti la Mwananchi la 03/09/2024 linalodaiwa kuchapisha taarifa hiyo halina chapisho hilo katika ukurasa wa mbele juu kushoto kama ambavyo taarifa zenye madi zinaokena kuwapo bali kuna taarifa inayosema Kauli za DC aliyeenguliwa zazua mjadala mkali, (Tazama hapa)

1725350781309-jpeg.3085638
Aidha katika gazeti linaloonekana mtandaoni linalomtuhumu Odemba limeelekeza taarifa hiyo inapatikana ukurasa wa 3 wa gazeti hilo, Jamiicheck imetazama ukurasa wa 3 wa Gazeti la Mwananchi na kuthibitisha kutokuwepo kwa taarifa hiyo bali kuna taarifa zinazomuhusu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido Marko Henry Ng'umbi. (Tazama hapa).
1725349853270-png.3085621
Kwa mantiki hiyo gazeti hilo linalodai Siri ya Odemba, Marekani kumchafua Nchimbi yafichuka si gazeti la Mwananchi bali taarifa ya Marko Ng'umbi imehaririwa na kutolewa kwenye gazeti la Mwananchi na kupachikwa hiyo tuhuma dhidi ya Odemba ili kuzusha.

Pia, Mwananchi kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii, wamechapisha taarifa ya kukanusha kuhusika na taarifa hiyo inayomtuhumu Odemba. (Tazama hapa)
UOVU WA ODEMBA WAMBAINIKA!

Anatumika na Ubalozi wa Marekani nchini kutaka kuchafua taswira ya Viongozi wa CCM.

Odemba ameweka mapenzi ya upinzani mbele kuliko kazi yake!

Wachambuzi wadai odemba anapaswa kuomba radhi kwa jamii kutokana na uongo aliozusha juu ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi.
Mmekimbia mdahalo nyie hamna kitu, acheni kutafuta visingizio vya kipumbavu!
 
UOVU WA ODEMBA WAMBAINIKA!

Anatumika na Ubalozi wa Marekani nchini kutaka kuchafua taswira ya Viongozi wa CCM.

Odemba ameweka mapenzi ya upinzani mbele kuliko kazi yake!

Wachambuzi wadai odemba anapaswa kuomba radhi kwa jamii kutokana na uongo aliozusha juu ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi.
Rubbish!
 
ODemba ni tapeli sana
 
Hatari sana
Bado mnatumiaga hizi propaganda za kizee kujificha kwenye aibu? Yaani balozi wa Marekani aichafue ccm kwa kumtumia Odemba?! Marekani iache kudeal na vita vya Israel na Ukraine, ije ipoteze muda na chama kinachokaa porini ili wagombea wake wapite bila kupingwa?
 
UOVU WA ODEMBA WAMBAINIKA!

Anatumika na Ubalozi wa Marekani nchini kutaka kuchafua taswira ya Viongozi wa CCM.

Odemba ameweka mapenzi ya upinzani mbele kuliko kazi yake!

Wachambuzi wadai odemba anapaswa kuomba radhi kwa jamii kutokana na uongo aliozusha juu ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi.
Mshaanza kumtafutia zengwe
 
CCM na Polisi hawatofautiani kwa utunzi wa mistari, aliyealikwa ni Nchimbi si CCM na ndiye alitakiwa ashiriki mdahalo, ukweli alisepa, na Kikwete ilimtokea hivyo.
CCM achaneni na propaganda za kichina, hata wachina walikwisha ziacha.
 
Utamaduni wa CCM kukimbia midahalo haujaanza leo!

Anatakiwa mwenyekiti wa chama atakae ondoa hii tabia!!
Inasikitisha sana!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom